Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akishiriki ujenzi wa majengo ya Shule ya Sekondari ya Unyianga, Singida jana, ikiwa ni shamrashamra ya maadhimisho ya miaka 39 ya kuzaliwa CCM yatakayofanyika kitaifa mkoani Singida kesho.
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akishiriki kupalilia katika shamba la mtama la mkulima wa kujitegemea Elisha Mdaa (kushoto) katika Kata ya Mtamaa, Singida jana, ikiwa ni shamrashamra ya maadhimisho ya miaka 39 ya kuzaliwa CCM yatakayofanyika kitaifa mkoani Singida kesho. Kauli mbiu ya maadhimisho hayo ni kuhimiza wananchi kuchapa kazi.
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akimkabidhi kadi ya uanachama wa Umoja wa Wanawake wa CCM (UWT), Hawa Mtipa wakati wa mkutano na Wajasiriamali uliofanyika katika ukumbi wa Jengo la CCM Mkoa wa Singida jana, ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 39 ya kuzaliwa CCM yatakayofanyika kitaifa kesho mjini Singida.
Ofisa Biashara wa Manispaa ya Singida, Erick Sinkwembe akitoa maelezo kwa Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana katika mkutano wa Wajasiriamali wa manispaa hiyo, kuhusu uendeshaji wa mafunzo kwa waendesha Bodaboda pamoja na utekelezaji wa sheria mbalimbali za kodi ambazo mara nyingine si rafiki kwa wajasiriamali. Mkutano huo ulifanyika katika Jengo la Ofisi ya CCM ya Mkoa huo jana.

No comments:
Post a Comment