TANGAZO


Thursday, January 7, 2016

Rais Dk. Shein afungua Skuli ya Mnarani Wilaya ya Micheweni Kisiwani Pemba

*Awataka wazazi kufuatilia maendeleo
ya watoto wao maskulini 
Rais wa Zanzbar na Menyekiti wa Baraza la Mapiduzi Dk. Ali Mohamed Shein akisalimiana na Katibu Mkuu Wizra ya Elimu na Mafunzo ya Amali, Bi. Khadija Bakari wakati alipowasili viwanja vya Skuli ya Msingi Mnarani Wilaya ya Micheweni kuifungua Skuli hiyo iliyojengwa kwa Nguvu za wananchi na Ufadhili ya Shirika la Milele Foundation la Zanzibar leo ikiwa katika shamra shamra za kusherehekea miaka 52 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar. ([Picha zote na Ikulu) 
Rais wa Zanzbar na Menyekiti wa Baraza la Mapiduzi Dk.Ali Mohamed Shein akifungua pazia kuashiria uzinduzi wa Skuli ya Msingi Mnarani leo Wilaya ya Micheweni Mkoa wa Kaskazini Pemba iliyojengwa kwa nguvu za wananchi na Ufadhili ya Shirika la Milele Foundation la Zanzibar. Ufunguzi huo ikiwa katika shamra shamra za kusherehekea miaka 52 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar. Kulia ni Katibu Mkuu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali, Bi. Khadija Bakari na kushoto ni Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Ali Juma Shamuhuna.
Rais wa Zanzbar na Menyekiti wa Baraza la Mapiduzi Dk. Ali Mohamed Shein akikata utepe kuashiria ufunguzi wa Skuli ya Msingi Mnarani leo Wilaya ya Micheweni Mkoa wa Kaskazini Pemba iliyojengwa  kwa  Nguvu za wananchi na Ufadhili ya Shirika la Milele Foundation la Zanzibar,ufunguzi huo ikiwa katika shamra shamra za kusherehekea miaka 52 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.
Rais wa Zanzbar na Menyekiti wa Baraza la Mapiduzi Dk. Ali Mohamed Shein akiuliza jambo kwa Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Ali Juma Shamuhuna (wa pili kushoto) baada ya kuifungua   Skuli ya Msingi Mnarani   Wilaya ya Micheweni Mkoa wa Kaskazini Pemba leo,iliyojengwa  kwa  Nguvu za wananchi na Ufadhili ya Shirika la Milele Foundation la Zanzibar, ikiwa katika shamra shamra za kusherehekea miaka 52 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.
Rais wa Zanzbar na Menyekiti wa Baraza la Mapiduzi Dk. Ali Mohamed Shein akiwapungia mkono wanafunzi  mara baada ya kuifungua na kuitembelea  Skuli ya Msingi Mnarani   Wilaya ya Micheweni Mkoa wa Kaskazini Pemba leo, iliyojengwa  kwa  Nguvu za wananchi na Ufadhili ya Shirika la Milele Foundation la Zanzibar,  ikiwa katika shamra shamra za kusherehekea miaka 52 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.
Wanafunzi wa Skuli ya Msingi Mnarani   Wilaya ya Micheweni Mkoa wa Kaskazini Pemba wakimsikiliza Rais wa Zanzbar na Menyekiti wa Baraza la Mapiduzi Dk. Ali Mohamed Shein wakati alipokuwa akizungumza nao baada ya kuifungua rasmi leo ikiwa ni katika sherehe za maadhimisho ya miaka 52 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.  
Baadhi ya Wazee, Walimu na Wanafunzi wa Mnarani Wilaya ya Micheweni Mkoa wa Kaskazini Pemba wakimsikiliza Rais wa Zanzbar na Menyekiti wa Baraza la Mapiduzi Dk.Ali Mohamed Shein wakati alipokuwa akizungumza nao baada ya kuifungua rasmi Skuli ya Msingi Mnarani leo ikiwa ni  katika sherehe za maadhimisho ya miaka 52 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.
Wananchi na Wanachama w Chama cha Mapinduzi CCM waliohudhuria sherehe za ufunguzi wa Skuli ya Msingi Mnarani wakimsikiliza Rais wa Zanzbar na Menyekiti wa Baraza la Mapiduzi Dk. Ali Mohamed Shein wakati alipokuwa akizungumza nao baada ya kuifungua rasmi Skuli ya Msingi Mnarani leo ikiwa ni  katika sherehe za maadhimisho ya miaka 52 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.    
