TANGAZO


Tuesday, February 16, 2016

Boutros Boutros Ghali aaga dunia

Image captionBoutros Boutros Ghali
Aliyekuwa katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Boutros Boutros Ghali amefariki akiwa na umri wa miaka 93.
Kifo chake kilithibitishwa na Rafael Dario Ramirez Carreno,rais wa baraza la usalama katika umoja wa mataifa.
Akiwa raia wa Misri,bwana Ghali alikuwa mwarabu wa kwanza kushikilia wadhfa huo wa Umoja wa Mataifa.
Alichukua wadhfa huo mwaka 1992 kutokana na ushawishi kufuatia msimamo wake katika vita vya Ghuba,akishikilia kwa kipindi kimoja cha miaka mitano.
Baraza hilo la usalama lenye wanachama 15 lilinyamaza kwa dakika moja ili kutoa heshima yake.

No comments:

Post a Comment