TANGAZO


Monday, November 30, 2015

Viongozi wa Ofisi ya Rais-Utumishi wa Umma wala kiapo cha uadilifu

Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais-Utumishi Bw. Tixon Nzunda (kushoto) akielekeza namna ya kutoa Ahadi ya Uadilifu kwa watumishi wa Umma zoezi lililofanyika mapema leo Ofisi ya Rais-Utumishi jijini Dar es Salaam. (Picha zote na Happy hayo-Utumishi wa Umma)
Wakuu wa Idara na Vitengo wa Ofisi ya Rais-Utumishi wakiweka Ahadi za Uadilifu katika fomu maalum wakati wa zoezi hilo lililoratibiwa na Katibu Mkuu Ofisi ya Rais-Utumishi Bw.HAB Mkwizu mapema leo jijini Dar es Salaam. 
Wakuu wa Idara na Vitengo wa Ofisi ya Rais-Utumishi wakila kiapo cha  Uadilifu kwa Katibu Mkuu Ofisi ya Rais-Utumishi Bw.HAB Mkwizu (kushoto) mapema leo. 
Katibu Mkuu Ofisi ya Rais-Utumishi Bw.HAB Mkwizu (kushoto) akimkabidhi Mkurugenzi wa Idara ya Ukuzaji wa Maadili wa Ofisi ya Rais-Utumishi Bw.Mathew Kirama fomu maalum ya kuweka Ahadi ya Uadilifu kwa Watumishi wa Umma mapema leo ofisini kwake. 
Katibu Mkuu Ofisi ya Rais-Utumishi Bw.HAB Mkwizu akitia saini fomu ya Ahadi ya Uadilifu kwa watumishi wa Umma ya Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais-Utumishi Bw. Tixon Nzunda (kulia) ofisini kwake mapema leo.

No comments:

Post a Comment