TANGAZO


Monday, February 29, 2016

UNCDF yawakutanisha wataalamu wa fedha kutoka nchi mbalimbali kujadili jinsi ya kuleta maendeleo kwa kutumia vyanzo vya ndani

Mkurugenzi wa Maendeleo ya Fedha wa Umoja wa Mataifa (UNDCF), David Jackson, (kulia), akitoa mada kwenye mkutano wa siku mbili wa wataalamu wa fedha na wadau wa maendeleo 62 kutoka nchi mbalimbali Duniani, kwenye hoteli ya Hyaatt Regency, Kilimanjaro jijini Dar es Salaam, Februari 29, 2016. 
Naibu Mkurugenzi Mtendaji Benki ya TIB, Jaffer Machano, akitoa mada kwenye mkutano wa siku mbili wa Wataalamu wa fedha na wadau wa maendeleo 62 kutoka nchi mbalimbali Duniani, kwenye hoteli ya Hyaatt Regency, Kilimanjaro jijini Dar es Salaam, Februari 29, 2016.
 Mtoa Mada, Suzane Ngane kutoka Cameroun,  akitoa mada kwenye mkutano huo.
Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Tawala za Serikali za Mitaa Tanzania (ALAT), Habraham Shemumoyo, kitoa mada kwenye mkutano wa siku mbili wa Wataalamu wa fedha na wadau wa maendeleo 62 kutoka nchi mbalimbali Duniani uliofanyika jijini Dar es Salaam, Februari 29, 2016.

Na Beda Msimbe
WATAALAMU  wa fedha na wadau wa maendeleo 62 kutoka nchi mbalimbali duniani wameanza mkutano wa siku mbili jijini Dare s Salaam kuangalia namna ya  kuwezesha fedha za kusaidia maendeleo endelevu  kwa kutumia vyanzo vya ndani.

Mkutano huo wa siku mbili ulioanza jana katika hoteli ya Hyatt Regency, Kilimanjaro umelenga kuja na maelezo muafaka ya namna ya kupata fedha za kuendesha na kujenga miundombinu mbalimbali kwa ajili ya miji inayotanuka.

Katika mahojiano na mwandishi wa Mo Blog kuhusu mkutano huo , mmoja wa wakurugenzi wa UNCDF kutoka makao makuu anayeshughulikia uendelezi wa fedha, David Jackson alisema kwamba wataalamu walioalikwa wanatarajiwa kutoka na msimamo unahusu uwezeshaji wa fedha wa ndani.

Alisema wakati dunia inakabiliwa na mabadiliko makubwa ya wananchi kutoka vijijini kwenda mijini uwezo wa majiji mengi duniani ikiwamo manispaa ni mdogo kuwezesha kutengeneza miundombinu na pia kuwezesha ajira.

Alisema  kwa sasa kutokana na uwingi wa watu wanaofurika katika miji, halmashauri  na uhaba wa fedha kutoka katika vyanzo vya mapato kumesababisha kushindwa kuendelezwa mifumo endelevu ya miundombinu na ajira na kulazimisha wataalamu kuanza kuangalia namna nyingine ya kupata fedha.

Alisema mpango wa kutafuta vyanzo vingine vya fedha kwa kuunganisha nguvu nje ya mfumo rasmi umewezekana Tanzania hasa kutokana na manispaa kama ya Kibaha kuwezeshwa kupata fedha za miradi mbalimbali na wengine nao watatoa uzoefu wao.

“Zamani ilikuwa rahisi sana kwa manispaa nyingi kutengeneza mipango ya maendeleo, lakini kwa sasa kutokana na uwingi wahamaji vyanzo vya kawaida vimezidiwa na kuonekana haja ya kutafuta vyanzo vingine ili kuwezesha maendeleo na ajira,” alisema Jackson.

Alisema mataifa yanahitaji sasa kuangalia mifumo yao ya kuwezesha maendeleo endelevu kwa kutumia vyanzo vya ndani ambavyo vinawezekana kupatikana.

Aliongeza kuwa miradi mikubwa ya maendeleo haiwezi kufanywa na vyanzo vya zamani na kutolea mfano mradi wa maji wa Abu Dhabi ambao umewezeshwa kwa kutumia vyanzo vya ndani lakini kwa namna ambayo inasaidia mji huo kuwa na maji ya uhakika pamoja na kwamba vyanzo vyake havifai.

Alisema ni matumaini yake kwamba baada ya kusikiliza mada mbalimbali wataalamu hao watakuwa na nafasi ya kutoa tamko la namna bora ya kushirikisha wadau wa maendeleo wa ndani kutengeneza miradi mikubwa ya huduma kwa jamii.

Pia alisema kwamba washiriki katika mkutano huo wa siku 2 ni pamoja na wadau wa maendeleo kutoka Uswisi, Sweden na Denmark wapo pia wataalamu wa masuala ya fedha, miradi kutoka Afrika Kusini, Ethiopia, Benin, Rwanda, Mali, Senegal,Uganda, Msumbiji, india, Bangladesh , Marekani na Tanzania.

