Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Dk. Donan Mmbando akibonyeza kitufe cha kompyuta ili kuzindua mfumo wa utunzaji wa taarifa za vituo vya afya vya Tanzania Bara jijini Dar es Salaam leo.
Baadhi ya wadau
wakiwa katika uzinduzio huo.
Beatrice Lyimo- MAELEZO
SERIKALI kupitia Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii imezindua mfumo wa utunzaji wa taarifa za vituo vya afya vya Tanzania Bara.
Akizindua mfumo huo leo jijini Dar es salaam Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Dkt. Donan Mmbando amesema kuwa katika kutekeleza mkakati wa kielekroniki katika sekta ya afya (e-Health) wizara imetengeneza mfumo huo ili kuhifadhi taarifa za vituo vya afya vya huduma za afya za serikali na binafsi.
Dkt Mmbando ameongeza mfumo huo utasaidia watumiaji kupata taarifa za vituo sahihi na kwa wakati pia utakuwa chanzo cha taarifa za vituo vya huduma za afya kwa mifumo mingine na utafiti kwa ujumla.
“Mfumo huu unahifadhi taarifa muhimu na huduma zinazotolewa na vituo vyote vya huduma za afya vilivyopo Tanzania bara, taarifa hizo ni kama kujua jina la kituo taarifa za kijiografia, mahali kituo kinapatikana na huanzia kwa ngazi ya kanda mpaka kijiji, aina, umiliki, hali ya utendaji kazi na huduma zote zinazotolewa na vituo”alifafanua Dkt. Mmbando.
Aliongeza kwa huu utawezesha watumiaji kujua idadi ya vituo kutokanan na mahali vilipo, aina na umiliki wa vituo. Pamoja na hayo watumiaji wote wataweza kupata taarifa za upatikanaji wa huduma za afya zilizopo karibu hao.
Dkt. Mmbando alisema mfumo huo ujnatengeneza namba maalum kwa kila kituo kitakachoingizwa namba hiyo haijirudii wala haitabadilika kama kituo kitafungwa.
“Tunawahimiza wadau watumie mfumo huu katika kufanya mipango na usimamizi wa kazi mbalimbali. Pia tunasisitiza mfumo huu utumike kama chanzo pekee cha taarifa za vituo na mwisho mfumo huu utumiwe na wananchi wote kupata huduma za afya zilizopo karibu nao,” alisisitiza.
Kwa upande wake Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano, ICT Hermas Rulagirwa alisema tayari watumishi wa sekta ya afya wamepwa mafunzo juu ya mvfumo huo hadi wale kwenye ngazi za halmashauri.
Alisema watumishi wa afya wa Serikali ndio waliopewa mamlaka wa kuingiza taarifa mpya.
Aliomba ushirikiano kutoka kwa sekta binafsi wa kupata taarifa mara kwa mara ili kuweza kuboresha mfumo huo.

No comments:
Post a Comment