TANGAZO


Friday, December 11, 2015

Washiriki 15 wachaguliwa katika shindano la Tigo Digital Change Makers’ la 2015

Baadhi ya washindi wa shindano la Tigo Changemakers katika miaka ya hivi karibuni wakipokea hundi zao dola 20,000 kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa Tigo Bw. Diego Gutierrez.

Dar es Salaam, Desemba 11, 2015: 
KAMPUNI ya Tigo Tanzania kwa kushirikiana na Reach for Change (R4C) wametangaza  washiriki 15 wenye vipaji vya ujasiriamali wa kijamii wamechaguliwa katika shindano la  “Tigo Digital Change Makers’ ambapo washindi wawili watatangazwa wiki ijayo.

Shindano hili lilioanza Septemba, limepokea mamia ya maombi kutoka kwa washiriki wenye ubunifu wa kiteknologia katika sekta mbalimbali zikiwemo elimu, ukulima na afya kwa mujibu wa Afisa wa Huduma kwa Jamii wa Tigo, May Thomas.

Katika taarifa iliyotumwa kwa vyombo vya habari jijini Dar es Salam leo, May amesema, wajasiriamali wa kidijitali 15  waliochaguliwa kila mmoja wao alileta suluhisho la kidijitali lenye ubunifu lilokusudia kuboresha maisha ya watoto nchini Tanzania, na ndio kigezo kilicho wafanya wafuzu kushiriki katika shindano hilo.

May alisema: wengi katika hawa waombaji fikra zao bunifu zimeenda sambamba na mkakati wetu wa kuleta mabadiliko ya kidijitali maishani. Hali imesababisha changamoto kubwa katika zoezi la kuchagua washindani,” alisema, huku akiongeza kuwa washindi hao wawili watapokea dola za kimarekani 20,000 kila mmoja kwa ajili ya kutekeleza miradi yao.

Tigo na Reach for Change wameendesha shindano hili la Digital Change-Makers nchini Tanzania kwa kipindi cha miaka mitatu sasa, ambapo wajasiriamali wa kijamii  saba wameshinda fedha kwa ajili ya kutekeleza miradi yao. Kwa mujibu wa May, miradi ya wajasiriamali wa kijamii hao saba kwa pamoja imesaidia zaidi ya watoto 10,000 nchini katika kipindi hicho.

Shindano la Tigo Digital –Makers lina malengo ya kuwaendeleza na kuwatia moyo wajasiriamali wa kijamii kutumia teknolojia za kidijitali kusuluhisha baadhi ya matatizo sugu nchini Tanzania.

No comments:

Post a Comment