Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora Mhe. Angella Kairuki akiwa katika kikao na Wajumbe wa Sekretarieti ya Ajira pamoja na Watumishi wa Sekretarieti hiyo.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora Mhe. Angella Kairuki akipata Maelezo ya juu wa upokeaji wa maombi ya kazi kwa njia ya Mtandao kutoka kwa Naibu Katibu wa Kitengo cha TEHAMA Mhandisi Samweli Tanguye.
Na
Kassim Nyaki, Sekretarieti ya Ajira
WATUMISHI wa Sekretarieti ya Ajira wameaswa kuzingatia Sheria, Kanuni na Taratibu za
Utumishi wa Umma katika kutekeleza majukumu yao, kwa kuwa kazi wanayoifanya ni
nyeti na inagusa maisha ya watu ambayo itahitaji watu waadilifu, wapenda haki
na mfano mwema kwa jamii.
Waziri
wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Angella
Kairuki amesema hayo leo wakati alipotembelea ofisi hiyo na kuzungumza na
Wajumbe wa Sekretarieti ya Ajira pamoja na Watumishi.
''Nataka
mzingatie uadilifu katika utendaji kazi wenu wa kila siku, maana nitawafatilia
kila hatua kwani ninataka Watumishi wa Umma waadilifu ili mwisho wa siku tuwe
na Utumishi wa Umma uliotukuka'' alisisitiza Kairuki.
Aliongeza
kuwa Watanzania wako wengi wenye sifa za kuajiriwa, ambao wanahitaji kupata
huduma bora na inayostahili kwa kuwa kila Mtumishi aliyeko katika Sekretarieti
ya Ajira aliajiriwa akijua Utumishi wa Umma una taratibu zake za kiutendaji, kwa
mujibu wa Sheria, Kanuni na miongozo mbalimbali na si vinginevyo.
Aidha,
aliwataka Watumishi hao kutumia hazina kubwa ya Wajumbe wa Sekretarieti ya
Ajira waliopo kwa kuwa anawafahamu, anajua uwezo wao katika kazi, kwakuwa
walikuwa Watumishi waadilifu wa Umma na
wa muda mrefu. Hivyo ushauri wao na maelekezo wanayotoa yakitumika vizuri
yataisaidia sana Sekretarieti ya Ajira katika kutimiza malengo yake na kuwa
chombo cha mfano wa kuigwa kiutendaji.
Wakati
huohuo, Mwenyekiti wa Wajumbe wa Sekretarieti ya Ajira Bw. Bakari Mahiza alimpongeza
Waziri huyo kwa kuchaguliwa kusimamia Wizara hii nyeti inayosimamia
rasimaliwatu ambayo ni rasilimali muhimu sana katika taifa lolote na anaamini ujio
wake utaongeza chachu katika utendaji wa Taasisi hiyo.
Kwa
upande wake Katibu wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma Bw. Exavier
Daudi mbali na kueleza jinsi Mchakato wa Ajira unavyoendeshwa, mafanikio,
changamoto na matarajio ya chombo hiko alimshukuru Waziri huyo kwa kuwatembelea
na kumwahidi kufanyia kazi maelekezo na ushauri alioutoa.

No comments:
Post a Comment