TANGAZO


Friday, January 29, 2016

Kikao cha Bungeni leo Mjini Dodoma

Baadhi ya wabunge wakiwasili katika ukumbi wa Bunge kuhudhuria kikao cha Bunge la 11 linaloendelea Mjini Dodoma.
Naibu Spika Mhe Dkt Tulia Ackson akiongoza kikao cha Bunge la 11 linaloendelea Mjini Dodoma.   
Mwenyekiti wa Bunge Mhe. Adrew Chenge akiwakiwasilia tayari kuongoza kikao cha Bunge katika Bunge la 11 linaloendelea mjini Dodoma.
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe Dkt Philip Mpango akiwasilisha hoja ya Serikali ili Bunge lijadili na kuidhinisha Mpango wa pili wa Maendeleo ya Taifa kwa kipindi cha miaka mitano.  
Naibu Waziri  wa Nchi Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora Mhe. Suleiman Jafo akitoa ufafnuzi juu ya maswali yaliyoulizwa na wabunge kuhusu wizara hiyo katika kikao cha cha Bunge la 11 linaloendelea Mjini Dodoma. 
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) Mhe.George Simbachawene akitoa ufafnuzi juu ya maswali yaliyoulizwa na wabunge kuhusu wizara hiyo katika kikao cha cha Bunge la 11 linaloendelea Mjini Dodoma. 
Waziri wa Elimu, Sayansi na Mafunzo ya ufundi Mhe. Prof. Joyce Ndalichako akitoa ufafanuzi kuhusu maswali yaliyoulizwa na wabunge kuhusu wizara hiyo katika kikao cha cha Bunge la 11 linaloendelea Mjini Dodoma.
Waziri wa Habari,utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye akimsikiliza Naibu wake Mhe. Anastazia Wambura walipokuwa katika kikao cha Bunge la 11 linaloendelea Mjini Dodoma.  
Waziri wa Katiba na Sheria Mhe Dkt. Harrison Mwakyembe akimsikiliza Mbunge wa Kigoma  Mjini (ACT) Mhe. Zitto Kabwe  walipokuwa katika kikao cha Bunge la 11 linaloendelea Mjini Dodoma.
Baadhi ya wabunge wakifatilia kikao cha Bunge la 11 linaloendelea Mjini Dodoma.
Waziri wa Elimu, Sayansi na Mafunzo ya ufundi Mhe.Prof Joyce Ndalichako akiwa katika picha ya pamoja na walimu na wanafunzi wa Shule ya Sekondari Sangu iliyoko Jijini Mbeya.   
Waziri wa Sayansi,Teknolojia na Mafunzo ya ufundi Mhe.Prof Joyce Ndalichako akiwa katika picha ya pamoja na walimu na wanafunzi wa shule ya Sekondariya Mtakatifu Monica iliyoko Jijini Arusha. (Picha zote na Raymond Mushumbusi, Maelezo)

No comments:

Post a Comment