Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete akifungua mkutano wa siku mbili wa Takwimu Huria Kanda ya Afrika unaofanyika nchini katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere leo jijini Dar es Salaam. Katikati ni Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue na Mwakilishi wa Benki ya Dunia nchini Bella Bird (wa kwanza kulia).
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete akifungua mkutano wa siku mbili wa Takwimu Huria Kanda ya Afrika unaofanyika nchini katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere leo jijini Dar es Salaam. Katikati ni Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue na Mwakilishi wa Benki ya Dunia nchini Bella Bird (wa kwanza kulia).
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mathias Chikawe akimkaribisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete (hayupo pichani) kufungua mkutano wa siku mbili wa Takwimu Huria Kanda ya Afrika unaofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere leo jijini Dar es Salaam.
Mwakilishi wa Benki ya
Dunia nchini Bella Bird akiongea wakati wa ufunguzi wa mkutano wa siku mbili wa
Mfumo wa Takwimu Huria Kanda ya Afrika utakavyoleta maendeleo katika nchi za
Afrika leo jijini Dar es Salaam.
Mwakilishi wa Benki ya
Dunia nchini Bella Bird akiongea wakati wa ufunguzi wa mkutano wa siku mbili wa
Mfumo wa Takwimu Huria Kanda ya Afrika utakavyoleta maendeleo katika nchi za
Afrika leo jijini Dar es Salaam. Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue akitoa neno la shukrani mara baada ya ufunguzi wa mkutano wa siku mbili wa Mfumo wa Takwimu Huria Kanda ya Afrika leo jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete (kulia) akibadilishana mawazo na Mwakilishi wa Benki ya Dunia nchini Bella Bird (kushoto) mara baada ya ufunguzi wa mkutano wa siku mbili wa Mfumo wa Takwimu Huria Kanda ya Afrika leo jijini Dar es Salaam.
Mwanzilishi na Mkurgenzi Mtendaji wa Kampuni ya Bongo Live masuala ya ujumbe mfupi wa simu na mifumo ya simu Taha Jiwaji (kushoto) akifafanua kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete (kulia) namna kampuni yake inavyofanya kazi mara baada ya ufunguzi wa mkutano wa siku mbili wa Mfumo wa Takwimu Huria Kanda ya Afrika leo jijini Dar es Salaam.
Angelina Misso (katikati) akimwelea jambo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete (kulia) namna Chuo Kikuu cha Dar es salaam Kitengo cha Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (CoICT) kinavyofanya kazi na sekta mbalimbali katika matumizi sahihi ya takwimu huria mara baada ya ufunguzi wa mkutano wa siku mbili unaohusu Mfumo wa Takwimu Huria Kanda ya Afrika leo jijini Dar es Salaam. Wa kwanza kushoto ni Biasha Mkenga kutoka Kitengo cha Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (CoICT), Chuo Kikuu cha Dar es salaam.
Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu Dkt. Albina Chuwa (wa kwanza mstari wa mbele kushoto) akifuatilia hotuba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete (hayupo pichani) alipokuwa akifungua mkutano wa siku mbili wa Takwimu Huria Kanda ya Afrika unaofanyika nchini katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere leo jijini Dar es Salaam.
Baadhi wa Makatibu Wakuu na Manibu Katibu Wakuu kutoka Wizara mbalimbali wakifuatilia wakifuatilia hotuba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete (hayupo pichani) alipokuwa akifungua mkutano wa siku mbili wa Takwimu Huria Kanda ya Afrika unaofanyika nchini katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere leo jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete (katikati) akiongea na baadhi ya waandishi wa habari mara baada ya ufunguzi wa mkutano wa siku mbili wa Mfumo wa Takwimu Huria Kanda ya Afrika leo jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu Dkt. Albina Chuwa akiongea na baadhi ya waandishi wa habari mara baada ya ufunguzi wa mkutano wa siku mbili wa Mfumo wa Takwimu Huria Kanda ya Afrika leo jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete (katikati mstari wa mbele walioketi) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Makatibu Wakuu na Manaibu Katibu Wakuu kutoka Wizara mbalimbali mara baada ya ufunguzi wa mkutano wa siku mbili wa Mfumo wa Takwimu Huria Kanda ya Afrika leo jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete (katikati mstari wa mbele walioketi)
akiwa katika picha ya pamoja na kamati ya maandalizi ya mkutano huo mara baada
ya ufunguzi wa mkutano wa siku mbili wa Mfumo wa Takwimu Huria Kanda ya Afrika
leo jijini Dar es Salaam.
