TANGAZO


Friday, December 11, 2015

IS lajipatia zaidi ya $500m kupitia mafuta

Image copyrightIS propaganda
Image captionIslamic State
Kundi la wapiganaji wa Islamic State limejipatia zaidi ya dola milioni 500 kupitia uuzaji wa mafuta kulingana na afisa mmoja wa wizara ya fedha nchini Marekani.
Mteja wake mkubwa amekuwa rais wa Syria Bashar al Assad,licha ya vita vya kutaka kuiangusha serikali,Adam Szubin ameambia BBC.
IS imeiba takriban dola bilioni moja kutoka maeneo inayodhibiti.
Muungano unaoongozwa na Marekani umekuwa ukishambulia maeneo ya kundi hilo ikiwemo maeneo ya mafuta nchini Syria na Iraq kwa zaidi ya mwaka mmoja sasa.
Image captionIraq,Syria
Afisa anayesimamia fedha katika kundi hilo aliuawa hivi majuzi katika mashambulio hayo kulingana Pentagon.
''Pande hizo mbili zinakabiliana vilivyo lakini pia zinashirikiana katika biashara zinazogharimu mabilioni ya madola'', alisema Szubin kuhusu Syria na IS katika tamko lililotolewa na kituo cha habari cha Reuters.
Kundi hilo limedaiwa kutengeza zaidi dola milioni 40 kwa mwezi kutoka kwa biashara hiyo ya mafuta ikiwemo wanunuzi kutoka Uturuki.
Ukatizaji wa fedha wa kundi hilo ulikuwa miongoni mwa mikakati ya muungano huo kulishinda kundi hilo.
Image copyrightAP
Image captionIslamic State
Ikilinganishwa na makundi mengine ya kigaidi ,IS halikutegemea ufadhili kutoka kwa wafadhili wa kigeni bali lilijapatia fedha kutokana na oparesheni zake, alisema Szubin.
Muungano unaoongozwa na Marekani hivi majuzi ulizindua kampeni za kijeshi kwa jina Wave 2,na kuimarisha mashambulio ya angani katika visima vya mafuta vinavyomilikiwa na IS,viwanda vya kusafishia mafuta na magari yanayotumiwa na kundi hilo.

No comments:

Post a Comment