TANGAZO


Thursday, December 17, 2015

Ofisi ya Waziri Mkuu yaendesha mafunzo ya Taratibu za kiuendeshaji katika kukabiliana na maafa ya mafuriko na ukame

Mratibu wa mradi wa Msaada wa sheria kwa wanawake na watoto Bi. Hidaya O. Chikawa akichangia mada wakati wa kazi za vikundi kwenye mafuzo ya taratibu za kiuendeshaji katika kukabiliana na maafa ya mafuriko na ukame katika Ukumbi wa Tengeneza Uliopo Liwale mkoani Lindi, tarehe 17 Desemba, 2015. (Picha zote na Ofisi ya Waziri Mkuu) 
Mkuu wa Wilaya ya Liwale Mhe. Ephraim Mmbaga (wa kwanza kulia) akimsikiliza mwezeshaji wa mafunzo ya taratibu za kiuendeshaji katika kukabiliana na maafa ya mafuriko na ukame Bw. Wilhelm Kiwango kutoka Chuo Kikuu cha Dodoma Idara ya Mazingira. Desemba17, 2015 Liwale Lindi.
Mhadhiri Msaidizi wa masuala ya Mazingira Bw. Wilhelm Kiwango akitoa mafunzo juu taratibu za kiuendeshaji katika kukabiliana na maafa ya mafuriko na ukame kwa baadhi ya Watendaji wa Serikali Wilayani Liwale mkoani Lindi yaliyofanyika Desemba 17, 2015. 
Mkuu wa Wilaya ya Liwale Mhe. Ephraim Mmbaga (wa kwanza kulia) akisalimiana na Mratibu wa Taifa wa Mradi wa Kuimarisha Taarifa za hali ya hewa na Mifumo ya Taadhari Bw. Daniel Alfei kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu Idara ya Uratibu wa Maafa wakati wa mafunzo yaliyoratibiwa na ofisi hiyo Wilayani Liwale mkoani Lindi, tarehe 17 Desemba, 2015. 
Mkuu wa Wilaya ya Liwale Mhe. Ephraim Mmbaga akifungua mafunzo ya taratibu za kiuendeshaji katika kukabiliana na maafa ya mafuriko na ukame yaliyoratibiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu katika Ukumbi wa Tengeneza Wilayani Liwale Lindi, tarehe 17 Desemba, 2015. 

No comments:

Post a Comment