Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri ya Wizara ya Fedha na Mipango Prof. Isaya Jairo akimkaribisha Mgeni Rasmi ambaye pia ni Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Dkt. Hamisi Mwinyimvua kutoa hotuba wakati mahafali ya 13 ya Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA) kwa Kampasi ya Dar es Salaam na Mtwara mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam.
Ofisa Mtendaji Mkuu ya Taasisi ya Uhasibu Tanzania Dkt. Joseph Kihanda akitoa taarifa fupi ya taasisi hiyo inayojumuisha pia idadi ya wahitimu 3,169 ambao kati yao wanawake ni 1,562 sawa na asilimia 49.3 na wanaume ni 1,607 sawa na asilimia 50.7 wakati mahafali ya 13 ya Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA) kwa Kampasi ya Dar es Salaam na Mtwara mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam.
Mgeni Rasmi ambaye pia ni Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Dkt. Hamisi Mwinyimvua akiwasili viwanja vya mahafali ya 13 ya Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA) kwa Kampasi ya Dar es Salaam na Mtwara mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Dkt. Hamisi Mwinyimvua akimkbidhi Mwanafunzi Cosmas Ephraim zawadi ya kufanya vizuri katika masomo yake ya shahada ya Uhasibu wakati mahafali ya 13 ya Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA) kwa Kampasi ya Dar es Salaam na Mtwara mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wahitimu wakifuatilia hotuba ya Mgeni Rasmi ambaye pia ni Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Dkt. Hamisi Mwinyimvua wakati wa mahafali ya 13 ya Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA) kwa Kampasi ya Dar es Salaam na Mtwara mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wahitimu wakifuatilia hotuba ya Mgeni Rasmi ambaye pia ni Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Dkt. Hamisi Mwinyimvua wakati wa mahafali ya 13 ya Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA) kwa Kampasi ya Dar es Salaam na Mtwara mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam.Baadhi ya wahitimu wakisiliza Mgeni Rasmi ambaye pia ni Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Dkt. Hamisi Mwinyimvua akisoma tamko la kuwatunuku vyeti wahitimu hao wakati wa mahafali ya 13 ya Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA) kwa Kampasi ya Dar es Salaam na Mtwara mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wahitimu wakisiliza Mgeni Rasmi ambaye pia ni Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Dkt. Hamisi Mwinyimvua akisoma tamko la kuwatunuku vyeti wahitimu hao wakati wa mahafali ya 13 ya Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA) kwa Kampasi ya Dar es Salaam na Mtwara mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wahitimu washangilia kwa furaha baada ya kutunukiwa vyeti na Mgeni Rasmi ambaye pia ni Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Dkt. Hamisi Mwinyimvua wakati wa mahafali ya 13 ya Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA) kwa Kampasi ya Dar es Salaam na Mtwara mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wahitimu washangilia kwa furaha baada ya kutunukiwa vyeti na Mgeni Rasmi ambaye pia ni Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Dkt. Hamisi Mwinyimvua wakati wa mahafali ya 13 ya Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA) kwa Kampasi ya Dar es Salaam na Mtwara mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam.
Mgeni Rasmi ambaye pia ni Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Dkt. Hamisi Mwinyimvua (katikati) pamoja na Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri ya Wizara ya Fedha na Mipango Prof. Isaya Jairo (kushoto) wakiondoka eneo la mahafali mara baada ya kuatunuku vyeti wahitimu 3,169 wakati wa mahafali ya 13 ya Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA) kwa Kampasi ya Dar es Salaam na Mtwara mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam. Kulia ni Afisa Mtendaji Mkuu ya Taasisi ya Uhasibu Tanzania Dkt. Joseph Kihanda.
Baadhi ya wananchi wakifuatilia shamra shamra za mahafali ya 13 ya Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA) kwa Kampasi ya Dar es Salaam na Mtwara mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam.
Na Eleuteri
Mangi-MAELEZO
WAHITIMU wa Taasisi ya
Uhasibu Tanzania (TIA) wameaswa kutumia mafunzo ya ujasiriamali waliyoyapata
chuoni hapo katika kukabiliana na changamoto ya soko la ajira na kuelekeza
mawazo yao katika kujiajiri badala ya kuajiriwa.
