Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-Utumishi na Utawala Bora Mhe. Anjella Kairuki (Mb) akiweka saini katika kitabu cha wageni baada ya kuwasili rasmi katika ofisi yake leo Jumamosi.
Kaimu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais-Utumishi na Utawala Bora Bw. Tixon Nzunda (aliyesimama) akimkaribisha Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-Utumishi na Utawala Bora Mhe. Anjella Kairuki (wa kwanza kutoka kulia) kuongea na watendaji wa ofisi yake baada ya kuapishwa kushika wadhifa huo na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-Utumishi na Utawala Bora Mhe. Anjella Kairuki (Mb) (kulia) akizungumza na watendaji wa Ofisi ya Rais-Utumishi na Utawala Bora mara baada kufika ofisini kwake kuanza kazi leo Jumamosi. (Picha zote na James Katubuka Mwanamyoto, Ofisa Habari, Ofisi ya Rais-Utumishi)
Na Mwandishi wetu
WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya
Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Angella Kairuki (MB) ameanza
kazi rasmi Leo Jumamosi Desemba 12/2015 mara baada ya kuapishwa Ikulu na Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli.
Mhe. Kairuki akiongea na
watendaji wa Wizara yake alielekeza masuala ya kiutumishi ikiwamo kusimamia nidhamu ya kazi ni jambo la
msingi hivyo kutumia daftari la
mahudhurio peke yake haitoshi.
“Tutumie Teknolojia ya
Habari na Mawasiliano (TEHAMA) ili kubaini Watumishi wanaoiba muda wa kazi wa
Serikali” Mhe. Kairuki alisisitiza na kusema kazi lazima zitekelezwe kwa kiwango cha juu.
Mhe. Waziri Kairuki alisema suala
la kufanya kazi kwa kushirikiana na taasisi nyingine za Serikali ni muhimu kwa
kuwaelekeza watendaji wa Wizara yake kushirikiana na Wakala ya Usajili, Ufilisi
na Udhamini (RITA) kubaini taarifa za watumishi wanaofariki ili wafutwe katika
orodha ya malipo.
Mhe. Waziri Kairuki alisema
ushirikiano katika kazi ni jambo la msingi ili kushauriana katika kutatua
changamoto zinazojitokeza katika utekelezaji wa masuala mbalimbali ya
kiutumishi na kuondoa malalamiko.
Awali, Kaimu Katibu Mkuu Ofisi
ya Rais-Utumishi na Utawala Bora Bw. Tixon Nzunda akimkaribisha Mh. Waziri
Kairuki kuongea na watendaji wa Wizara alisema waajiri wote nchini
walishaelekezwa kufanya kazi ya kusafisha takwimu zisizohitaji katika Mfumo
Shirikishi wa Taarifa za Kiutumishi na Mishahara Serikalini (HCMIS).
Bw. Nzunda alisema Watumishi
wote wenye takwimu chafu (takwimu zisizohitajika) katika mfumo wa HCMIS watafutwa
baada ya kukamilika kwa zoezi hilo ifikapo mwisho wa mwezi Desemba 2015 na endapo
kutakua na mwajiri atakayekua na takwimu chafu atawajibika kwa kushindwa
kutekeleza agizo hilo.
No comments:
Post a Comment