Baadhi ya Wanafunzi wa Skuli ya Msingi Mnarani, Wilaya ya Micheweni Mkoa wa Kaskazini Pemba wakimsikiliza Rais wa Zanzbar na Menyekiti wa Baraza la Mapiduzi Dk. Ali Mohamed Shein wakati alipokuwa akizungumza nao baada ya kuifungua rasmi leo ikiwa ni katika sherehe za maadhimisho ya miaka 52 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.
Rais wa Zanzbar na Menyekiti wa Baraza la Mapiduzi Dk.Ali Mohamed Shein  akisalimiana na wasoma utenzi Salama Nassor Shehe na Sharifa Juma Hamadi katika hafla ya ufunguzi wa Skuli ya Msingi Mnarani  Wilaya ya Micheweni Mkoa wa Kaskazini Pemba iliyojengwa  kwa ushirikiano wa Serikali, nguvu za wananchi na Shirika la Milele Zanzibar Foundation  leo ikiwa ni katika sherehe za maadhimisho ya miaka 52 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar. 
Rais wa Zanzbar na Menyekiti wa Baraza la Mapiduzi Dk. Ali Mohamed Shein  akipokea Risala kutoka kwa Mossi Hamadi Khamis katika sherehe ya ufunguzi wa Skuli ya Msingi Mnarani  Wilaya ya Micheweni Mkoa wa Kaskazini Pemba iliyojengwa  kwa ushirikiano wa Serikali,Nguvu za Wananchi na Shirika la Milele Zanzibar Foundation  leo ikiwa ni katika sherehe za maadhimisho ya miaka 52 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.
Rais wa Zanzbar na Menyekiti wa Baraza la Mapiduzi Dk.Ali Mohamed Shein  akisalimiana na Mkurugenzzi Mkuu wa Shirika la Milele Zanzibar Foundaation Yousuf Caires wakati wa sherehe ya  ufunguzi wa Skuli ya Msingi Mnarani  Wilaya ya Micheweni Mkoa wa Kaskazini Pemba iliyojengwa  kwa ushirikiano wa Serikali,Nguvu za Wananchi na Shirika la Milele Zanzibar Foundation  leo ikiwa ni katika sherehe za maadhimisho ya miaka 52 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.
Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Pemba Omar Khamis Othman alipokuwa akitoa salamu za Mkoa kwa Rais wa Zanzbar na Menyekiti wa Baraza la Mapiduzi Dk. Ali Mohamed Shein kabla ya kuzungumza na Wananchi, Walimu na Wanafunzi pamoja na viongozi mbali mbali waliohudhuria katika ufunguzi wa Skuli ya Msingi Mnarani  Wilaya ya Micheweni Mkoa wa Kaskazini Pemba iliyojengwa  kwa ushirikiano wa Serikali,Nguvu za Wananchi na Shirika la Milele Zanzibar Foundation  leo ikiwa ni katika sherehe za maadhimisho ya miaka 52 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.
Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali   Ali Juma Shamuhuna akimakaribisha Rais wa Zanzbar na Menyekiti wa Baraza la Mapiduzi Dk.Ali Mohamed Shein kuzungumza na Wananchi, pamoja na viongozi mbali mbali waliohudhuria katika ufunguzi wa Skuli ya Msingi Mnarani Wilaya ya Micheweni Mkoa wa Kaskazini Pemba leo iliyojengwa  kwa ushirikiano wa Serikali,Nguvu za Wananchi na Shirika la Milele Zanzibar Foundation   ikiwa ni katika sherehe za maadhimisho ya miaka 52 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar. 
Rais wa Zanzbar na Menyekiti wa Baraza la Mapiduzi Dk.Ali Mohamed Shein akizungumza na Wananchi, pamoja na viongozi mbali mbali waliohudhuria katika ufunguzi wa Skuli ya Msingi Mnarani  Wilaya ya Micheweni Mkoa wa Kaskazini Pemba leo iliyojengwa  kwa ushirikiano wa Serikali,Nguvu za Wananchi na Shirika la Milele Zanzibar Foundation   ikiwa ni katika sherehe za maadhimisho ya miaka 52 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar

