Na Mwandishi wetu
AKIZUNGUMZA na
uongozi wa Wizara na Taasisi Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji aliwaasa viongozi kutekeleza
majukumu waliyokabidhiwa na kuhakikisha bajeti ya Serikali inalenga vipaumbele
vinavyogusa wananchi katika kutekeleza ahadi ya Serikali.
Katibu Mkuu Wizara
ya Fedha na Mipango na Mlipaji Mkuu wa Serikali
Dkt. Servacius Likwelile akitoa
ufafanuzi kwa Naibu Waziri Wizara ya Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji
kabla ya kuanza majadiliano na watendaji wa Wizara na Taasisi.
Naibu Waziri, Wizara ya Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji akiongea na watendaji wa Wizara na Taasisi alipokutana nao katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango. Naibu Waziri, Wizara ya Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji akijadiliana na watendaji wa Wizara na Taasisi kuhusu masuala mbalimbali ya Wizara pamoja na Taasisi zilizo chini ya Wizara. (Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Wizara ya Fedha na Mipango)
No comments:
Post a Comment