Rais wa tume ya Ulaya Jean Claude Juncker, ametoa wito kwa watu barani ulaya kujitolea na kuonyesha utu na usawa kwa wakimbizi wanaoingia barani ulaya.
Junker amesema kwa licha ya muungano wa ulaya kutokuwa katika hali nzuri kiuchumi, ulaya inaonekana kama eneo salama na la matumaini kwa watu wengi kutoka
AP
mashariki ya kati.
Akilihutubia bunge la ulaya bwana Junker alizitaka nchi za muungano wa ulaya kuwapa makao wakimbizi 160,000 wanaogawana kama sehemu ya mpango wa lazima baina ya nchi za ulaya.
Getty
Mapema mpango huo ulioonekana kuwa bora ulipingwa vikali na baadhi ya nchi za muungano huyo.
Sasa mpango mwingine utajadiliwa kwenye mkutano wa mawaziri wa nchi za muungano wa ulaya siku ya Jumatatu.


No comments:
Post a Comment