Hayo yamesemwa na Naibu
Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Dkt. Hamisi Mwinyimvua wakati mahafali
ya 13 ya taasisi hiyo kwa Kampasi ya Dar es salaam na Mtwara mwishoni mwa wiki jijini
Dar es Salaam.
“Mafunzo ya
ujasiriamali mliyoyapata yawe chachu ya ufanisi wenu katika kufanyakazi kwa
bidii, uadilifu, ubunifu, umakini na weledi wa hali ya juu ili kujiletea
maendeleo yenu wenyewe yenye na yenye tija kwa taifa”,
“Msingi wa mafanikio na
kuhifadhi ajira ni kufanya kazi kwa kuzingatia sheria, taratibu na kanuni,
jiepusheni na vitendo vya rushwa na ubadhirifu mkitabua kuwa rushwa ni adui wa
haki na maendeleo” alisisitiza Dkt. Mwinyimvua.
Mahafali hayo ya 13
yanajumuisha wahitimu kutoka fani za Uhasibu, Ununuzi na Ugavi, Usimamizi wa Biashara,
Uongozi wa Rasilimali Watu, Masoko na Uhusianao wa Jamii na Uhasibu wa Fedha za
Umma ambazo msingi wake ni kendesha uchumi wa taifa katika kusimamia mapato na
matumizi ya fedha za umma kwa kutumia wataalamu mbalimbali ambao wengi wao ni
tunda la Taasisi ya Uhasibu Tanzania.
Aidha, Dkt. Mwinyimvua
aliwasihi wahitimu hao kutumia elimu waliyoipata vema katika kuendeleza uchumi
wa taifa, kuboresha maisha yao na jamii inayowazunguka pamoja na kupambana na
kupambana na changamoto zinazolikabili taifa kwa kudhibiti ubadhirifu na
matumizi yasiyo sahihi ya rasilimali za taifa.
Awali akitoa taarifa
fupi kwa Mgeni Rasmi, Afisa Mtendaji Mkuu ya Taasisi ya Uhasibu Tanzania Dkt.
Joseph Kihanda alisema kuwa wapo jumla ya wahitimu 3,169 kati yao wanawake ni
1,562 sawa na asilimia 49.3 na wanaume ni 1,607 sawa na asilimia 50.7.
Idadi hiyo inajumuisha
wahitimu 441 kutoka kampasi ya Mtwara na wahitimu 2,728 kutoka kampasi ya Dar
es salaam kwa ngazi ya cheti, stashahada, shahada na shahada ya uzamili.
Dkt. Kihanda alisema
kuwa kwa mwaka wa masomo 2014/2015 Taasisi ya Uhasibu Tanzania ina jumla ya
wahitimu 6,949 kutoka kampasi za Dar es salaam, Mbeya, Singida, Mtwara, Mwanza
na Kigoma.
Kati ya wahitimu hao
idadi ya wanawake ni 3,458 ambao ni sawa na asilimia 49.8 na idadi ya wanaume
ni 3,491 ambao ni sawa na asilimia 50.2,
wahitimu kutoka kampasi ya Kigoma ni wa kwanza tangu taasisi hiyo ianzishwe
mkoani humo.
Dkt. Kihanda aliongeza
taasisi bado inaendelea na zoezi la udahili kwa mwaka wa masomo 2015/1016 kwa
ngazi ya shahada ya kwanza pamoja na wanafunzi katika ngazi ya cheti cha awali
kwa awamu ya pili mwanzoni mwa mwaka 2016.
Taasisi hiyo inatarajia
kudahili wanachuo wapatao 10,500 katika kampasi zake zote na kufanya idadi ya
wanafunzi kuongezeka kutoka 12,899 ya sasa hadi 17,739.
Kwa upande wake mwanafunzi
Cosmas Ephraim alisema kuwa amefarijika kuhitimu masomo ya shahada ya Uhasibu
mbayo ameahdi kuitumia elimu hiyo ili kutoa mchango wake katika kuendeleza
taifa liweze kuwa na maendeleo yenye tija kiuchumi kwa Watanzania wote.
No comments:
Post a Comment