TANGAZO


Wednesday, November 18, 2015

Shilingi bilioni mbili kutengwa kwa ajili ya kusaidia utafiti wa zao la Korosho

Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Korosho Tanzania, Mudhihir Mudhihir, akizungumza wakati alipokuwa akiufunga mkutano wa 3 wa Kimataifa wa Korosho, Dar es Salaam jana. Katikati ni Mtafiti Kiongozi wa Korosho nchini na Mratibu wa Kanda, Profesa Peter Masawe na kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa Utafiti na Maendeleo wa Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika, Dk. Hussein Mansour. (Picha na Kassim Mbarouk-www.bayana.blogspot.com)

Na Lorietha Laurence-Maelezo
Bodi ya Korosho Tanzania imeadhima kutoa asilimia 7 ya mapato yake sawa na shilingi bilioni mbili kwa ajili ya kusaidia utafiti wa zao hilo  unaofanywa na  kituo cha utafiti cha Naliendele.

Akiongea wakati wa kufunga kwa mkutano wa tatu wa kimataifa  uliowahusisha wadau kutoka nchi mbalimbli duniani ,Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Korosho Tanzania Bw. Muhidhiri Muhidhiri amesema kuwa   changamoto kubwa wanayokabiliana nayo ni ukosefu wa fedha kwa ajili ya  kuendeshea utafiti wa zao la korosho unaofanywa na kituo cha Naliendele na hivyo wamejipanga  kwa kuchangia kiasi cha mapoto ili kufanikisha tafiti hizo.

Muhidhiri  aliongeza kuwa licha ya changamoto za ukosefu wa fedha wamepata fursa ya kujifunza mambo mbalimbali kupitia mkutano huo ikiwemo maadhimio ya uzalishaji bora wa zao hilo, namna ya kutatua matatizo ya magonjwa yanayoikumba korosho,dawa asilia zitakazosaidia katika kulinda mbegu, na njia bora  ya uzalishaji.

“Mkutano ulikuwa wa kisayansi kwa kuwa umeangalia  mambo ya kiutafiti na teknolojia katika uzalishaji wa zao la korosho  hivyo ninaamini baada ya hapa ni kuanza utekelezaji wa yale tuliyoyajadili na kufanya vizuri zaidi ” alisema Muhidhiri.

Kwa upande wa Mtafiti Mkuu wa Masuala ya korosho  Prof.Peter Masawe ameeleza kuwa mkutano huo wa wadau umewapa fursa ya kufahamu mambo mazuri katika uboreshaji na uzalishaji wa zao la korosho katika kiwango kizuri na kilicho bora.

Pia alibainisha kuwaTanzania ndiyo nchi yenye mtafiti anayetegemewa  katika masuala ya korosho na hivyo kupitia  mkutano huo wadau wamepata fursa ya kufahamu  mambo ya msingi kama vile mbegu bora zinazozalishwa nchini  ,mbegu fupi, mbegu zinazostahimili  ukame pamoja na kukopa teknolojia ya uzalishaji.

“Mkutano huu umetoa fursa kwa wadau kujua mambo muhimu kuhusu mbegu ukizingatia Tanzania ndiyo nchi pekee barani Afrika inayozalisha mbegu bora hivyo natumai wajumbe wataenda kutendea kazi yale yote waliyojifunza hapa kwetu na nasisi pia tutayafaniya kazi yale tuliyoyapata kutoka kwao ” alisema  Prof Masawe.


Mkutano huo wa kimatifa wa wadau wa Korosho umefanyika kwa mara ya pili nchini  ambapo mara ya kwanza ilikuwa mwaka 1997 na hivyo kuipa fursa nchi  ya kujitangaza kupitia  sekta ya kitalii kwa kuwahamasisha  wadau waliohudhuria mkutano huo kutembelea sehemu za vivutio  ikiwemo Bagamoyo na Zanzibar.

No comments:

Post a Comment