Mkutano huo wa mashauriano uliandaliwa na UNCDF ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa azimio la AddisAbaba kuhusu maendeleo endelevu na umuhimu wa kuimarisha uwezo wa kifedha wa manispaa mbalimbali.
Mchumi Daniel Platz kutoka Umoja wa Mataifa akiwasilisha mada kwa wataalamu wa masuala ya fedha na wadau wa maendeleo waliokutana jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Maendeleo ya Fedha wa Umoja wa Mataifa (UNDCF),David Jackson (kulia), akizungumza kwenye mkutano wa siku mbili wa wataalamu wa fedha na wadau wa maendeleo 62 kutoka nchi mbalimbali Duniani, kwenye hoteli ya Hyaatt Regency, Kilimanjaro jijini Dar es Salaam, Februari 29, 2016. Kushoto ni Kaimu Katibu Mkuu, Wizara ya Serikali za Mitaa nchini Uganda, John Genda Walala.
 Washiriki wa mkutano wa kimataifa wa siku mbili wa wataalamu wa masuala ya fedha na wadau wa maendeleo wakifuatilia mada ikliyorushwa kwa njia ya video na Profesa Paul Smoke kutoka Chuo Kikuu Cha New York, nchini Marekani.
 Mchumi, John Boex, akitoa mada kwenye ufunguzi wa mkutano huo wa siku mbili ulioanza Februari 29, 2016
 Kaimu Katibu Mkuu, Wizara ya Serikali za Mitaa nchini Uganda, John Genda Walala, akiongoza mkutano wakati wa asubuhi
Mkurugenzi wa Maendeleo ya Fedha wa Umoja wa Mataifa (UNDCF), David Jackson, (kushoto), akijadiliana jambo na Mkurugenzi wa Mfuko wa Mtaji wa Maendeleo wa Umoja wa Mataifa(UNCDF) nchini Tanzania, Peter Malika.
Mkurugenzi wa Maendeleo ya Fedha wa Umoja wa Mataifa (UNDCF),David Jackson (kulia), akizungumza kwenye mkutano wa siku mbili wa wataalamu wa fedha na wadau wa maendeleo 62 kutoka nchi mbalimbali Duniani, kwenye hoteli ya Hyaatt Regency, Kilimanjaro jijini Dar es Salaam, Februari 29, 2016. Kushoto ni Kaimu Katibu Mkuu, Wizara ya Serikali za Mitaa nchini Uganda, John Genda Walala
 Baadhi yawashiriki wakifuatilia kwa makini yanayoendelea katika mkutano
Mkurugenzi wa Maendeleo ya Fedha wa Umoja wa Mataifa (UNDCF), David Jackson, (kulia), akiwa kwennye mahojiano na Mjumbe kutoka nchini Uganda, Naibu Mkurugenzi wa usimamizi wa mikakati na maendeleo ya biashara, jiji la Kampala, Patrick Musoke, pembezonimwa mkutano wa siku mbili wa wa wataalamu wa fedha na wadau wa maendeleo 62 kutoka nchi mbalimbali Duniani, kwenye hoteli ya Hyaatt Regency, Kilimanjaro jijini Dar es Salaam, Februari 29, 2016.
Wajumbe wakibadilishana mawazo.(Picha zote na Khalfan Said na Geofrey Adroph.)

Wadau wa watakiwa kutoa maoni juu ya Maboresho ya Sera ya Michezo

Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Bibi. Zawadi Msalla( katika) akizungumza na waandishi wa Habari (hawapo pichani) kuhusu wanachi kutoa maoni juu ya Maboresho ya Sera ya Michezo leo jijini Dar es Salaam.Kaimu Mkurugenzi wa Maendeleo ya Michezo Bw. Alex Makoye Nkenyenge na kushoto ni Afisa Uchumi Mwandamizi wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Bw. Richard Kundi.
Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Michezo kutoka Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Bw. Alex Makoye Nkenyenge akizungumza na waandishi wa Habari (hawapo pichani) kuhusu wadau kutoa maoni ili kuboresha Sera ya Michezo leo jijini Dar es Salaam. Katikati ni Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Bibi. Zawadi Msalla na kushoto ni Afisa Uchumi Mwandamizi wa Wizara hiyo Bw. Richard Kundi.
Picha na: WHUSM.

Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo kupitia Idara ya Maendeleo ya Michezo, inapenda kuwafahamisha wananchi kwamba imefanya mabadiliko ya Sera ya Michezo ya mwaka 1995 na sasa itatoa sera mpya ya mwaka 2016 ambayo wadau mbalimbali wameshiriki kwa kutoa maoni yao ili yatumike kuboresha  Sera hii mpya. Wizara kwa mara nyingine tena inategemea kupokea maoni kupitia Tovuti Rasmi ya wananchi ambayo ni www.wananchi.go.tz ambapo rasimu ya Sera hii mpya ya mwaka 2016 inapatikana katika tovuti ya wizara ambayo ni:www.habari.go.tz,na kwa wale wanaoweza kufika ofisini kwetu Golden Jubilee Towers ghorofa ya 8 au kupitia barua pepe ifuatayo, nicholaus bulamile@habari.go.tz.

Maoni hayo yatakuwa yamelenga katika maeneo makuu kumi ambayo ni;
Kuwa na jamii inayoshiriki katika michezo na mazoezi ya viungo vya mwili kwa afya endelevu na msingi wa maendeleo ya michezo. 

Kuwa na wataalamu wa michezo wanaokidhi viwango na mahitaji.
Kuwa na mifumo anuai na thabiti ya uratibu, usimamizi na uendelezaji wa michezo. 
Kuimarisha ajira na mikataba katika michezo.

 Kuwa na uwekezaji unaokidhi mahitaji ya maendeleo ya michezo.
 Kuwa na tafiti endelevu katika michezo.

