Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Rais John Pombe Joseph Magufuli akimkabidhi hati Naibu Waziri, Wizara ya Fedha na Mipango Dkt. Ashantu Kijaji mara baada ya kumuapisha leo Ikulu Jijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri, Wizara ya Fedha na Mipango Dkt. Ashantu Kijaji (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Dkt. Servacius Likwelile (kushoto), mara baada ya hafla ya kuapishwa Mawaziri na Manaibu Waziri wa Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Mhe. Rais John Pombe Joseph Magufuli. Kulia ni Mkurugenzi wa Idara Utawala Wizara ya Fedha na Mipango Deodata Makani.
Kamanda wa Kanda Maalum Dar es Salaam, Suleiman Kova (katikati) akimpongeza Naibu Waziri, Wizara ya Fedha na Mipango Dkt. Ashantu Kijaji (kushoto) mara baada ya hafla ya kuapishwa Mawaziri na Manaibu Waziri wa Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Mhe. Rais John Pombe Joseph Magufuli. Kulia ni Mkurugenzi wa Idara Utawala Wizara ya Fedha na Mipango Deodata Makani.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. John Pombe Joseph Magufuli (watano), Makamu wa Rais, Mhe. Samia Suluhu Hassan (wa tatu kushoto waliokaa), pamoja na Waziri Mkuu, Mhe. Kaasim Majaliwa Majaliwa wakiwa katika picha ya pamoja na Manaibu Waziri, leo Ikulu jijini Dar es Salaam. (Picha zote na Eleuteri Mangi-MAELEZO)
No comments:
Post a Comment