Kundi la kislamu la Islamic State limesema lilitekeleza mashambulizi katika mji mkuu wa Syria Damascus na mji wa Homs, ambao uliwauwa watu 140.
- Mashambulizi ya mabomu manne kusini mwa Damascus eneo la ,Sayyida Zeinab yaliwauwa watu 83, shirika la habari la taifa hilo limesema.
Mapema huko Homs watu 57 , wengi wao raia waliuwawa katika mashambulizi mawili ya magari, Kulingana na ripoti za makundi yanayofuatilia habari za nchi hiyo.
AFP
Mashambulizi hayo mawili ya Jumapili yalilenga maeneo yaliozingirwa na waislamu wachache, kama inavyosemekana na kundi la waislamu la Sunni la IS.
Mashambulizo hayo yalitokea baada ya rais Bashar Al – Assad kutoa ripoti kuhusu wakimbizi wa Syria kutoogopa kurudi makao.
Bwana Assad ambaye analaumiwa kwa kuwakandamiza watu wake, aliwaambia waSyria waliokuwa wamehama kutokana vita wasiwe na uoga wowote wa kurejea makwao na kuwa serikali ingewahakikishia usalama.
‘Tunataka watu warudi Syria,’aliambia wanahabari.
Getty
Zaidi ya raia 250,000 kutoka Syria wameuwawa katika mashambulizi.
Wengine milioni 11 wamehamishwa makwao.
Milioni 4 kati yao walihamia nje ya nchi wakijumuisha wale wanaosafiri safari kwenda ulaya.


No comments:
Post a Comment