Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe.
Nape Moses Nnauye (kushoto) akizungumza na wajumbe wa Kamati ya
wasanii wa Muziki inayofuatilia suala la malipo ya mrabaha kutokana na kazi zao
Jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwezeshaji Mhe.
Charles Mwijage akizungumza na wajumbe wa Kamati ya wasanii wa Muziki
inayofuatilia suala la malipo ya mrabaha kutoka kwa vyombo vya habari na miito
ya simu. Kushoto ni Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape
Moses Nnauye na kulia ni Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA)
Bw. Godfrey Mungereza leo jijini Dar es Salaam.
Msanii wa Muziki wa Kizazi kipya ambaye pia ni
Kiongozi wa Kamati ya wasanii wa muziki, Nickson Simon kwa jina la kisanii
Nikki wa Pili akiwasilisha hoja za kwa niaba ya wasanii wenzake wakati wa kikao
baina yao na waheshimiwa Mawaziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo pamoja
Mhe. Nape Moses Nnauye na Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwezeshaji Mhe. Charles
Mwijage leo jijini Dar es Salaam.Kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Sana
Bibi. Leah Kihimbi na kushoto ni msaanii Ditto.
Msanii wa Muziki wa Kizazi kipya ambaye pia mjumbe
wa Kamati ya wasanii wa muziki akichangia mada wakati wa kikao baina yao na
waheshimiwa Mawaziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo pamoja Mhe. Nape
Moses Nnauye na Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwezeshaji Mhe. Charles Mwijage
leo jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo
Mhe. Nape Moses Nnauye akizungumza na msanii mkongwe wa muziki wa injili Bw.
Cosmas Kidumule mara baada ya kumaliza kikao na Kamati ya wasanii leo jijini
Dar es Salaam.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo
Mhe. Nape Moses Nnauye (aliyevaa batiki) na Waziri wa Viwanda, Biashara na
Uwezeshaji Mhe. Charles Mwijage wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya
wasanii mara baada ya kumaliza kikao na Kamati ya wasanii leo jijini Dar es
Salaam. (Picha zote na Frank Shija-WHUSM)







No comments:
Post a Comment