Rais Jakaya Kikwete, akizungumza na Balozi Mteule wa Uswiss nchini, Florence Mattli, wakati alipofika Ikulu, kujitambulisha, Dar es Salaam leo.
Balozi mpya wa Finland nchini Bw. Pekka Hukka akisanini kitabu cha wageni alipowasili Ikulu jijini Dar es Salaam kuwasilisha hati za utambulisho kwa Rais Jakaya Mrisho Kikwete leo Septemba 9, 2015.
Balozi mpya wa Finland nchini Bw. Pekka Hukka akisoma salamu kabla ya kumkabidhi hati za utambulisho kwa Rais Jakaya Mrisho Kikwete Ikulu jijini Dar es Salaam leo Septemba 9, 2015.
Balozi mpya wa Finland nchini Bw. Pekka Hukka akiwasilisha hati za utambulisho kwa Rais Jakaya Mrisho Kikwete Ikulu jijini Dar es Salaam leo Septemba 9, 2015.
Balozi mpya wa Finland nchini Bw. Pekka Hukka baada ya kuwasilisha hati za utambulisho akiongea na Rais Jakaya Mrisho Kikwete Ikulu jijini Dar es Salaam leo Septemba 9, 2015.
Balozi mpya wa Finland nchini Bw. Pekka Hukka akipigiwa nyimbo za taifa baada ya kuwasilisha hati za utambulisho kwa Rais Jakaya Mrisho Kikwete Ikulu jijini Dar es Salaam leo Septemba 9, 2015.
Balozi mpya wa Sweden Bi. Katrina Rangnitt nchini akiweka saini kitabu cha wageni kabla ya kuwasilisha hati za utambulisho kwa Rais Jakaya Mrisho Kikwete Ikulu jijini Dar es Salaam leo Septemba 9, 2015.
Balozi mpya wa Sweden nchini Bi. Katrina Ranngitt akiwasilisha hati za utambulisho kwa Rais Jakaya Mrisho Kikwete Ikulu jijini Dar es Salaam leo Septemba 9, 2015.
Balozi mpya wa Sweden nchini Bi. Katrina Ranngitt akisalimiana na Naibu Waziri wa mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa baada ya kuwasilisha hati za utambulisho kwa Rais Jakaya Mrisho Kikwete Ikulu jijini Dar es Salaam leo Septemba 9, 2015.
Balozi mpya wa Sweden nchini Bi. Katrina Ranngitt akiwa katika mazungumzo na Rais Jakaya Mrisho Kikwete Ikulu jijini Dar es Salaam leo Septemba 9, 2015.
Balozi mpya wa Sweden nchini Bi. Katrina Ranngitt akisindikizwa na Mnikulu wa Ikulu Bw. Jumaa Bwambo baada ya kuwasilisha hati za utambulisho kwa Rais Jakay Mrisho Kikwete Ikulu jijini Dar es Salaam leo Septemba 9, 2015.
Na Beatrice Lyimo-Maelezo
9/9/2015
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete amepokea hati za utambulisho wa mabalozi wanne kutoka nchi nne kwa nyakati tofauti, ambao wanaziwakilisha nchi zao hapa nchini.
Halfa hiyo ilifanyika leo Ikulu jijini Dar es salaam ambapo Rais Kikwete alimpokea mhe. Balozi Florence Tinguely kutoka Uswis, ambaye alikuwa wa kwanza kuwasili, wa pili kuwasili ni mhe. Balozi Yasemin Fraip kutoka Uturuki, na watatu ni mhe. Balozi Pekka Hukka anayeiwakilisha Finland pamoja na Katarina Rangnitt anayeiwakilisha Sweden.
Mabalozi hao waliwasili Ikulu kwa nyakati tofauti, ambapo wa kwanza aliwasili kuanzia majira ya saa 5:00 asubuhi na hafla hiyo ilimalizika majira ya saa 7:00 mchana.
Katika hatua nyingine, Rais Kikwete amemkabidhi Bwana. Haroub Soud Mzee ambaye ni mlemavu wa miguu bajaji itakayomsaidia katika shughuli zake mbalimbali za kimasomo.
Mzee ambaye ni mwanafunzi wa mwaka wa tatu katika Chuo Kikuu cha Kampala nchini kutoka fani ya uhasibu amekabidhiwa bajaji hiyo yenye namba za usajili MC 835 AVU.
Mzee amemshukuru Rais Kikwete kwa usikivu wake na kujali kusikiliza na kufanikisha ombi lake lililochukua muda wa miezi mitatu tangu alipowasilisha.
Kwa upande wake Mwandishi Msaidizi wa Rais Bi. Premi Kibanga amesema kuwa Rais anapokea maombi mbalimbali ya vitu tofauti kutoka kwa wananchi na kujitahidi kufanikisha na kutatua shida zinazowakabili.












No comments:
Post a Comment