TANGAZO


Tuesday, October 13, 2015

Dk. Magufuli asema wapinzani wanune, wacheka yeye ndiye Rais 2015, Amfagilia Nape Jimbo la Mtama

Mgombea Urais wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. John Magufuli akimnadi kwa wananchi mgombea ubunge wa Jimbo la Mtama, ambaye pia Katibu wa Itikadi na Uenezi wa chama hicho, Nape Nnauye mjini Mtama jana. Akihutubia mjini Mtama, amesema kuwa Wapinzani Wanune, Wacheke yeye ndiye Rais 2015 na atahakikisha anafanya kazi kwa kuwaletea mafanikio watanzania.
Moja ya mabango katika mkutano wa kampeni mjini Mtama.
Mgombea ubunge Jimbo la Mtama, Nape Nnauye akimuombeakwa Wananchi  kura za ndio  katika mkutano wa kampeni mjini Mtama.
Dk. Magufuli akifurahi wakati Nape Nnauye akimmwagia sifaa za kufaa kuwa Rais  wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakati wa mkutano wa kampeni mjini Mtama.
Warembo wafuasi wa CCM wakitabasamu huku wakiwa wamejiremba wakati wa mkutano wa kampeni kwenye Uwanja wa Mpilipili mjini Lindi jana.

Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM, Mke wa Rais, Mama Salma Kikwete akimuombea kwa wananchi kura za ndiyo Dk Magufuli wakati wa mkutano wa kampeni kwenye Uwanja wa Mpilipili mjini Lindi jana.
Mfano wa karatasi la kupigia kura likionesha jinsi watu wanavyotakiwa kumpigia kura za ndiyo Mgombea wa Tanzania kupitia CCM, Dk Masgufuli na mgombea mwenza, Samia Suluhu Hassan katika mkutano huo.
Dk. Magufuli akihutubia wananchi katika Mji wa Nachingwea Asubuhi saa 2:30 katika mkutano wa kampeni.
Wananchi wa Nachingwea wakisashangilia baada ya kufurahishwa na ahadi za Dk. Magufuli kwao.
Wananchi wakinyoosha mikono kukubali kumpigia Dk Magufuli na Mgombea ubunge Jimbo la Nachingwea, Hassan Massala.
Dk. Magufuli akimnadi kwa wananchi mgombea ubunge Jimbo la Nachingwe wakati wa mkutano wa kampeni mjini Nachingwea jana asubuhi.
Dk. Magufuli akimnadi kwa wananchi mgombea ubunge Jimbo la Ruangwa wakati wa mkutano wa kampeni mjini Ruangwa jana.
Baadhi ya kadi zilizorudishwa na waliotoka upinzani, zikiwa zimesambazwa baada kutangaza kujiunga na CCM wakati wa mkutano wa kampeni mjini Ruangwa.
Mmoja wa waliokuwa wanachama wa upinzania akielezea mbele ya Dk. Magufuli sababu zilizomfanya aihame CUF na kujiunga na CCM, wakati wa mkutano wa kampeni mjini Ruangwa jana. Moja ya sababu alizozitoa ni kwamba ni chama cha uhuni na fujo pia hakijaweka mgombea urais.
Mwenyekiti wa CCM, Mkoa wa Lindi, Mzee Ali Mtopa akifungua mkutano wa kampeni kabla ya kumkaribisha kujinadi Dk Magufuli.
Mmoja wa wananchi Jimbo la Mtama akiwa amejichora kichwani neno CCM.
Msanii Ali Kiba akitumbuiza wakati wa mkutano wa kampeni mjini Mtama.
Dk. Magufuli akisalimiana na Msanii Ali Kiba.
Dk. Magufuli akiunguruma katika Jimbo la Mtama ambapo alimnadi Nape Nnauye kwa kuwaambiwa wananchi wasije wakafanya makosa kutompigia kura za ndiyo Nape ambaye alimwita kuwa ni mpiganaji jasiri na hapendwi na mafisadi kwa sababu anapingana nao waziwazi.
Jisomee mwenyeeeeeweeeeee
Dk. akimwagia Nape sifa lukuki kwa wananchi wakati wa mkutano wa kampeni Jimbo la Mtama.
Wananchi wa Jimbo la Mtama wakinyoosha mikono ikiwa ni ishara ya kukubali wakuwapigia kura za ndiyo Dk Magufuli na Nape wakati wa mkutano wa kampeni Jimbo la Mtama, mkoani Lindi.
Ni furaha iliyoje kwa wakazi wa Mtama.
Dk. Magufuli akimvisha kofia aliyekuwa dereva wa Mgombea ubunge Jimbo la Mtama kupitia Chadema, Seleman Mathew, baada ya kutangaza kuchana na chama hicho na kujiunga na CCM katika kiutano wa kampeni Jimbo la Mtama.
Wasanii Temba na Chege wakifanya vitu vyao wakati wa mkutano wa kampeni kwenye Uwanja wa Mpilipili mjini Lindi jana.
Dk. Magufuli akisalimiana na Mke wa Rais, Salma Kikwete wakati wa mkutano wa kampeni kwenye Uwanja wa Mpilipili. 
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi ya CCM, ambaye pia ni Mratibu wa Kampeni za Mgombea urais wa Tanzania kupitia CCM, Dk. Magufuli (katika), Abdallah Bulembo.
Yamoto Band akitumbuiza wakati wa mkutano wa kampeni mjini Lindi.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe akimpigia kamnpeni Dk Mgufuli wakati wa mkutano wa kampeni mjini Lindi jana.
Sehemu ya umati wa wananchi wakati wa mkutano wa kampeni za CCM mjini Lindi jana.
Dk. Magufuli akijinadi kwa wananchi mjini Lindi jana.
Dk. Magufuli akimnadi Mgombea ubunge Jimbo la Lindi Mjini, Hassani Kaunje.
Malkia wa Mipasho, Khadija Kopa akitumbuiza wakati wa mkutano huo.
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Lindi, Ali Mtopa akicheza taarabu hiyo. (Picha zote na Richard Mwaikenda;Kamanda wa Matukio Blog)

No comments:

Post a Comment