 Kuwa na mfumo thabiti wa utoaji huduma za bima, kinga, tiba na uthibiti wa matumizi ya dawa na mbinu haramu katika michezo.

Kuwa na maendeleo endelevu ya utalii wa michezo.

 kuwa na mfumo shirikishi wa utoaji wa habari za michezo.
 Kuwa na utaratibu wa kumlinda mwanamichezo dhidi ya maambukizi ya VVU na UKIMWI.

Wizara inapenda kutoa wito kwa wadau wote washiriki kutoa maoni yao yenye tija ambayo yataboresha Sera ya maendeleo ya Michezo ya mwaka 2016. Ukusanyaji wa maoni utaanza leo tarehe 29 Februari hadi tarehe 5 Machi 2016.

Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini,​
Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Said Sadiki azindua duka la Huawei jijini


 Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Saidi Meck Sadiki akizungumza na waandishi wa habari juu ya ufunguzi wa duka la simu za mkononi na huduma za matengenezo ya simu Samora jijini Dar es Salaam. Wananchi wametakiwa kutumia simu orijio ili kuepuka usumbufu utakojitokeza kwa kuzimwa kwa simu feki ifikapo June mwaka huu.


Akizungumza jijini Dar es Salaam wakati wa uzindizi wa duka jipya la kampuni ya huwawei mkuu wa mkoa bwana said Meck sadiki amesema kuwa zoezi la uzimaji wa simu hizo uzimaji huo haujaanzia hapa nchini bali limefanyika katika nchi nyingi zilizoendelea.



Aidha Meck Sadick amesema kuwa ni wakati sasa wa makampuni ya simu kuakikisha yanatengeneza simu imara na kuwa na mafundi wa uhakika ili kupunguza usumbufu unaojitokeza kwa wateja wao.


 Meneja Huawei nchini Tanzania Peter Zhangjunliang, akizungumza na wandishi wa habari hawapo picha juu ya mbinu zilizotumika na kampuni ya  Huawei, ambapo wanajitahidi  kuwa Karibu zaidi na wateja wake na kuendeleza zaidi uzoefu katika matumizi ya bidhaa za Huawei. 



"Ili kuwahudumia Zaidi wateja wake Huawei tume fungua Maduka Mapya ya Huawei pamoja na huduma za matengenezo ya simu za mkononi jijin Dar es Salaam,baada ya kuongezeka kwa uhitaji wa bidhaa za Huawei na kuhakikisha kuwa na vifaa vya uhakika na orijino vinapatikana kwa wateja wao kirahisi.jijini Dar es Salaam" amesema Zhangjunliang.


 Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Said Meck Sadiki akipatiwa maelekezo na Meneja Huawei nchini Tanzania Peter Zhangjunliang.


 Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Saidi Meck Sadiki akikata utepe kuashiria uzinduzi wa  duka la simu za mkononi na huduma za matengenezo ya simu , Samora jijini Dar es Salaam.


 Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Said Meck Sadiki akiwa katika picha ya pamoja na uongozi wa Huawei Tanzania.


 Mkurugenzi wa Mawasiliano na Teknolojia, Mh. Peter Philip akizungumza na wandishi wa habari hawapo pichani juu duka la kuwapatia wananchi bidhaa zenye viwango vya uhakika, huduma zilizo bora na pia Huawei wameweza kuenda sambasamba na mabadiliko ya teknolojia hivyo kuwapatia wateja wao simu za mkononi za kisasa,jijini Dar es Salaam.

Mkurugenzi wa Mawasiliano na Teknolojia, Mh. Peter Philip akiwa katika picha ya pamoja na uongozi wa Huawei Tanzania, jijini Dar es Salaam.

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam, 
25 Febuari 2016: 
KAMPUNI ya simu kutoka nchini China ya Huawei, imezidi kutanua wigo wa huduma kwa kuzindua maduka mawili ya simu moja likiwa jengo la JMall na duka la pili lenye Kituo cha huduma ya matengenezo ya simu za mkononi likiwa jengo la NHC karibu na TTCL mtaa wa Samora.

Hii ikiwa ni baada ya kuongezeka kwa uhitaji wa bidhaa za Huawei jijini Dar es Salaam na pia kuhakikisha kuwa vifaa vya uhakika na orijino vinapatikana kwa wateja wao kirahisi.kwa ukaribu zaidi jijini la Dar es Salaam.

Maduka hayo ya Huawei yana mahali husika panapo ruhusu wateja wake kuangalia na kujaribu simu na vifaa vingine vya Huawei. Maduka hayo pia yanatoa nafasi nzuri kwa wateja kupata huduma bora na kuzoea bidhaa za Huawei na hata kwa kujaribu baadhi ya vifaa vyetu vya mtandao vyenye uwezo wa 3G/4G LTE Smartphone.

Maisha ya wateja wetu yana badilika kila siku na matarajio yao ni kuona ubora na ukuaji wa huduma katika kiwago cha juu zaidi. Kama wadau wakubwa Huawei imekuwa ikijitahidi katika kukidhi mahitaji ya kila siku ya wateja na pia kuahidi kuwaonyesha wateja thamani ya pesa yao.

“Dar es salaam kama kitovu katika ukuaji wa uchumi, tunaamini maduka yetu ya simu na pia kituo cha matengenezo ya simu za mkononi yataongeza ufanisi na kusaidia ufikiaji wa huduma za mawasiliano kwa ukaribu Zaidi. Maduka yetu yamejikita katika ubora wa kutoa bidhaa kwa wateja wa rejareja na kuwapa wauzaji uwezo wa kupata vifaa halisi, bora na pekee”.

