TANGAZO


Saturday, December 12, 2015

Wajumbe ‘waafikiana’ mkutano wa Paris

Joto


Image copyrightGetty
Image captionMataifa yanahimizwa kupunguza utoaji wa gesi zinazochangia ongezeko la joto duniani

Waandalizi wa mkutano kuhusu mabadiliko ya tabia nchi mjini Paris wanasema mswada wa mkataba mpya umeafikiwa baada ya karibu wiki mbili za mazungumzo.
Afisa katika afisi ya waziri wa mashauri ya kigeni wa Ufaransa Laurent Fabius ameambia AFP kwamba mswada huo utawasilishwa kwa mawaziri saa 10:30 GMT (saba unusu saa za Afrika Mashariki).
Hakuna maelezo yaliyotolewa kuhusu mswada huo kufikia sasa.
Mafanikio hayo yalipatikana saa 16 baada ya wakati uliotarajiwa.
"Tuna mswada wa kuwasilisha,” afisa huyo alisema, akiongeza kuwa mswada huo sasa utatafsiriwa kwa lugha sita rasmi za UN.
Wadadisi wa mambo wanasema bado huo hauwezi kuchukuliwa kama mkataba kamili.

Image copyrightEPA
Image captionBw Fabius alikuwa ameeleza matumaini mkataba utapatikana

Mswada huo utaidhinishwa iwapo hakutakuwa na pingamizi kwenye mkutano wa mawaziri kutoka nchi mbalimbali, ambao unatarajiwa kufanyika baadaye mjini Paris.
Bw Fabius, aliyeongoza mazungumzo hayo, alikuwa awali amesema kwamba “hali ni nzuri zaidi” ya kupatikana kwa mkataba thabiti na wa kufana.

No comments:

Post a Comment