Mashabiki wa Yanga wakifuatilia mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom kati ya timu yao hiyo dhidi ya Azam FC, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam leo. (Picha zote na Kassim Mbarouk-www.bayana.blogspot.com)
Purukushani kwenye lango la Azam FC.
Mashabiki wa Azam wakifuatilia mchezo huo, dhidi ya Yanga.
Thaban Kamusoko wa Yanga (kulia), akiudhibiti mpira huku akifuatwa na Aggey Morris wa Azam FC.
Thaban Kamusoko wa Yanga (kulia), akiudhibiti mpira huku akifuatwa na Aggey Morris wa Azam FC.
Donald Ngoma wa Yanga akipiga tik tak kufunga bao kwa timu yake dhidi ya Azam FC, wakati wa mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam leo. Anayeangalia kulia ni mchezaji mwenzake, Amis Tambwe na kushoto ni Pascal Wawa wa Azam. Timu hizo zimetoka sare kwa kufungana bao 1-1.
Wachezaji wa Yanga wakishangilia bao hilo, lililofungwa na Donald Ngoma.
Ubao wa matokeo ukionesha Yanga bao 1 Azam FC 0.
Mashabiki wa Azam wakishangilia timu yao.
Mashabiki wa Yanga wakiwafanyia utani mashabiki wa Azam FC kwa kuwaletea kiroba cha kujaza mabao kwenye mchezo huo.
Simon Msuva wa Yanga akiudhibiti mpira katika mchezo huo.
Amis Tambwe wa Yanga akiutuliza mpira huku akifuatwa na Farid Mussa wa Azam FC.
Pascal Wawa wa Azam FC, akiudhibiti mpira huku akifuatwa na SalumTelela wa Yanga.
Pascal Wawa wa Azam FC na SalumTelela wa Yanga, wakiwania mpira.
Mpigapicha wa Azam TV akiwa kazini kuchukua picha za kuurusha mchezo huo.
Pascal Wawa wa Azam FC na Mwinyi Haji wa Yanga, wakiwania mpira wa juu.
Mashabiki wa Yanga wakifuatilia mchezo huo.
Madaktari wakimshona Mbuyu Twitwe baada ya kupasuka juu ya jicho la kushoto wakati wa mchezo huo.
Ubao wa matokeo ukionesha Yanga bao 1 na Azam FC bao 1, hadi mwisho wa mchezo huo.

No comments:
Post a Comment