TANGAZO


Saturday, September 5, 2015

Baba wa mtoto aliyekufa akataa hifadhi


Image copyrightReuters
Image captionBaba wa mtoto aliyekufa akataa hifadhi

Baba wa mtoto kutoka nchini Syria ambaye alikufa maji wiki hii na kuzua changamoto za kutaka kuchukuliwa hatua za kutatua suala la uhamiaji nchini syria anaripotiwa kukataa hatua ya Canada ya kumpa makao.
Tima Kurd, ambaye ni dadake Abdullah al Kurdi alisema, alimuambia kuwa anataka kusalia nchini Syria yaliko makaburi ya mkewe na wanawe wawili wa kiume ambao pia walikufa maji nje ya pwani ya Uturuki siku ya jumatano.

Image copyrightReuters
Image captionBaba na watoto wake waliokufa maji

Wote hao walizikwa nchini Syria siku ya Ijumaa
Picha za mwili wa mtoto huyo wa miaka mitatu katika ufuo wa Uturuki zilizua mjadala kuhusu hatma ya watu wanaokimbia mapigano nchini Syria.

No comments:

Post a Comment