Mkurugenzi
Idara ya Habari Bw. Assah Mwambene akizungumza na waandishi wa habari (hawapo
pichani) leo jijini Dar es Salaam kuhusu Timu ya Taifa itakayoshiriki katika
Michezo ya Afrika (All Africa Games) Congo Brazaville. Kushoto ni Mkurugenzi Msaidizi
Maendeleo ya Michezo Bibi. Juliana Yassoda na kulia ni Mkuu wa kitengo cha
Mawasiliano Serikalini kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo
Bibi. Concilia Niyibitanga.
Mkurugenzi Msaidizi Maendeleo ya Michezo Bibi. Juliana Yassoda (kushoto) akifafanua jambo wakati wa Mkutano na waandishi wa habari kuhusu Timu ya Taifa itakayoshiriki katika Michezo ya Afrika (All Africa Games) Congo Brazaville. Kulia ni Mkurugenzi Idara ya Habari Bw. Assah Mwambene. (Picha zote na Genofeva Matemu - Maelezo)
Na Genofeva Matemu
- Maelezo
TIMU ya Taifa
ya Tanzania yenye wachezaji wapatao 30 na viongozi 7 wa michezo mbalimbali
inatarajia kuondoka Jijiji Dar es Salaam kesho jioni na ndege maalum kuelekea
Congo Brazaville kushiriki katika Michezo ya Afrika (All Africa Games)
itakayofunguliwa rasmi Septemba 4, 2015.
Hayo yamesemwa
leo Jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi Idara ya Habari
Bw. Assah Mwambene wakati wa Mkutano na Waandishi wa habari kuhusu Timu ya
Taifa itakayoshiriki katika Michezo ya Afrika (All Africa Games) huko Congo
Brazaville.
Bw. Mwambene
amesema kuwa Tanzania itawakilishwa na Michezo sita ikiwemo Mchezo wa Ngumi za
Ridhaa yenye wachezaji watatu, Timu ya Mpira wa Miguu ya Wanawake (Twiga Stars)
yenye wachezaji 18, na Timu ya Riadha yenye wachezaji wanne.
Nyingine ni
Timu ya kuogelea yenye wachezaji wawili, wachezaji wawili wa Judo pamoja na
Michezo kwa watu wenye Ulemavu yenye wachezaji wawili.
Naye Mkurugenzi
Msaidizi Maendeleo ya Michezo Bibi. Juliana Yassoda amesema kuwa Timu ya Taifa
ya Tanzania ilikua iondoke kwenda Congo Brazaville leo lakini kutokana na ugumu
wa upatikanaji wa nafasi katika ndege mbalimbali timu hiyo imelazimika kuondoka
kesho na usafiri maalum.



No comments:
Post a Comment