Alisema Mh Peter Zhangjunliang, Meneja wa Huawei nchini Tanzania aliyasema hayo wakati wa ufunguzi wa vifaa vya Huawei.

Maduka mapya ya Huawei, mbali na uuzaji wa Simu za mkonon , Pia  yatatoa huduma baada ya mauzo wataalam wa mauzo wataweza watatoa msaada wa  kifundi na utumiaji na matengenezo
Katika kusherekea ufunguzi huu wa maduka ya Huawei na kituo cha huduma za simu, Huawei inatoa punguzo la bei kuanzia tarehe 25 mpka tarehe 29 mwezi huu ikiwa pamoja na promosheni za simu zao P8 na G8. Manunuzi ya simu hizi mbili za P8 na G8 yataambatana na zawadi kama selfie stiki, spika za Bluetooth na tisheti.

Huawei Tanzania imejipanga kuhakikisha ina weza kuwafikia wateja wake wote Tanzania kote katika ubora na huduma zenye ufanisi Zaidi.

Maduka yetu yatakuwa yanatoa huduma itakayo fanya manunuzi yako yawe ya kihistoria, pia tupo kwenye msimu wa kuhakikisha uwepo wetu unajulikana Tanzania kwa ujumla kwa kuanza na Dar es salaam” aliongeza meneja wa Huawei nchini.

Maduka hayo yatatoa huduma siku zote za wiki saa 2 asubuhi hadi saa kumi na moja jioni jumatatu hadi Ijumaa na jumamosi yatakuwa wazi kuanzia saa 2 asubuhi hadi saa saba mchana.
Maduka ya Huawei yatakuwa kwa ajili ya kuboresha utumiaji sahihi wa  teknolojia  katika njia sahihi zaidi, Wateja Wote mnakaribishwa,

Kuhusu Huawei
Huawei ni vinara wa teknolojia na mawasiliano hususani katika kutimiza matakwa ya wateja wao, katika kuhakikisha wanawapa wateja wao kile kilicho bora katika viwango vya juu, umuhimu wa mawasiliano na vifaa vya mawasiliano vinatumika katika nnchi Zaidi ya 170 na mikoa yake, Huawei ilishika nafasi ya 228 ulimwenguni kwa mwaka kutokana na mapato yake mwaka 2014 kati ya makampuni 500. Mapato ya kampuni yamefikia kiasi cha dolla za kimarekani bilioni 46.5. Huawei imeshika nafasi ya 3 kwenye usambazaji wa simu kwa mwaka 2015 kwa kusambaza zaidi ya simu milioni 100 duniani kote, Kampuni ya Huawei ipo katika kuhakikisha inatoa ushirikiano katika kukuza na kuboresha vifaa vya mawasiliano  duniani kote.

Kampuni ya Huawei inajihusisha na utengenezaji wa simu za mkononi, huduma za intaneti kwa njia ya modemu na vifaa vya matumizi ya nyumbani.

Huawei imeimarisha mahusiania ya biashara na makampuni kama Tigo, Vodacom, Tigo, Vodacom, Airtel, Zantel, Sasatel, TTCL, SmileCom, Safaricom, MTN, CellC, Telefónica, China Mobile, Vodafone, T-Mobile, BT, China Telecom, NTT Docomo, France Telecom, na China Unicom.
Kupata habari Zaidi tembelea www.huaweidevice.com
Hotuba ya Mkurugenzi wa TEHAMA, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mh. Peter Philip
Uongozi wa Huawei
Wadau mbalimbali wa Huawei
Waandishi wa Habari
Mabibi na Mabwana
------------------------------------------------------------------------------------------------------

Nina furaha kubwa kuwa miongoni mwenu leo pamoja na timu nzima ya Huawei. Katika dunia ambayo teknolojia ya mawasiliano inabadilika kwa kasi kushiriki  katika mabadiliko hayo ya maendeleo ni upendeleo mkubwa.

Mabibi na Mabwana, Christine Qiang mwana Uchumi wa Benki ya Dunia alisema” Wigo wa simu za mkononi unakuwa kwa kasi, ukiwa ni njia moja kuu ya kutanua fursa za kiuchumi na huduma za msingi kwa mamilioni ya watu” Kuunganishwa kupitia Intaneti au simu za mkononi kunaleta taarifa za masoko, huduma za kifedha na huduma za kiafya sehemu za mbali zisizofikika kiurahisi na ina saidia kubadilisha maisha ya watu kwa namna za kipekee.

Mabibi na Mabwana Ningependa kuchukua nafasi hii kuwapongeza Huawei Tanzania kwa hatua hii nzuri katika kuendeleza sekta ya mawasiliano na teknolojia nchini Tanzania.

Sekta ya mawasiliano na teknolojia nchini Tanzania inakua kwa kasi na kuwa moja ya nguzo muhimu katika maendeleo ya kijamii na kiuchumi. Maendeleo haya ya kasi katika mawasiliano na teknolojia yamepelekea wawekezaji Wengi kuwekeza katika sekta hii nchini kwetu. Kwa sasa sekta hii inakua kwa kasi ya asilimia kumi na tano na asilimia ishirini kwa mwaka, kiwango ambacho kinaonyesha kua cha juu katika ukanda wa afrika mashariki.

