TANGAZO


Saturday, January 30, 2016

Marais sasa kujadili mgogoro wa Burundi

Image copyrightReuters
Image captionViongoz wa AU wanakutana kujadiliana kuhusu
Kamati ya Amani na Usalama ilioyofanya kikao chake kirefu hapo jana usiku ilishindwa kuafikia maamuzi kuhusu mgogoro wa Burundi na hivyo kuamua kulipeka swala hilo katika ngazi ya viongozi wakuu wa nchi.
Hata hivyo Waziri wa Mambo ya Nje wa Tanzania Balozi Augustine Mahiga aliiambia BBC kwamba hoja ya kupeleka vikosi vya kulinda amani nchi Burundi tayari ilikuwa imeondolewa mezani na kwamba kilichokuwa kinatarajiwa kujadiliwa ni namna gani ya kuendeleza mazungumzo ya kisiasa ambayo yamekuwa yakisuasua.
Wakuu wa nchini wanakutana juamosi.
Mkutano huo wa wakuu wa nchi unatarajiwa kubariki maamuzi ambayo yamefikiwa na Kamati ya Amani na Usalama ambayo ilikaa jana usiku.
Hata hivyo kushindwa kufikiwa kwa maamuzi ya kamati hiyo, kuna maanisha wakuu hao wa nchi wana kibarua kikubwa kuliko kupitisha maamuzi
Kama jinsi ambavyo mkutano mzima ulitawaliwa na swala la Burundi, bado hali ya udadisi inaendelea kutaka kujua mkutano huu unapofungwa ni hatua gani ambayo Umoja huu wa Afrika utakuwa umeifikia
Mgogoro wa Sudani ya Kusini nao bado unaendelea kufuatiliwa kwa karibu. Wakati hakuna kilicho wazi juu ya nini kamati ya amani na usalam iliafikia juu ya mgogoro huu, Rais wa nchi hiyo Salva Kiir amesusia mkutano huo wakati ambapo alitarajiwa kwamba angekutana na mpinzani wake Riech Machar.
Hii si mara ya kwanza kwa rais huyu kususia mkutano unaojadili nchi yake moja kwa moja.
Mwaka jana mwezi 9, rais Kiir alikwepa mkutano wa viongozi wa juu wa dunia ambao ulikuwa ukijadili swala la Amani
Bila shaka maamuzi ya mkutano huo wa wakuu wa nchi utajulikana baadaye jioni.

No comments:

Post a Comment