Naibu Katibu Mkuu anayeshughulikia Sera Prof. Adolph Mkenda akifafanua jambo ofisini kwa Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Mpango mara baada ya kuwasili Wizarani hapo jana jijini Dar es salaam.
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji akitoa taarifa fupi kwa Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Mpango (wa kwanza kulia) ikiwa ni sehemu ya ukaribisho kwa Waziri huyo Wizarani hapo.
Watendaji wa Wizara ya Fedha na Mipango wakielezea majukumu ya Idara na Vitengo katika mkutano na Waziri wa Fedha na Mipango Mhe.Dkt. Philip mara baada ya kuwasili Wizarani hapo jana jijini Dar es Salaam.
Watendaji wa Wizara ya Fedha na Mipango wakielezea majukumu ya Idara na Vitengo katika mkutano na Waziri wa Fedha na Mipango Mhe.Dkt. Philip mara baada ya kuwasili Wizarani hapo jana jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Mpango akionesha kadi aliyoipokea kutoka kwa viongozi kwaniaba ya watumishi wa Wizara hiyo yenye lengo la kumpongeza kwa kuteuliwa kushika wadhifa huo. Wa kwanza kulia ni Kaibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Dkt. Servacius Likwelile na Mkurugenzi Idara ya Utawala na Rasilimaliwatu Bi. Deodatha Makani (katikati).
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Mpango akionesha kadi aliyoipokea kutoka kwa viongozi kwaniaba ya watumishi wa Wizara hiyo yenye lengo la kumpongeza kwa kuteuliwa kushika wadhifa huo. Wa kwanza kulia ni Kaibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Dkt. Servacius Likwelile na Mkurugenzi Idara ya Utawala na Rasilimaliwatu Bi. Deodatha Makani (katikati). (Picha zote na Kitengo cha Mawasiliano Wizara ya Fedha na Mipango)
WATUMISHI Wizara ya
Fedha na Mipango wameaswa kufanya kazi kwa weledi na kuwekeza nguvu zaidi katika ukusanyaji
mapato ili kukuza uchumi wa nchi na kuifanya nchi iwe kitovu cha uchumi Barani
Afrika.
Hayo yamesemwa na Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt.
Philip Mpango alipokuwa akiongea na watendaji wa Wizara hiyo alipowasili
Wizarani hapo mara baada ya kuapishwa jana Ikulu jijini Dar es Salaam.
Katika mazungumzo yake na watendaji hao, Mhe. Dkt. Mpango, aliuagiza
uongozi wa Wizara yake kuunda na
kisimamia sera za mfumo wa ukusanyaji
kodi ambao utabaki kuwa rafiki kwa wafanyabiashara ili kukuza biashara
na uwekezaji nchini.
“Ili kutekeleza
kutekeleza ukusanyaji wa kodi kwa kutumia mfumo rafiki kwa wafanyabiashara na
Serikali, Wizara inawajibu wa kusimamia na kukuza uchumi ambao utawanufaisha
wananchi walio wengi, kwa kuhakikisha kodi zote ndogondogo ambazo ziko chini na
nje ya Wizara, ambazo ni kero kwa wanachi wa hali ya chini zinapatiwa ufumbuzi
kwani wananchi hao nao wanastahili maisha mazuri” Alisema Mhe. Dkt. Mpango.
Waziri Dkt. Mpango aliwasisitiza
watendaji kufanya kazi kwa bidii, maarifa na weledi ili nchi iweze kupiga hatua
kwa kuzingatia nidhamu katika kufanya kazi ambayo ni dhamana walizokabidhiwa.
Naye Naibu Waziri
Wizara ya Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji aliwahimiza watendaji wa
wizara hiyo kufanyakazi kwa umoja na mshikamano waliokuwa nao katika utendaji
kazi ili kuleta maendeleo yenye tija huku akisisitiza kuwa wizara hiyo ndiyo
msingi katika kukuza uchumi wa nchi.
Kwa upande wake Katibu
Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango na Mlipaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Servacius Likwelile
aliwapongeza Viongozi hao wapya wa Wizara kwa kuteuliwa kwao kuiongoza Wizara
ambayo ndiyo muhimili wa Serikali.
Aidha, Dkt. Likwelile
alitoa wito kwa watendaji wa wizara hiyo kuzingatia maagizo ya Mhe. Waziri kwa
maendeleo ya nchi ili kulinda hadhi na heshima ya wizara.
Imetolewa
na Kitengo cha Mawasiliano
Wizara
ya Fedha na Mipango
28
Desemba, 2015

No comments:
Post a Comment