Nchi Zaidi ya thelathini duniani hutengeneza simu za mkononi, hata hivyo ubora umekua alama ya utofautishaji katika makampuni haya ya simu. Kampuni ya Huawei imethibitisha mara kwa mara uwezo wao katika kuridhisha wateja wao kwa kuwapatia bidhaa zenye viwango vya uhakika, huduma zilizo bora na pia Huawei wameweza kuenda sambasamba na mabadiliko ya teknolojia ivyo kuwapatia wateja wao simu za mkononi za kisasa.

Mabibi na Mabwana

Duka hili jipya na huduma matengenezo ya simu za mkononi la Huawei haliashirii ongezeko katika utajiri au mauzo yao ila inaashiria kutambua mahitaji ya wateja wao na fursa ya kupata bidhaa zenye uhakika na zilizo bora.

Nina Imani kuwa Huawei itaendelea kuwatosheleza wateja wake. Nchi ya Tanzania ni nchi inayokua kwa kasi katika sekta ya teknolojia ivyo natumai na naamini Huawei watatumia fursa hiyo kuongoza soko la simu za mkononi nchini Tanzania.

Mabibi na Mabwana, Kwa mara nyingine nishukuru sana Uongozi mzima na menejimenti ya Huawei kwa kunishirikisha katika tukio hili tunapo fungua rasmi duka la Huawei na huduma za simu hapa J Mall.

Nina uhakika kila mteja atakae pita katika malango haya ya Huawei atapata kumbukumbu njema na mguso wa teknolojia ya uhakika.

Asanteni sana.

Hali ya unyonyeshaji watoto nchini sio nzuri (AUDIO)

IMEELEZWA kuwa wastani wa unyonyeshaji kwa watoto walio chini ya miezi sita nchini sio mzuri na hivyo kuwa na uwezekano wa watoto kudhoofika kwa kukosa maziwa ya mama ambayo yanakuwa na virutibisho muhimu kwa ukuaji ya mtoto.

Hayo yamesemwa na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Chakula na Lishe, Dkt. Joyceline Kaganda katika warsha iliyoandaliwa na UNICEF ili kujadili jinsi uwekezaji mkubwa zaidi katika kunyonyesha maziwa ya mama kunaweza kusaidia maendeleo kiuchumi na kuokoa maisha ya watoto nchini.

Dkt. Kaganda amesema wastani wa unyonyeshaji kwa watoto walio chini ya miezi sita ni asilimia 42 na wastani huo ni mdogo hivyo kuashiria kuwa hali sio njema kwa watoto ambao hawapati maziwa ya mama.

Amesema kiafya inatakiwa mtoto aanze kunyonya nusu saa baada ya kuzaliwa na mtoto anyonye maziwa ya mama yake kwa kipindi kisichopungua miezi sita na baada ya hapo anaweza kuanza kuwa anachanganya na vyakula vingine kama uji na maji.

“Hali sio nzuri ukiangalia wastani wa wamama ambao wanawapa watoto wao maziwa ya kunyonya ni wachache na labda inawezekana wengi wakawa hawatambui matatizo yanayoweza kutokea kama hawatawanyonyesha watoto wao,” amesema Dkt. Kaganda.

Aidha Dkt. Kaganda amesema kazi zinachangia kina mama wengi kushindwa kuwanyonyesha watoto wao lakini wanaweza kuweka utaratibu wa kuwa wanakamua maziwa yao na kuyahifadhi sehemu nzuri ili hata kama wanapokuwa mbali na watoto wao, msimamizi anayemuangalia mtoto aweze kumpa mtoto ili kumfanya apate virutubisho muhimu kutoka kwenye maziwa ya mama yake.

Nae Mwakilisha wa Shirika la Kimataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF) nchini, Bi. Maniza Zaman amesema katika kusaidia Tanzania kuongeza wastani wa watoto ambao wananyonya wamekuwa wakitoa elimu kwa kina mama wanaonyonyesha pamoja na familia zao ili wajue umuhimu wa mtoto kunyonya maziwa ya mama.

Alisema watoto wengi wamekuwa wakipoteza maisha kwa matatizo ambayo yanatokana na kukosa maziwa ya mama zao na hivyo ili kuzidi kushughulikia tatizo hilo wanataraji kuanza kutoa elimu kwa watumishi wa afya katika mikoa ya Mbeya, Iringa na Njombe na wanataraji kutembelea zaidi maeneo ya vijijini kutokana maeneo hayo kuonekana kutokuwa na elimu hiyo zaidi.

“Watoto wamekuwa wakipata matatizo na kupoteza maisha na hiyo inachangiwa na kutokunyonya kwa mama … tumeshirikiana na serikali tunataraji kutoa elimu katika vijiji zaidi ya 15,000 kwenye mikoa ya Njombe, Iringa na Mbeya na tutafundisha pia mama na familia umuhimu wa mtoto kunyonya,” alisema Bi. Zaman.

Alisema baada ya kumalizika kwa mikoa hiyo wataendeleza utoaji wa elimu nchi nzima ili jamii ya Tanzania itambue umuhimu wa watoto kunyonya maziwa ya mama na pia kuwaomba waandishi wa habari kutumia nafasi yao katika jamii ili kuwaelimisha watanzania kuhusu tatizo hilo.

