TANGAZO


Thursday, September 3, 2015

Mtoto Happy Limwamwa (9) aomba kurejeshwa nyumbani kwao Mbinga

Happy Limwamwa (9-10), Binti aliyechukuliwa na mama mkazi wa Njombe, kwa ajili ya kufanyakazi za ndani, anaomba msaada wa kurejeshwa nyumbani kwao Mbinga baada ya kutoroka kwa mama huyo kwa kile alichokieleza kuwa ni kipigo alichokuwa akikipata kutoka kwa mama huyo pamoja na mume wake hadi kulazimika kutoroka na kuwa mtoto wa mitaani pasi na kujua pa kuelekea kwa ajili ya kurejea nyumbani kwao Mbinga......maelezo zaidi ya binti Happy yanafuata chini...
Happy Limwamwa 9-10 (kushoto) akizungumza kwa uchungu kwa Msaidizi wa Kisheria Geophrey Kaduma, (wapili kulia)  manyanyaso aliyokuwa akiyapata kutoka kwa mama aliyekuwa amemchukua nyumbani kwao alikozaliwa Wilaya ya Mbinga, Mkoa wa Ruvuma, kwa malengo la kufanya kazi za ndani.

Binti Happy, akiwa kwa mama huyo, aliyekuwa akimfanyia kazi za ndani, alisema kuwa alikuwa akipata kichapo toka kwa mama huyo pamoja na mume wa mama huyo hadi akalazimika kuwakimbia na kuishi mitaani hadi kuokotwa na Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Bryceson Mgaya wa Mtaa wa Kambarage, Kata ya Njombe Mjini, wilayani Njombe.

Mwenyekiti huyo baada ya kumchukua binti huyo, alitoa taarifa katika Kituo cha Polisi na pia kumtembeza katika mitaa tofauti ikiwemo mtaa wenye nyumba aliyokuwa akifanya kazi za ndani zaidi ya wiki 3, lakini juhudi hizo hazikuweza kuasidia mtoto huyo kupata msaada wa kurudishwa kwao, Mbinga.

Kwa ajili ya kumsaidia Happy kurudi nyumbani kwao Mbinga unaombwa kuwasiliana kwa kupitia Mwenyekiti huyo wa mtaa, kwa namba ya simu 0766336403, ama Mwenyekiti wa Kituo cha Sheria, Geophrey Kaduma simu namba 0759601915 na 0655601915, Njombe. 

Pichani, wapili kushoto ni Katibu wa Kituo cha Msaidizi wa Kisheria Magy Mtalla na wa kwanza kulia ni mke wa mwenyekiti huyo wa mtaa wa Kambarage, Matha Maiseli (Maelezo na Picha: Na Khamisi Mussa)

Katibu wa Kituo cha Msaidizi wa Kisheria Magy Mtalla, akizungumza na mtoto, Happy  Limwamwa.
Happy  Limwamwa 9-10, akipozi kwa picha

No comments:

Post a Comment