TANGAZO


Sunday, November 22, 2015

Tope la sumu lakaribia ufukweni Brazil

Image copyrightAFP
Image captionTope la sumu lakaribia ufukweni Brazil
Tope la taka ya sumu linalosafirishwa na mto Rio Doce nchini Brazil linatarajiwa kuwasili kwenye ufukwe wa bahari ya Atlantic saa chache zinazokuja.
Image copyrightAssociacao dos Pescadores e Amigos do Rio Doce
Image captionTope hilo lina sumu inayotokana na madini ya chuma
Tope hilo la sumu ya chuma lilitokea baada ya bwawa lililoko karibu na timbo la madini ya chuma kuvunja kingo zake majuma mawili yaliyopita.
Inakisiwa kuwa tope hilo limesafirishwa zaidi ya kilomita 500 kutoka eneo la milimani.
Image copyrightReuters
Image captionUdongo huo umesombwa umbali wa kilomita 500 tangu bwawa hilo kuvunjika zaidi ya wiki mbili zilizopita.
Kampuni inayomiliki mgodi huo (- Samarco -) imekuwa ikijenga vizuizi katika mto Rio Doce ikijaribu kuwakinga wanyama na mimea kutoka kwa udongo huo wenye taka nyingi ya chuma.
Udongo huo umesombwa umbali wa kilomita 500 tangu bwawa hilo kuvunjika zaidi ya wiki mbili zilizopita.
Image copyrightReuters
Image captionEneo ambapo mto huo unaingilia bahari ni mazingira muhimu kwa samaki na kasa
Eneo ambapo mto huo unaingilia bahari ni mazingira muhimu kwa samaki na kasa mbali na viumbe wengine walio kwenye hatari ya kuangamia.
Wafanyikazi wa kampuni hiyo wamekuwa wakiwashika kasa waliokuwa wanataga mayai na kuwahamisha katika maeneo salama kabla ya udongo huo kuwasili.

No comments:

Post a Comment