Katika makala zilizoandikwa katika jarida la habari za afya la The Lancet linaonyesha kuwa uboreshaji wa kunyonyesha maziwa ya mama kunaweza kuokoa maisha zaidi ya watoto 820,000 kila mwaka duniani na Dola za Kimarekani Bilioni 302 kila mwaka.
Imendaliwa na Rabi Hume wa Modewjiblog
DSC_0599Mwakilisha wa Shirika la Kimataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF) nchini, Bi. Maniza Zaman akitoa neno la ufunguzi katika warsha iliyoandaliwa na UNICEF ili kujadili jinsi uwekezaji mkubwa zaidi katika kunyonyesha maziwa ya mama kunaweza kusaidia maendeleo kiuchumi na kuokoa maisha ya watoto nchini.(Picha zote na Rabi Hume wa Modewjiblog)
DSC_0630Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Chakula na Lishe, Dkt. Joyceline Kaganda katika warsha iliyoandaliwa na UNICEF akielezea hali ya unyonyeshaji kwa watoto ilivyo nchini.
DSC_0622Baadhi ya wadau wa sekta ya afya waliohudhuria katia warsha hiyo wakifatilia kwa makini ripoti zilizokuwa zikitolewa.
DSC_0654Mshauri Mwandamizi wa maswala ya watoto wadogo na unyonyeshaji kutoka Makao Makuu ya UNICEF, New York, Dr. France Begin akielezea kuhusu makala za The Lancet juu ya uwekezaji mkubwa zaidi katika kunyonyesha maziwa ya mama jinsi kunavyoweza kusaidia maendeleo ya kiuchumi na kuokoa maisha ya watoto nchini.
DSC_0655Mshauri Mwandamizi wa maswala ya watoto wadogo na unyonyeshaji kutoka Makao Makuu ya UNICEF, New York, Dr. France Begin akiwaonyesha wahudhuriaji wa warsha hiyo ripoti ya utafiti uliofanywa na jarida la The Lancet linalohusika na kuandika habari za afya.
DSC_0661Viongozi wa Taasisi mbalimbali waliofika katika warsha hiyo wakifatilia ripoti ya utafiti uliofanywa na jarida la The Lancet. Wa kwanza kulia ni Mkurugenzi Msaidizi Huduma za Lishe katika Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto. Dkt. Vicent Assey, Mkurugenzi Idara ya Uratibu wa Shughuli za Serikali, Ofisi ya Waziri Mkuu,Obey Assery Nkya, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Chakula na Lishe, Dkt. Joyceline Kaganda na Mwakilisha wa Shirika la Kimataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF) nchini, Bi. Maniza Zaman.
DSC_0665Mkurugenzi Idara ya Uratibu wa Shughuli za Serikali kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu, Obey Assery Nkya akielezea hatua ambazo serikali imechukua ili kupunguza idadi ya kina mama ambao hawanyonyeshi watoto.
DSC_0674Viongozi wa Taasisi mbalimbali waliofika katika warsha hiyo wakisikiliza maswali yaliyokuwa yakiulizwa na wadau wa sekta ya afya na waandishi wa habari. Wa kwanza kulia ni Mshauri Mwandamizi wa maswala ya watoto wadogo na unyonyeshaji kutoka Makao Makuu ya UNICEF, New York, Dr. France Begin, Mkurugenzi Msaidizi Huduma za Lishe katika Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto. Dkt. Vicent Assey, Mkurugenzi Idara ya Uratibu wa Shughuli za Serikali, Ofisi ya Waziri Mkuu,Obey Assery Nkya, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Chakula na Lishe, Dkt. Joyceline Kaganda na Mwakilisha wa Shirika la Kimataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF) nchini, Bi. Maniza Zaman.
DSC_0696Mkuu wa kitengo cha fedha na malipo nchini kutoka Benki ya Dunia, Douglas Pearce akiuliza swali katika warsha hiyo.
DSC_0711Mwakilisha wa Shirika la Kimataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF) nchini, Bi. Maniza Zaman akitoa neno la shukrani kuashiria kumalizika kwa warsha hiyo.

