TANGAZO


Tuesday, October 13, 2015

Euro:England, Hispania zashinda tiketi


Image copyrightEPA
Image captionEngland wakata tiketi kushiriki michuano ya Euro 2016

Timu ya taifa ya England imeshinda mchezo wake wa kumi katika michezo kumi ya kusaka tiketi ya kushiri katika michuano ya Euro mwaka 2016 huko nchini Ufaransa.
England ambao tayari wamefuzu kushirikia michuano ijayo ya ulaya imewachapa Lithuania kwa mabao 3-0 kwa mabao ya Ross Barkley golikipa Giedrius Arlauskis akijifunga bao la pili na Alex Oxlade-Chamberlain akifunga bao la ushindi.
Hispania nao wakawachapa Ukraine kwa bao 1-0 bao pekee la Hispania likifungwa na Pérez Martínez katika dakika ya 21 ya mchezo.
Matokeo mengine ya michezo hiyo ya kufuzu kwa michuano ya ulaya
Belarus 0 – 0 Macedonia
Luxembourg 2 – 4 Slovakia
Estonia 0 – 1 Switzerland
San Marino 0 – 2 Slovenia
Austria 3 – 0 Liechtenstein
Russia 2 – 0 Montenegro
Sweden 2 – 0 Moldova

No comments:

Post a Comment