(Picha zote na Eleuteri
Mangi-MAELEZO)
Na Beatrice Lyimo-
Maelezo
4/9/2015
RAIS wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete amawaasa Asasi za kiraia na Taasisi
binafsi kuwa wazi katika masuala yao katika shughulizao kwa wananchi ili kuleta
maendeleo nchini.
Rais Kiwete amesema
hayo wakati akifungua mkutano wa siku mbili wa Takwimu Huria Kanda ya Afrika unaofanyika
katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere leo jijini Dar es
Salaam.
Rais Kiwete amesema
kuwa mkutano wa Takwimu Huria Kanda ya Afrika ni wa kwanza na wa aina yake kufanyika Barani Afrika na Tanzania imepewa
heshima ya kuwa mwenyeji ambapo imeshirikiana na Benki ya Dunia katika kuandaa mkutano
huo.
Dkt. Kikwete ameongeza
kuwa heshima hiyo imetokana na Tanzania kujiunga na Mpango wa Uendeshaji wa
Shughuli za Serikali kwa Uwazi (OGP) unaolenga kuifanya Serikali kuwa wazi na
hivyo kuleta uadilifu na uwajibikaji katika kuwahudumia Wananchi.
“Katika utekelezaji wa
Mpango wa OGP, Tanzania iliweka kipaumbele katika kuanzisha Tovuti ya Takwimu
Huria itakayoweka wazi takwimu mbalimbali za Serikali na Taasisi zake”
amefafanua Rais Kikwete.
Naye
Mwakilishi wa Benki ya Dunia nchini Bella Bird amesema kuwa lengo la mkutano
huo ni kujadiliana kuhusu mfumo wa Takwimu Huria na jinsi utakavyoleta
maendeleo hususani kwa nchi za Afrika ikiwemo mwenyeji Tanzania.
Kwa upande wake Katibu
Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue amesema kuwa Takwimu huria itawasaidia
wananchi kujua nini kinaendelea katika sekta mbalimbali ikiwemo sekta ya maji,
elimu na afya ambazo ndio sekta zinazogusa jamii kwa ukaribu na kupelekea
kuanza na sekta hizo.
Pia ameongeza kuwa sera
ya Takwimu huria ipo kwenye matayarisho na inategemewa kuanza kutumika baada ya
miezi sita ijayo na hivyo kumfanya mwanachi kuweza kuingia kwenye mtandao na
kujua matatizo yanayoikabili jamii.
Halikadhalika Mkurugenzi
Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu Dkt. Albina Chuwa akiongea na waandishi wa
habari mara baada ya ufunguzi wea mkutano huo amesisitiza kuwa nchi za Afrika zitumie
takwimu huria kwa ajili ya kuleta maendeleo katika nchi zao kwani zinasaidia
kupata fursa mbalimbali ikiwemo upatikanaji wa ajira na pia kumfanya mwananchi
kufanya uchambuzi wa kutosha kwa kufuata viwango na kujua hali halisi juu ya
mambo mbalimbali yanayoendelea katika nchi taifa yao.
Mkutano
huo unaoendelea jijini Dar es salaam unajumuisha takribani nchi 30 kutoka ndani
na nje ya Afrika kwa kushirikisha wawakilishi mbalimbali kuwakilisha Serikali
zao, Asasi za Kiraia, Sekta Binafsi,
Taasisi za Elimu ya Juu pamoja na Washirika mbalimbali wa Maendeleo.

















No comments:
Post a Comment