Kikosi cha Simba kabla ya mchezo na Azam FC Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam leo. (Picha zote na Kassim Mbarouk-www.bayana.blogspot.com)
Kikosi cha Azam FC kilichopambana na Simba, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam leo.
Mashabiki wa Simba wakifuatilia mchezo kati ya timu yao hiyo na Azam FC.
Ubao wa matangazo ukionesha Azam FC wakiwa wamejipatia bao la kwanza lililofungwa na Nahodha John Bocco.
Ibrahim Ajib wa Simba akiwania mpira na beki wa Azam FC, Said Morad wakati wa mchezo huo, wa Ligi Kuu ya Vodacom, uliochezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam leo. Timu hizo zilitoka sare kwa kufungana mabao 2-2.
Danny Lyanga wa Simba (kushoto), akiwania mpira na Jean Mugiraneza wa Azam FC.
Danny Lyanga wa Simba (kushoto), akiwania mpira na Jean Mugiraneza wa Azam FC.
Ibrahim Ajib wa Simba akikimbia kushangilia bao lake aliloifungia timu yake hiyo, likiwa ni bao la kusawazisha dhidi ya Azam FC.
Ibrahim Ajib (mbele aliyevua fulana), akiwa na Mohamed Hussein (Tshabalala), wakishangilia bao hilo la kusawazisha dhidi ya Azam FC.
Ibrahim Ajib (kushoto), akiwa na Hassan Isihaka, wakishangilia kwa kusali bao hilo la kusawazisha dhidi ya Azam FC.
Ubao wa matokeo ukionesha Azam FC 1 na Simba SC 1.
Danny Lyanga wa Simba (kulia), akimvalisha kazu Said Morad wa Azam FC.
Ibrahim Ajib wa Simba FC akimkabili Paschal Wawa wa Azam FC.
Wachezaji wa Simba wakiondoa hatari iliyoelekezwa langoni kwao.
Shomari Kapombe wa Azam FC akiupiga kichwa mpira kuondoa hatari langoni kwa Azam FC.
Mashabiki wa Simba wakifuatilia mchezo huo.
Shomari Kapombe wa Azam FC akiuondoa mpira miguuni mwa Emery Nimubona wa Simba.
Danny Lyanga wa Simba SC akimtoka Jean Mugiraneza wa Azam FC.
Ibrahim Ajib wa Simba akifunga bao la pili kwa timu yake, huku akiwaacha golikipa Aishi Manula na beki Said Morad wa Azam FC wakiwa wamedondoka chini, wakati wa mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom, uliochezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam leo. Timu hizo zilitoka sare kwa kufungana mabao 2-2.
Ibrahim Ajib (kulia) na Danny Lyanga wote wa Simba wakikimbia kushangilia bao la pili aliloifungia timu yake hiyo.
Ibrahim Ajib na Kessy Ramadhan wote wa Simba wakishangilia bao hilo.
Ubao wa matangazo ukionesha Azam bao 1 na Simba mabao 2.
Baada ya dakika chache Azam FC walisawazisha bao hilo na hivyo ubao wa matangazo kusomeka Azam mabao 2 na Simba mabao 2.
Ibrahim Ajib akizongwa na Erasto Nyoni wa Azam FC.
Hamis Kiiza wa Simba akijaribu kumtoka Paschal Wawa wa Azam AF. Hadi mwisho wa mchezo huo, Simba ilipata mabao 2 yaliyofungwa na Ibrahim Ajib na Azam mabao 2 yaliyofungwa na John Bocco na Kipre Tchetche.
No comments:
Post a Comment