TANGAZO


Sunday, December 13, 2015

Mkondo wa pili wa uchaguzi Ufaransa

Image copyrightReuters
Image captionWananchi wa Ufaransa wanapiga kura katika duru ya pili ya uchaguzi wa serikali za majimbo
Wananchi wa Ufaransa wanapiga kura katika duru ya pili ya uchaguzi wa serikali za majimbo, ambapo chama cha siasa kali za mrengo wa kulia, National Front, kinatarajiwa kupata wingi kwa mara ya kwanza katika angalu jimbo moja la nchi.
Chama kinachoongozwa na Bibi Marine Le Pen, kilipata kura nyingi kabisa katika duru ya kwanza juma lilopita.
Tangu wakati huo, chama tawala cha Socialist, kimejitoa katika sehemu kadha za nchi, ili wafuasi wake wakipigie kura chama cha mrengo wa kulia, cha Bwana Sarkozy, na hivyo wakishinde chama cha National Front.
Image copyrightAFP
Image captionKiongozi wa FN Marine Le Pen
Huu ndio uchaguzi mkubwa kabisa nchini Ufaransa, kabla ya uchaguzi wa rais wa mwaka 2017.
Chama hicho cha National Front kilipata asilimia 27.73% ya kura zote katika mkondo wa kwanza juma lililopita .
Chama cha aliyekuwa rais Sarkozy, Republican kilipata asilimia 26.65% ya kura huku chama cha rais wa sasa Francois Hollande cha Socialists kikimaliza katika nafasi ya tatu na asilimia 23.12%.
Image copyrightAFP
Image captionNational Front kilipata asilimia 27.73% Republican kinachoongozwa na Sarkozy kikimaliza katika nafasi ya pili na asilimia 26.65%
Kiongozi wa FN Marine Le Pen, anawania katika jimbo la kaskazini la Nord-Pas-de-Calais-Picardie.
Mwanaye bi Marion Marechal-Le Pen, anawania kuiwakilisha jimbo la Provence-Alpes-Cote d'Azur kusini mwa Ufaransa.
Wawili hao walishinda asilimia 40 % ya kura za mkondo wa kwanza.

No comments:

Post a Comment