Umoja wa Mataifa unasema mafanikio makubwa yamepatikana katika kupunguza vifo vya watoto wadogo.
Ripoti ya shirika la afya duniani na shirika linaloshughulikia maswala ya watoto la Umoja wa Mataifa Unicef linasema idadi ya vifo vya watoto wadogo vimepungua kwa zaidi ya nusu katika kipindi cha miaka ishirini na mitano iliyopita.

Mwaka huu idadi hiyo imeonekana kupungua kwa kiwango cha milioni sita kwa mara ya kwanza.
Lakini mashirika ya misaada yanasema bado kuna changa moto kubwa, hasa kwa nchi zenye kipato cha chini kusini mwa jangwa la sahara.


No comments:
Post a Comment