Amiri Jeshi Mkuu Dkt.Jakaya Mrisho akiwa katika gari maalum la wazi na Mkuu wa Chuo cha maafisa wa Jeshi(TMA) Monduli akiingia katika uwanja wa paredi tayari kwa kutunuku kamisheni kwa maafisa wapya wa jeshi leo. (Picha zote na Freddy Maro)
Mkuu wa Majeshi Jenerali Davis Adolf Mwamunyange akimkaribisha Amiri Jeshi mkuu Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete katika chuo cha jeshi Monduli (TMA) ili kutukunu kamisheni kwa maafisa wapya leo.
Maofisa wapya wa Jeshi wakila kiapo mbele ya Amiri jeshi Mkuu Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete.
Mkuu wa Majeshi Jenerali Davis Adolf Mwamunyange akimkabidhi moja ya zawadi Amiri Jeshi mkuu Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete katika chuo cha jeshi Monduli(TMA) ili kutukunu kamisheni kwa maafisa wapya leo.
Amiri Jeshi Mkuu Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akitunuku Kamisheni kwa Maafisa wapya wa Jeshi katika Cho cha Jeshi(TMA) Monduli Mkoani Arusha leo.
Mkuu wa Majeshi Jenerali Davis Mwamunyange akimkabidhi Amiri Jeshi Mkuu Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete zawadi ya picha akiwa katika gari la wazi katika sherehe za awali chuoni hapo, na kitara pamoja na nembo maalum ya jeshi kwa kutambua mchango wake katika kuliboresha na kulifanya la kisasa Jeshi la Wananachi wa Tanzania wakati wa Sherehe za kutunuku l\kamisheni kwa maafisa wapya wa jeshi katika chuo cha jeshi Monduli leo.
Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiangalia michoro ya majengo ya chuo hicho.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiiangalia picha ya kuchora ya Mkewe Mama Salma Kikwete aliyoipokea kwa niaba yake.
Amiri Jeshi Mkuu Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akikagua gwaride muda mfupi kabla ya kutunuku Kamisheni kwa Maofisa wapya wa Jeshi katika Chuo cha Jeshi Monduli leo.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimpa zawadi Afisa mwanafunzi bora Luteni Usu Antony Shija wakati wa sherehe za kutunuku kamisheni kwa maafisa wapya leo katika chu cha jeshi TMA Monduli leo.
Amiri Jeshi Mkuu Rasi Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akitoa akimpa zawadi afisa mwanafunzi bora wa kike Luteni Usu Martina James Shija wakati wa sherehe za kutunuku kamisheni kwa maafisa wapya wa jeshi katika chuo hca jeshi Monduli leo.
Na Richard Mwangulube na Wankyo Gati, TMA, Monduli
RAIS Jakaya Mrisho Kikwete na Amri Jeshi Mkuu leo ametunuku Kamisheni ya lutein Usu kwa Maofisa Wanafunzi 166 wa Kozi ndefu katika Chuo cha Mafunzo cha Kijeshi TMA Monduli
Kati ya wahitimu hao pia wamo maofisa wanawake 21 ikiwa ni kozi ya 56 iliyoanza mwaka 2014
Tangu aingie madarakani mwaka 2005 Rais Kikwete na Amiri Jeshi Mku ameweza kutunuku Kamisheni Makundi 18 ambapo maofisa wanafunzi 3,000 wakiwemo wanawake 132 wamehitimu mafunzo katika chuo hicho.
Mbali na kutunuku Kamisheni kwa maofisa wanafunzi hao Rais Kikwete pia ametoa zawadi kwa maofisa wanafunzi wanne waliofanya vizuri wakati wa mafunzo hayo.
Maofisa wanafunzi waliotunukiwa zawadi na Amri Jeshi Mkuu ni Anton Shija alipata zawadi kwa kuwa mshindi wa Jumla wakati wa Kozi hiyo, Sharma Aman Mbegu aliyepata zawadi kwa kuwa mshindi katika masuala ya taaluma.
Aidha Rais Kikwete pia ametoa zawadi kwa afisa mwanafunzi Nuru Joseph Mhama ambaye ni mshindi katika masuala ya medani za kivita na upande wa wanawake Amiri Jeshi Mkuu ametoa zawadi kwa afisa mwanafunzi Amartina James Simba
Rais Kikwete ambaye ni Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama awali alikagua gwaride la wahitimu hao lililoundwa na Gadi nne ambapo wahitimu hao pia walikula kiapo cha utii kwa Rais na Amiri Jeshi Mkuu baada ya kupitia mbele ya Rais kwa mwendo wa pole na wa haraka.
Hii ni sherehe yake ya mwisho kabla kipindi cha Urais Kumalizika Oktoba mwaka huu ambapo mwaka 1992 Rais Kikwete aliwahi kuwa Kamisaa katika Chuo hicho cha TMA.
Sherehe hizo pia zimehudhuriwa na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama Jenerali Davis Adolf Mwamunyange, Mnadhimu Mkuu Luteni Jenerali Samwel Ndomba, Waziri wa Ulinzi Dkt Hussein Ali Mwinyi. NA Aliyewahi kuwa Mkuu wa Majeshi Mirisho Sarakikya Sherehe hizo pia zimehudhuriwa na Waziri Mkuu Mizengo Kayanza Pinda.
Aidha Sherehe hizo Pia zimehudhuriwa na Wakuu wa Vyuo vya Kijeshi kutoka nchi za Afrika ya Mashariki (EAC) za Uganda, Kenya, Rwanda na Burundi na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue.
Wakati wa Sherehe hizo uongozi wa chuo ulimtunuku zawadi mbalimbali kwa kutambua mchango wake kwa chuo hicho yeye na mama Salma Kikwete ambapo mkozi hiyo imehusisha maofisa wanafunzi wote kutoka Tanzania.

No comments:
Post a Comment