Mashabiki wa Simba wakifuatilia mchezo kati ya timu yao hiyo dhidi ya African Sports, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam leo. Simba imeshinda mabao 4-0. (Picha zote na Kassim Mbarouk-www.bayana.blogspot.com)
Ubao wa matokeo ukionesha Simba bao 1 na African Sports 0. Bao lililofungwa na Hamis Kiiza.
Ibrahim Ajib wa Simba akimiliki mpira huku akifuatwa na Juma Shemvun wa African Sports.
Juma Shemvun wa African Sports, akipiga tik tak mbele ya Ibrahim Ajib wa Simba.
Hassan Kessy wa Simba akipiga shuti huku akizuiwa na Juma Shemvun wa African Sports.
Wachezaji wa Simba wakimpongeza Hassan Kessy baada ya kuifungia timu yake bao la 2.
Wachezaji wa Simba wakimpongeza Hassan Kessy baada ya kuifungia timu yake bao la 2.
Hamis Kiiza (kulia), akimpongeza Hassan Kessy.
Hassan Kessy akishangilia bao lake hilo, huku akipongezwa na Ibrahim Ajib.
Halfan Twenye wa African Sports akiruka juu kuupiga mpira kichwa huku akifuatwa na Hassan Kessy wa Simba.
Ubao wa matokeo ukionesha Simba mabao 2 na African Sports 0.
Hamis Kiiza akichezewa rafu na beki wa African Sports.
Wachezaji Ibrahim Ajib (kushoto) na Haji Ugando (kulia), wote wa Simba, wakimpongeza mwenzao Hamis Kiiza baada ya kuifungia bao la tatu timu yake hiyo, iliyoshinda mabao 4-0 dhidi ya African Sports katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam leo. Kiiza aliifungia Simba mabao 2 katika mchezo huo.

Ubao wa matokeo ukionesha Simba mabao 3 African Sports 0.
Mashabiki wa Simba wakiwapongeza wachezaji wao wakati wakipita kuingia kwenye vyumba vya mapumziko.

No comments:
Post a Comment