![]() |
Aaliyekuwa Waziri katika
serikali ya awamu ya kwanza hadi ya nne na Mbunge wa Jimbo la Mufindi Kaskazini
kwa miaka 35, Joseph Mungai.
|
Naibu Waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Ustawi wa Jamii,
Jinsia, Wazee na Watoto , Dk Hamis Kigwangalla akiwa na Mbunge wa Jimbo la Mafinga Mjini, Cosato
Chumi wakati wa ziara yake.
Taarifa
ya kurejeshwa kwa eneo hilo lililopo nyuma ya hospitali hiyo liyopo mjini
Mafinga, wilayani humo ilitolewa na Mkuu wa Wilaya ya Mufindi, Jowika Kasunga
kwa Naibu Waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Ustawi wa Jamii,
Jinsia, Wazee na Watoto kya Tatu, Dk Hamis Kigwangalla alipotembelea hospitali
hiyo juzi.
Akizungumzia
mipaka ya kiwanja cha hospitali hiyo baada ya waziri huyo kutaka kujua kama
haijakumbwa na uvamizi kutoka kwa wananchi, Kasunga alisema; “sehemu ya eneo la
hospitali hii ilikuwa na mgogoro baada ya Mzee Mungai kudai kuimiliki kihalali.”
Alisema
mgogoro huo ambao hata hivyo haukutajwa muda wake, umekwisha baada ya mbunge
huyo mstaafu kurejesha eneo hilo mikononi mwa hospitali hiyo.
Akipokea
taarifa hiyo, Dk Kingwala alitoa siku saba kwa uongozi wa halmashauri ya
Mafinga Mji inayosimamia hospitali hiyo kujenga uzio utakaounganisha uzio wa
hospitali hiyo ili kulinda mipaka yake.
“Pamoja
na kujenga uzio nataka mniletee ofisini kwangu ramani ya eneo zima la hospitali
na taarifa rasmi inayoonesha mgogoro baina yenu na mvamizi huyo umemalizika.
Haya ni mambo ya kisheria, isije ikawa leo mnasema mgogoro umekwisha halafu
kesho tukasikia mzee Mungai kaenda mahakamani,” alisema.
Dk
Kigwangalla alizitaka halmashauri zote nchini kulinda maeneo yake kwa
kuhakikisha yamesajiliwa na yana hati ili inapokuja mipango ya kuboresha au
kutanua matumizi ya eneo kusiwepo na changamoto.
Akizungumzia
huduma hospitali hapo, naibu waziri alisema; “hospitali hiyo ni muhimu katika
eneo hilo lakini hamuipatii kipaumbele. Nimekagua na kujionea hospitali hii,
kuna maeneo ya changamoto. Mfano ni vyumba vyake vya upasuaji, nyie mnaona kama
mnavyo lakini kiukweli ni kama hamna kwani vilivyopo vinafanana na stoo ambacho
sio kipimo chake,” alisema.
Alisema
changamoto zingine katika vyumba hivyo ni uchakavu, havina mgawanyo wa vyumba,
zinavuja, hazina maji, makabati yamechoka na paa lake halina viwango.
Alisema
angetembelea hospitali hiyo kama mkaguzi angelazimika kufunga vyumba hivyo vya
upasuaji visitumike kwasababu ya mapungufu yake.
Alitoa
miezi mitatu kwa mkurugenzi wa halmashauri ya mji wa Mafinga, Shaibu Nnunduma
kukamilisha ukarabati wa vyumba hivyo viwili vya upasuaji ili vikidhi vigezo
vinavyotakiwa vinginevyo mkurugenzi huyo atatumbuliwa jipu.
Aliitaka
hospitali hiyo pia kuanza mara moja ukusanyaji mapato yake kwa njia ya
kielektoniki akisisitiza kwamba njia hiyo inapunguza mianya ya upotevu wa fedha
zinazokusanywa.
Ili
maagizo hayo yatekelezwe kwa ufanisi Mbunge wa Jimbo la Mafinga Mjini, Cosato
Chumi alimuomba waziri huyo kuangalia uwezekano wa wizara yake kuwasaidia
kuboresha hospitali hiyo ambayo kwasasa inasimamiwa na halmashauri mpya ya
Mafinga Mji badala ya halmashauri ya wilaya ya Mufindi.
“Mheshimiwa
waziri halmashauri hii iliundwa Julai mwaka jana, imetokana na halmashauri ya
Mufindi; bado haiko sawa kiutendaji na kimapato. Kwahiyo kuna mapato
tunaitegemea mpaka sasa halmashauri mama ambayo wakati mwingine inatoa kama
hisani tu,” alisema.
Akitoa
mfano Chumi alisema zinaweza kuja Sh Milioni 17 kwa ajili ya sekta hiyo ya
afya, lakini halmashauri yao pamoja na kubeba mzigo mkubwa wa kuhudumia
hospitali hiyo ya wilaya inapata mgao wa Sh Milioni 3 tu.
Akiahidi
kuyafanyia kazi maelekezo ya waziri huyo, mkurugenzi wa halmashauri hiyo
alisema utekelezaji wake utanza mara moja wiki hii.


No comments:
Post a Comment