Mashindano ya Tigo Kili Half Marathon yafana mjini Moshi



Maelfu ya wakazi wa Moshi na wanariadha mbalimbali wakifuatilia  mashindano ya Tigo Kili Half Marathon  katika mashindano hayo yaliyofanyika jana kwenye viwanja vya chuo cha Ushirika Mjini Moshi.
Wafanyakazi wa  kampuni ya Tigo wakiwa katika picha  ya pamoja  kabla  ya kuanza    mashindano ya Tigo Kili Half Marathon  katika mashindano hayo yaliyofanyika jana kwenye viwanja vya chuo cha Ushrika Mjini Moshi.
Waziri wa habari, utamaduni, Sanaa na michezo Mhe. Nape mnauye   (katikati mwenye kofia) akisubiri kufungua mbio za Tigo Kili half Marathon 2016, mkoani Kilimanjaro, kulia kwake  Meneja masoko Olivier prentout  atika mashindano hayo yaliyofanyika jana kwenye viwanja vya chuo cha Ushrika Mjini Moshi .
Wanariadha wa Tigo Kili half Marathon wakisubiri kuanza mbio   katika mashindano ya Tigo Kili Half Marathon  katika mashindano hayo yaliyofanyika jana kwenye viwanja vya chuo cha Ushrika Mjini Moshi.  
Wafanyakazi wa kampuni ya Tigo wakikimbia mbio za Tigo half Marathon katika mashindano ya Tigo Kili Half Marathon  katika mashindano hayo yaliyofanyika jana kwenye viwanja vya chuo cha Ushrika Mjini Moshi.   
Meneja chapa Tigo, William Mpinga akimalizia mbio za kilometa 21      katika mashindano ya Tigo Kili Half Marathon  katika mashindano hayo yaliyofanyika jana kwenye viwanja vya chuo cha Ushrika Mjini Moshi.  
Wafanyakazi wa Tigo wakiwa kwenye water point kwa kutoa huduma kwa wakimbiaji   katika mashindano ya Tigo Kili Half Marathon  katika mashindano hayo yaliyofanyika jana kwenye viwanja vya chuo cha Ushrika Mjini Moshi.  
Mzee mwenye Umri wa miaka 70 akiungana na wanariadha wenzake  katika mashindano ya Tigo Kili Half Marathon  katika mashindano hayo yaliyofanyika jana kwenye viwanja vya chuo cha Ushrika Mjini Moshi.
Wanariadha mbalimbali wakikimbia katika  katika mashindano ya Tigo Kili Half Marathon  mashindano hayo yaliyofanyika jana kwenye viwanja vya chuo cha Ushrika Mjini Moshi.  
Mkurugenzi Mkuu wa Tigo, Diego Gutierrez nae akionyesha ushirikiano mzuri kabisa na wananchi kwa wa kuungana nao katika mashindano ya Tigo Kili Half Marathon  mashindano hayo yaliyofanyika jana kwenye viwanja vya chuo cha Ushrika Mjini Moshi.
Mkurugenzi Mkuu wa Tigo, Diego Gutierrez  akipata huduma ya kwanza wakati akikimbia   na kumalizia kilomita 42 za kili marathon katika mashindano yaliyofanyika katika viwanja vya Chuo cha ushirika Mjini Moshi jana 
Meneja mkuu wa Tigo Tanzania, Diego Gutierrez akimaliza mbio za kilomita 42 za kili marathon katika mashindano yaliyofanyika katika viwanja vya Chuo cha ushirika Mjini Moshi jana.
Meneja mkuu wa Tigo , Diego Gutierrez akipongezwa na mkiambiaji wenzie Mara baada ya kumaliza mbio za Kilimanjaro marathon za kilomita 42   katika mashindano yaliyofanyika katika viwanja vya Chuo cha ushirika Mjini Moshi jana.
Waziri wa habari, utamaduni, Sanaa na michezo Mhe. Nape mnauye  akimkabidhi akimkabidhi hundi ya sh Milion 2 Bernard Matheka (mkenya miaka 27) baada ya kuibuka mshindi kwa upande wa wanaume  katika mashindano ya Tigo Kili Half Marathon kwa kukimbia kilometa 21 na kutumia saa 1.14.55  katika mashindano hayo yaliyofanyika jana kwenye viwanja vya chuo cha Ushrika Mjini Moshi.

Baadhi ya washiriki waliopata bahati ya kuzawadiwa na Tigo kwenye mbio za Kili Marathon  katika mashindano hayo yaliyofanyika jana kwenye viwanja vya chuo cha Ushrika Mjini Moshi.

Shule 18 Dar kunufaika na elimu ya usalama Barabarani kutoka kwa CFAO Motors Group na Alliance Autos

IMG_4204
Meneja wa Volkswagen nchini, Bi. Tharaia Ahmed (kulia) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu mafunzo ya elimu ya usalama barabarani ambayo wanataraji kufanya katika shule 18 zilizo katika Manispaa ya Ilala.Mkurugenzi Mtendaji wa CFAO Motors Group, Eric Potin, (katikati) na Mwanzilishi wa mashindano ya mbio za magari ya Go4school, Henning Nathow.

Katika kusaidia kupambana na ajali za barabarani kwa watoto wa shule za msingi jijini Dar es Salaam, kampuni ya CFAO Motors Group kwa kushirikiana na Alliance Autos ambao ni wauzaji wa magari ya Volkswagen wametoa msaada wa elimu na vifaa vya usalama barabarani kwa shule 18 zilizo katika Manispaa ya Ilala, Dar es Salaam.

Akizungumzia msaada huo Meneja wa Volkswagen nchini, Tharaia Ahmed amesema kuwa lengo la kutoa elimu na vifaa hivyo ni kuwasaidia wanafunzi wa shule ambao wengi wao wamekuwa hawana uelewa mzuri kuhusu kuvuka barabara.

Alivitaja vifaa hivyo kuwa ni alama za barabarani ambazo zinaonyesha alama za kusimamisha magari ili wanafunzi wavuke, makoti yanayowatambulisha waongozaji, kofia za kuwazuia na jua na mipira ya michezo mashuleni na watatoa elimu katika shule hizo ili kuwasaidia watoto kujua sheria za barabarani.

“Tumeamua kutoa msaada huu kwa shule 18 na tutatoa elimu na tutakabidhi vifaa … tunaamini msaada huu utaweza kuwasaidia watoto hao na tunaamini itasaidia kupunguza ajali barabarani,” alisema Bi. Tharaia.

Akipokea vifaa hiyvo kwa niaba ya Afisa Elimu wa Ilala, Helen Peter alisema wanaishukuru CFAO Motors Group kwa kutambua umuhimu wa elimu na kutoa vifaa vitakavyoweza kusaidia kuongoza wanafunzi wavukapo barabara.

"Tunashukuru sana kwa msaada huu na mmeonyesha ni jinsi gani mnatambua umuhimu wa elimu na sisi tupo pamoja nanyi na tupo tayari kupokea elimu hiyo," alisema Bi. Helen.

