Umati wa wananchi waliojitokeza kwenye kampeni za kumnadi Mgombea ubunge wa Jimbo la Lindi Mjini wakishuhudia hotuba mbalimbali zilizokuwa zikitolewa na viongozi wa Chama Cha Mapinduzi kwenye Kata ya Msinjahili jana tarehe 4.9.2015.
Mke wa Rais na Mjumbe wa NEC Taifa ya CCM, Mama Salma Kikwete akiwa ameshika bango la mgombea Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi Ndugu John Pombe Magufuli wakati alipokuwa akimnadi kwa wananchi wa Lindi Mjini. Aliyeshika bango hilo kushoto ni Mgombea ubunge katika Jimbo la Lindi Mjini Ndugu Hassan Kaunje na katikati ni mgombea udiwani wa kata ya Msinjahili Mama Asina Kawamba.
Mke wa Rais na MNEC Taifa anayewakilisha Lindi Mjini Mama Salma Kikwete akizungumza na wananchi wa Lindi Mjini (hawapo pichani) wakati akimnadi Ndugu Hassan Kaunje anayegombea ubunge katika jimbo hilo pamoja na madiwani kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) jana tarehe 4.9.2015. (Picha zote na John Lukuwi)

No comments:
Post a Comment