Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa, Balozi Seif Ali Idd, akizindua Maskani ya Chama hicho, ya Vijana wa Jimbo la Kiwani, Wilaya ya Mkoani, Mkoa wa Kusini Pemba iliyopewa jina lake leo.
Balozi Seif akipandisha Bendera ya Maskani ya CCM, ya Vijana wa Kiwani, iliyopewa jina la Balozi Seif Maskani mara baada ya kuizindua rasmi katika sherehe iliyofanyika jimboni humo leo.
Baadhi ya wanachama wa CCM na Wsananchi wa Kijiji cha Kiwani Michakweni wakifuatilia Hotuba ya Balozi Seif hayupo pichani wakati wa uzinduzi wa Maskani ya Jina wa Kijiji hicho iliyopewa jina lake.
Balozi Seif akisalimiana na Sheikh Faki Mohammed Khamis ambae ni mlemavu asiyeona baada ya kusoma Quran Tukufu wakati wa uzinduzi wa Balozi Seif Maskani hapo Kiwani Wilaya ya Mkoani.
Vijana Zuhura na Safi wakighani utenzi murua uliotoa burdani safi wakati wa hafla ya uzinduzi wa Balozi Seif Maskani ya Vijana wa CCM wa Kijiji cha Kiwani Michakweni.
Vijana wa Maskani ya CCM ya Balozi Seif iliyopo Kiwani wakitoa burdani ya nyimbo maalum iliyohanikiza katika uzinduzi wa Maskani yao waliyoamua kuipa jina la Balozi Seif Maskani.
Kaimu Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa CCM Shaka Hamdu Shaka, akiwakumbusha Vijana wa Kiwani Michakweni kuelewa wajibu wao wa kuhakikisha CCM inaendelea kushika dola kwa kuwapa ushindi wagombea wa chama hicho.
Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM Balozi Seif Ali Iddi akizungumza na wanachama wa CCM wa Jimbo la Kiwani mara baada ya kuizindua Balozi Seif Maskani ya Kijiji hicho.
Mwonekano wa jengo la Maskani ya Balozi Seif lililopo
Kiwani Kichakweni, lililojengwa kwa kuzingatia Utamaduni wa Visiwa vya Zanzibar. (Picha zote na Hassan Issa – OMR – ZNZ)
Na Othman Khamis Ame
Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar
14/9/2015.
MJUMBE wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Seif Ali Iddi amewaasa wanachama wa Vyama vya upinzani kisiwani Pemba kuacha kuendelea kukumbatia viongozi ambao tayari wameshaonesha mwelekeo wa kutokubali kusimamia maendeleo yao kwa zaidi ya miaka ishirini sasa.
Alitoa nasaha hizo wakati akizungumza na wanachama wa Chama cha Mapinduzi (CCM) na Wananchi wa Kijiji cha Kiwani – Michakweni Jimbo
la Kiwani mara baada ya kuizindua Rasmi Maskani ya Vijana wa CCM wa Jimbo hilo iliyopewa Jina lake.
Balozi Seif alisema wakati wa kuacha kudanganywa kwa sera na ahadi zisizotekelezeka za Viongozi hao wanaojali maslahi yao binafsi umefika kwa wafuasi hao wa Upinzani na badala yake wajiunge na Chama cha Mainduzi kabla hawajaachwa njia panda.
Alisema Gari la Chama cha Mapinduzi hivi sasa bado linaruhusu kupakiwa abiria wowote watakaoamua kutoka vyama vya upinzani ambao wanaonekana kuchoshwa na vitendo vinavyoviza Maendeleo yao kwa kiindi kirefu sasa.
Balozi Seif alielezea faraja yake kutokana na Wananchi walio wengi Kisiwani Pemba kuonyesha dalili za kuchoshwa na hatimae kukataa Viongozi wasiojali Maendeleo ya Wananchi.
Mjumbe huyo wa Kamati Kuu ya CCM Taifa alisema katika kuuzika upinzani katika Uchaguzi Mkuu ujao wa mfumo wa Vyama vingi vya Siasa aliwakumbusha wanaCCM waendelee kushikamana lengo likiwa ni kumaliza upinzani huo usio na muelekeo wa Maendeleo.
Amewapongeza Vijana hao wa Balozi Seif Maskani wa Kiwani Michakweni kwa uamuzi wao wa kujenga Jengo lililozingatia Utamaduni wao na kuwaahidi kusaidia kuiimarisha katika kiwango kinacholingana na Chama chenyewe.
Alisema msaada huo utakwenda sambamba na kuzingatia mipango imara ya kuwapatia Boti ya uvuvi itakayowapa fursa ya kujiajiri wenyewe ili waweze kukidhi mahitaji yao ya Kimaisha.
Balozi Seif alieleza kwamba tabia ya kukaa vijiweni hivi sasa imepitwa na wakati kulingana na mabadiliko ya mfumo wa Dunia uliopo hivi sasa ambao unamkaba mwanaadamu lazima afanye kazi.
Akitoa Taarifa fupi ya Vijana hao wa Balozi Seif Maskani Mmmoja wa Viongozi wa Maskani hiyo Ndugu Mohammed Juma alisema Maskani hiyo, imeasisiwa Mwaka 2014 ikianza na Wanachama 22 na hivi sasa imeongeza wanachama na kufikia 36.
Nd. Mohammed alisema kwamba Vijana hao wamejipanga kuwa Maskani ya chuo cha Vijana katika kuwafundisha sera za Chama cha Mapinduzi (CCM), pamoja na Itikadi zake zitakazosaidia Vijana hao kuelewa Historia ya Taifa hili lililojikomboa kutokana na madhila ya wakoloni.
Vijana hao wa Balozi Seif Maskani Kiwani Michakweni wameupongeza Uongozi wa Serikali ya Wilaya ya Mkoani kwa kuwahakikishia usalama licha ya vitisho wanavyoendelea kufanyiwa na wafuasi wa Upinzani kwa uamuzi wao wa kuunga mkono Chama cha Mapinduzi.
Naye akisalimia na Vijana hao wa Balozi Seif Maskani ya Kiwanchi Michakweni Mke wa Mjumbe huyo wa Kamati Kuu ya CCM Taifa Mama Asha Suleiman Iddi amewataka akina Mama wa Kijiji na Jimbo hilo kuhakikisha kwamba Viongozi watakaowachaguwa wawe tayari kufanya nao kazi pamoja.
Mama Asha alisema wapo viongozi wenye tabia ya kwenda Majimboni kuomba kura na baadaye kuwatelekeza Wananchi hao bila ya kujali kwa
vitendo vyao vya kutafuta maslahi katika maeneo mengine vinawanyima haki Wananchi wao.










No comments:
Post a Comment