Naibu waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (watu wenye ulemavu), Dkt Abdallah Possi
akizungumza na Wamiliki na wahariri wa vyombo vya habari leo ofisini kwake
Jijini Dar es Salaam. (Picha zote
na Raymond Mushumbusi)
Mhadhiri toka Chuo Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam Shule ya Uandishi wa Habari Dkt.
Harub Riyoba (katikati) akimsikiliza Naibu waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Watu
wenye Ulemavu) Dkt Abdallah Possi alipokutana na Wamiliki wa Vyombo vya
habri kulia ni Mkurugenzi wa Uendeshaji toka Azam Media Yahya Mohamed na
kushoto ni Meneja wa Uendeshaji toka Sahara Media Steve Diallo.
Na
Joseph Ishengoma
NAIBU Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Watu wenye Ulemavu)
Dkt Abdallah Possi ameviagiza vyombo vya habari nchini kuwa na sera katika
vyombo vyao inayojumuisha uandishi wa habari chanya kwa watu wenye ulemavu.
Akitoa
agizo hilo mbele ya wamiliki wa vyombo vya habari leo Ofisini kwake Jijini Dar
es Salaam Waziri Possi amesema habari nyingi zinazohusu watu wenye ulemavu ni
za kuwanyanyapaa na kuonesha kuwa hawana uwezo wa kufanya mambo chanya.
“Wekeni
kipengele katika sera zenu kitakachosaidia kuwaelimisha watu kuwa watu wenye
ulemavu ni sehemu ya jumuiya katika maisha ya kila siku ya wanadamu,” amesema.
Kwa
mujibu wa Waziri Possi, vyombo vya habari vikiwa na sera iliyowazi na
kuitekeleza, watu watabadilika na kupata taarifa nzuri za watu wenye ulemavu.
Dkt.
Possi ameeleza kuwa taarifa za watu wenye ulemavu hazitakiwi kuwa na lugha
zenye chembechembe za kunyanyapaa.
Amesema
kuwa kila kituo cha televisheni kinatakiwa kuwa na wataalamu wa kutafsiri
habari na vipindi muhimu kwa lugha za alama.
Amesema,
“Serikali kwa kutumia Sheria ya Watu wenye ulemavu Na. 9 ya mwaka 2010 inaandaa
tangazo kuvikumbusha vyombo vya habari kuwa kuwa na wataalam wa kutafsiri
habari na vipindi muhimu kwa lugha za alama kwa watu wenye ulemavu.”
Aidha
Naibu Waziri amewaagiza wamiliki wa vyombo vya habari kutoa ajira kwa watu
wenye ulemavu kwani Sheria inaagiza lazima chombo chochote chenye wafanyakazi
zaidi ya 20, angalau mfanyakazi mmoja awe mtu mwenye ulemavu.
Kwa
upande wao wamiliki wameiomba serikali kutotoza kodi tangazo lolote linalohusu
habari chanya za watu wenye ulemavu.
Hata
hivyo wamiliki hao wamemweleza Naibu Waziri kuwa ubadilishaji wa Sera pamoja na
kuwa na wataalam wa kutafsiri habari na vipindi muhimu kwa watu wenye ulemavu
ni jambo zuri, lakini wanahitaji kupewa muda wa maandalizi.

No comments:
Post a Comment