Alizitaja baadhi ya shule ambazo zitapata vifaa hivyo kuwa ni Shule ya Msingi Msimbazi, Boma, Mnazi Mmoja, Uhuru Mchanganyiko, Tabata, Ilala, Lumumba, Muhimbili, Buguruni, Kasulu, Mkoani, Msimbazi Mseto, Hekima, Amana, Mtendeni, Buguruni Viziwi na Tabata Jeta na Mtandani.

Pamoja na hayo pia kunataraji kufanyika mashindano ya mbio za magari yaliyo na lengo la kuchangia elimu nchini Rwanda yanayoratibiwa na kampuni ya CFAO Motors Group yanayofanyika nchini na yanataraji kumalizikia nchini Rwanda.
Attu Mynah
Meneja Masoko wa CFAO Motors Group nchini, Bi. Attu Mynah (kulia) akionyesha baadhi vifaa hivyo vya usalama barabarani kwa waandishi wa habari (hawapo pichani).

Mbio hizo za kusaidia elimu nchini Rwanda zimepewa jina la The go4school Charity Rally ambazo zimeshirikisha magari 18 ambayo yameanzia jijini Dar es Salaam na yanataraji kufikia kilele chake Machi, 13 nchini Rwanda na yatapita katika nchi za Kenya na Uganda na kisha Rwanda.

Akizungumzia mashindano hayo Mkurugenzi Mtendaji wa CFAO Motors Group, Eric Potin alisema mbio hizo za magari zimeanzishwa na taasisi ya Volkswagen kwa kushirikiana na taasisi ya Opportunity International Germany kwa kutambua kwao umuhimu wa elimu na usalama wa watoto wawapo barabarani.

Alisema kuwa wamekuwa wakisaidia zaidi katika sekta ya elimu na sio mara ya kwanza kufanya mbio hizo za magari kwani mwaka 2013 walifanya mbio kama hizo kutokea Senegal hadi Ghana na mwaka 2015 walifanya kutokea Namibia hadi Malawi na mara zote kampuni ya CFAO Motors Group imekuwa ikihusika kufanikisha mbio hizo.
Henning Nathow
Mwanzilishi wa mashindano ya mbio za magari ya go4school, Henning Nathow (wa pili kushoto) akielezea dhumuni lengo lao la kusaidia upatikanaji wa elimu bora kupitia mradi wa go4school.

“Mbio hizi zimeanzishwa na Wajerumani ili kusaidia elimu ya Rwanda na hii sio mara ya kwanza tayari yamefanyika mara mbili barani Afrika na sisi kama CFAO tumekubali kuungana na taasisi ya Opportunity International Germany ili kusaidia upatikanaji wa elimu,” alisema Potin.

Nae Henning Nathow ambaye ndiyo mwanzilishi wa mradi wa go4school ulio na lengo la kusaidia upatikanaji wa elimu bora alisema wanafurahi kufanya mbiao hizo ambazo zina lengo la kusaidia elimu nchini Rwanda wa wanaamini elimu ndiyo njia pekee inayoweza kusaidia kupambana na umasikini.

Alisema wanataraji kufanya mbio hizo na baada ya kufika Rwanda watayakabidhi magari yanayotumika kwa ofisi za CFAO za Rwanda na baada ya hapo watayauza na mapato yatakayopatikana watayakabidhi kwa serikali ya Rwanda ili kusaidia sekta ya elimu.

“Elimu ni njia ambayo inaweza kusaidia kumaliza janga la umasikini na sisi tuna furaha kufanya mbio hizo kuelekea Rwanda ili kusaidia kupatikana kwa elimu bora Rwanda,” alisema Nathow.
Helen Peter
Afisa Elimu wa Ilala, Helen Peter akitoa neno la shukrani kwa kampuni ya CFAO Motors Group kwa msaada huo wa vifaa vya usalama barabarani kwa shule 18 zilipo ndani ya Manispaa ya Ilala.
Eric Potin
Mkurugenzi Mtendaji wa CFAO Motors Group, Eric Potin (wa pili kushoto) akimkabidhi Afisa Elimu ya Ufundi wa Manispaa ya Ilala, Bi. Helen Peter (wa kwanza kushoto) msaada wa vifaa vya usalama barabarani kusaidia wanafunzi wavukapo barabarani pamoja na vifaa vya michezo, Wanaoshuhudia tukio hilo ni Meneja wa Volkswagen nchini, Bi. Tharaia Ahmed na (kulia) na Meneja Masoko wa CFAO Motors Group nchini, Bi. Attu Mynah.
Eric Potin
Attu Mynah
Meneja Masoko wa CFAO Motors Group nchini, Bi. Attu Mynah akifafanua jambo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani).
Volkswagen Tanzania
Pichani juu na chini ni kati ya magari 18 yaliyoondoka nchini jana kuelekea Rwanda kwa ajili ya kushiriki mashindano ya mbio za magari yaliyo na lengo la kuchangia elimu nchini Rwanda yanayoratibiwa na kampuni ya CFAO Motors Group.
Volkswagen, Tanzania
IMG_4332
Msafara wa magari aina ya Volkswagen yanayoelekea nchini Rwanda yakitoka kwenye 'showroom' ya Volkswagen iliyopo kampuni ya CFAO Motors Group, barabara ya Pugu jijini Dar.
Volkswagen Tanzania