TANGAZO


Wednesday, September 9, 2015

Makamu wa Rais Zanzibar, Balozi Seif Idd atembelea Uwanja wa Gombani Pemba kuangalia maendeleo ya uwekaji wa tatani

Ofisa Mdhamini Wizara ya Habari, Utamaduni, Utalii na Michezo Pemba Nd. Ali Nassor Mohammed akimuonesha Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi moja ya sampuli ya vipande vya Tatani inayotarajiwa kutandikwa katika uwanja wa Michezo wa Gombani Chake chake Pemba. Kulia ya Nd. Ali ni Mkuu wa Wilaya ya Chake chake Pemba Bibi Hanun Ibrahim Masoud.
Ndugu Ali akimpatia maelezo Balozi Seif juu ya  vipolo vya chenga chenga za Mipira  zitakazokujapikwa  kwa ajili ya utandikaji wa Tatani katika Uwanja wa Gombani. 
Balozi Seif akionyesha furaha yake kutokana na kukamilika kwa vifaa  kwa ajili ya utandikaji wa Tatani katika uwanja wa michezo wa Gombani Chake chake Pemba. Kushoto ya Balozi Seif ni Afisa Mdhamini Wizara ya Habari, Utamaduni, Utalii na Michezo Pemba Ndugu Ali Masoud Mohammed. 
Balozi Seif wa pili kutoka Kushoto akiangalia moja ya Kigari kitakachotumika katika kazi ya utandikaji wa Tatani katika Uwanja wa Gombani Chake chake Pemba. (Picha zote na – OMPR – ZNZ)

No comments:

Post a Comment