Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bibi. Sihaba Nkinga (kushoto) akimsikiliza kijana ambaye ni Katibu wa Saccoss ya Vijana ya Bega kwa Bega Bi. Mabone James alipokutana nae katika ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza walipofika kujitambulisha kwa Mkuu wa Mkoa huyo kabla ya kufungua Mafunzo ya Wawezeshaji wa Kitaifa wa Stadi za Maisha kanda ya ziwa jana jijini Mwanza.
Mkurugenzi Maendeleo ya Vijana kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bw. James Kajugusi (kushoto) akifafanua jambo walipotembelea ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Bw. Magesa S. Mulongo (kulia) kabla ya kufungua Mafunzo ya Wawezeshaji wa Kitaifa wa Stadi za Maisha kanda ya ziwa jana jijini Mwanza. Wa pili kushoto ni Katibu Mkuu Wizara hiyo Bibi. Sihaba Nkinga, na wapili kulia ni Afisa Vijana Bibi. Diana Kasonga.
Mwezeshaji wa kitaifa wa stadi za maisha Bibi. Octavina Kiwone (kulia) akimkaribisha mgeni rasmi katika Mafunzo ya Wawezeshaji kitaifa jana jijini Mwanza. Wapili kulia ni Mgeni rasmi katika Mafunzo hayo Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bibi. Sihaba Nkinga, na kushoto ni Mkurugenzi wa Vijana Bw. James Kajugusi huku wa wapili kushoto ni Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Mwanza Bw. Moses Pesha.
Mkurugenzi Maendeleo ya Vijana kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bw. James Kajugusi (kushoto) akizungumza na Vijana (hawapo pichani) wakati wa ufunguzi wa Mafunzo ya Wawezeshaji wa Kitaifa wa Stadi za Maisha jana Jijini Mwanza. Kulia ni Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bibi. Sihaba Nkinga, na katikati ni Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Mwanza Bw. Moses Pesha.
Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bibi. Sihaba Nkinga akifungua Mafunzo ya Wawezeshaji wa Kitaifa wa Stadi za Maisha kanda ya ziwa jana jijini Mwanza. Kulia ni Mwezeshaji wa kitaifa wa stadi za maisha Bibi. Octavina Kiwone.
Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bibi. Sihaba Nkinga (waliokaa katikati) katika picha ya pamoja na Wawezeshaji wa kitaifa wa stadi za maisha jana jijini Mwanza. Kushoto waliokaa ni Mkurugenzi Maendeleo ya Vijana Bw. James Kajugusi na wapili kulia waliokaa ni Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Mwanza Bw. Moses Pesha.
Wawezeshaji
wa kitaifa wa Stadi za Maisha wakiangalia mbinu mbalimbali za uwezeshaji
zilizowekwa ukutani wakati wa Mafunzo ya Wawezeshaji wa Kitaifa wa Stadi za
Maisha jna Jijini Mwanza. (Picha zote na
Genofeva Matemu – Maelezo, Mwanza)
WAWEZESHAJI wa
Kitaifa wa stadi za maisha wametakiwa kuwasaidia vijana kujitoa katika mitazamo
hasi na kuleta mabadiliko chanya katika jamii kwani vijana ni nguvu kazi ya Taifa letu.
Rai hiyo imetolewa na
Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bibi. Sihaba Nkinga
alipokua akifungua Mafunzo ya siku nane kwa Wawezeshaji wa Kitaifa wa Stadi za
Maisha jana Jijini Mwanza.
“Vijana
wakijiimarisha katika shughuli za kijamii na kiuchumi wataepuka kuzungukwa na
vihatarishi vya maisha kama vile HIV/AIDS, mimba zisizotarajiwa pamoja na
madawa ya kulevya hivyo kujenga nchi kwa kutumia nguvu kazi ya vijana” alisema
Bibi. Nkinga.
Aidha bibi.Nkinga
amesema kuwa matarajio ya serikali ni kuona vijana wa kitanzania wanajitambua kua wao ni nani, wanaenda wapi, na
watafikaje kwa kujua uwezo na udhaifu binafsi walionao ili waweze kupanga malengo waliyonayo na
kuyatekeleza kulingana na fursa zilizopo.
Akizungumza wakati wa
ufunguzi wa Mafunzo hayo, Mkurugenzi Maendeleo ya Vijana kutoka Wizara a
Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bw. James Kajugusi amesema kuwa lengo la
Mafunzo hayo kwa vijana ni kupata waelimishaji wa stadi za maisha wa kitaifa
kwa kutumia vijana walio nje ya shule.
Aidha Bw. Kajugusi
alisema kuwa Mafunzo haya yamelenga kupata waelimishaji wa kitaifa wa stadi za
maisha watatu kutoka kila mkoa katika mikoa yote ya Tanzania bara ambao
watawafikia waelimishaji rika wa kila mkoa ili kuweza kufikisha elimu
waliyoipata kwa vijana wa rika mbalimbali katika Mikoa, Wilaya, kata, vijiji,
vitongoji, mitaa, vijiweni na sehemu rasmi za shughuli za vijana.
Naye Katibu Tawala
Mkoa wa Mwanza Dr. Faisal H. Issa amewashukuru waandaaji wa Mafunzo hayo kwa
kuchagua kuanzisha mafunzo hayo kwa mikoa ya kanda ya Ziwa kwani ni jambo la
neema kwa mikoa hiyo hivyo kuwataka Wawezeshaji wa Kitaifa Mikoa ya Kanda ya
Ziwa kutumia nafasi waliyopewa kubadili fikra hasi za vijana katika mikoa ya
kanda ya ziwa.









No comments:
Post a Comment