Na Said Ameir, Pemba
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein amesisitiza umuhimu wa wazazi kufuatilia maendeleo ya elimu ya watoto wao maskulini ili hatua mbalimbali zinazochukuliwa na serikali kuimarisha elimu ziweze kufikia malengo yaliyowekwa.
Amefafanua kuwa mabadiliko ya sera ya elimu yaliyofanywa na serikali ambayo pamoja na mambo mengine yatawawezesha vijana wa Zanzibar kumaliza elimu wakiwa na umri wa wastani kama nchi nyingine yanahitaji ushirikiano wa karibu kati ya serikali na wazazi ili yaweze kutekelezeka.
Dk. Shein alibainisha kuwa kwa utaratibu wa sasa wa watoto kumaliza elimu ya msingi baada ya miaka sita badala ya saba yatawafanya watoto kuingia sekondari wakiwa na umri mdogo hivyo wazazi wanapaswa kufuatilia kwa karibu na kwa umakini zaidi maendeleo ya watoto wao kwa kushirikiana na walimu.
Akizungumza na wananchi kwenye hafla ya uzinduzi wa Skuli ya Msingi ya Mnarani ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 52 ya Mapinduzi huko wilaya Micheweni leo, Dk. Shein aliwahakikishia wananchi kuwa serikali itaendelea kuimarisha sekta ya elimu ili kutimiza malengo ya Mapinduzi ya mwaka 1964 ya kuwapatia elimu wananchi wote.
“Tulilazimika kufanya Mapinduzi kukomesha kila aina ya dhulma dhidi ya wananchi wanyonge wa Zanzibar na kazi yetu sasa ni kuhakikisha malengo ya Mapinduzi yanatekelezwa na kila mwananchi anafaidika kwa kuchukua hatua madhubuti za kuwapatia huduma kama hizi” Dk. Shein aliwaeleza wananchi hao.
Katika kuimarisha elimu, Dk. Shein alisema serikali imeangalia upya ramani za maskuli nchini ambapo kutokana na ukosefu wa ardhi skuli sasa zitajengwa za ghorofa kwa kadri hali itakavyoruhusu.
“Hivi sasa serikali ina mpango wa kujenga skuli nyingine kumi na moja, 9 zitakuwa za ghorofa ambapo 5 zitajengwa Unguja na 4 Pemba” Dk. Shein alisema na kubainisha kuwa fedha za ujenzi wa skuli hizo zitatolewa na Shirika la Nchi Zinazosafirisha Mafuta kwa Wingi Duniani (OPEC).
Alifafanua kuwa ujenzi wa skuli za aina hiyo ulianza katika awamu iliyopita ambapo jumla ya skuli 19 zilijengwa Unguja na Pemba miongoni mwao zikiwa za ghorofa.
Hata hivyo, Mheshimiwa Rais alieleza kutofurahishwa kwake na taarifa ya uandikishaji watoto katika Wilaya ya Micheweni ambapo kwa upande wa elimu ya maandalizi kiwango cha uandikishaji ni asilimia 35.6 tu wakati sekondari ni asilimia 40.3 tu.
Kwa hivyo aliwataka wazazi na walezi katika wilaya hiyo kuhakikisha kuwa watoto wote waliotimiza umri wa kwenda skuli wanaandikishwa na wanahudhuria masomo.
Hata hivyo aliwapongeza wananchi wa Mnarani katika wilaya hiyo ambapo kiwango cha uandikishaji watoto wenye umri wa kwenda skuli ni zaidi ya asilimia 100.
Katika hotuba yake hiyo Dk. Shein aliishukuru Taasisi ya Milele Zanzibar Foundation kwa kuchangia kwa kiwango kikubwa ujenzi wa skuli hiyo ambayo ujenzi wake wote uligharimu shilingi milioni 359.377.
Dk. Shein aliahidi kuipatia skuli hiyo kompyuta moja iliyokamilika pamoja na mashine ya kurudufia(Photopy machine) baada ya skuli hiyo kukamilisha kazi ya kuweka umeme.
Awali akitoa maelezo kuhusu ujenzi wa skuli hiyo Katibu Mkuu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Bibi Khadija Bakari alisema kukamilika kwa skuli hiyo kumeleta faraja kwa wananchi wa Mnarani na vijiji jirani ambapo mwaka huu wameweza kuandikisha watoto zaidi 240.
Alifafanua kuwa kati ya watoto hao wengine wana umri unaofikia miaka 11 ambao walishindwa kuandikishwa skuli kutokana na huko nyuma skuli kuwa mbali hivyo kuwafanya wazazi kutopeleka watoto skuli.
Katika risala yao kwa Mgeni Rasmi iliyosomwa na mwalimu Mosi Hamad Khamis wananchi walieleza kuwa uzinduzi wa skuli hiyo ni mwanzo ya safari ndefu ya wananchi wa kijiji hicho na jirani kutafuta elimu bra kwa watoto wao.
Risala hiyo ilieleza kuwa skuli hiyo ambayo ina uwezo wa kuchukua watoto 310 ambapo tayari ina watoto 477 imejengwa kwa ushirikiano kati ya wananchi, Serikali na Taasisi ya Milele Zanzibar Foundation.
Ikitoa ufafanuzi wa gharama, risala ilieleza kuwa Halmashauri ilitoa shilingi milioni 7.3, nguvu za wananchi ilikuwa shilingi milioni 3.3 , Mbunge milioni 3, Mwakilishi milioni 2, Kamati ya uvuvi laki 9 na hoteli ya Aiyana shilingi 350,000.
Kwa upande wa Taasisi ya Milele, risala ilieleza kuwa taasisi hiyo imejenga jengo jipya lenye vyumba 8 vya madarasa, Ofisi ya Mwalimu Mkuu, Ofisi ya walimu, vyoo viwili vyenye matundu 10, na nyumba moja ya walimu kwa familia mbili.
Dk. Shein anatarajiwa kumaliza ziara yake ya siku tatu kisiwani Pemba baadae jioni kwa kufungua mradi wa Taa za Kuongoza Ndege katika Uwanja wa Ndege wa Pemba uliopo Chake Chake.

No comments:

Post a Comment