Ofisa Uhusiano wa Shirika la Misaada ya Maendeleo la Japan (Jaica), nchini Tanzania, Raymond Msofe akizungumza, Dar es Salaam leo, wakati Walimu wa Kujitolea kutoka Japan, nchini Tanzania walipokutana na kuzungumza na waandishi wa habari, kuelezea kuhusu ziara yao nchini, iliyoanza Agosti 10 na kumalizika leo, Agost 19. Walimu hao walitembelea Shule na miradi mbalimbali, inayofadhiliwa na shirika hilo. Kushoto ni Mwalimu Kenichi Onuki wa Shule ya Sekondari Koryo, Ryutaro
Kudo wa Shule ya Kachida ya Yokohama na Takanori Koganei wa Yokohama Seiryo Sogo High School.(Picha zote na Kassim Mbarouk-www.bayana.blogspot.com)
Ofisa Mipango Mkuu wa Jaica Tanzania, Adachi Famiko, akizungumza wakati wa mkutano huo.
Baadhi ya walimu hao wa kujitolea kutoka Japan, walipokuwa wakizungumza na waandishi wa habari kuhusu ziara yao nchini Tanzania jijini leo.
Baadhi ya walimu wa kujitolea kutoka Japan, waliokuja nchini Tanzania, wakiwa katika mkutano huo na waandishi wa habari jijini leo.
Baadhi ya walimu wa kujitolea kutoka Japan, waliokuja nchini Tanzania, wakisikiliza maelezo yaliyokuwa yakitolewa na mmoja wa walimu huo.
Baadhi ya walimu wa kujitolea kutoka Japan, waliokuja nchini Tanzania, wakisikiliza maelezo yaliyokuwa yakitolewa na mmoja wa walimu huo.
Mwalimu Kenichi Onuki wa Shule ya Sekondari Koryo, akizungumza katika mkutano huo. Kushoto ni Ofisa Mwakilishi Mkuu wa Jaica nchini, Toshio Nagase na kulia ni Mwalimu Ryutaro Kudo wa Shule ya Kachida ya Yokohama nchini humo.
Mwalimu Ryutaro Kudo, akizungumza wakati wa mkutano huo.
Mwalimu Kenichi Onuki wa Shule ya Sekondari Koryo, akifafanua jambo katika mkutano huo.
Mwalimu Takanori Koganei akijibu moja ya maswali ya waandishi wa habari katika mkutano huo, alipokuwa akielezea kuhusu safari yao ya kikazi, kujifunza, kubadilishana uzoefu katika ufundishaji pamoja na kukuza uhusiano na walimu wa Tanzania kwenye shule na miradi mbalimbali waliyotembelea,
inayofadhiliwa na Shirika la Misaada ya Maendeleo la Japan (Jaica), Dar es Salaam leo.
Ofisa Utawala Msaidizi wa Jaica nchini, Nasib Hamis, akizungumza wakati wa mkutano huo, akielezea jinsi walimu hao, walivyoridhishwa na safari yao hiyo, walipotembelea miradi na shule zinazofadhiliwa na shirika hilo nchini.
Ofisa Mwakilishi Mkuu wa Jaica nchini, Toshio Nagase akizungumza katika mkutano huo. Wengine ni baadhi ya walimu hao.
Ofisa Mwakilishi Mkuu wa Jaica nchini, Toshio Nagase akifafanua jambo, wakati alipokuwa akijibu maswali ya waandishi wa habari katika mkutano huo,jijini leo.

No comments:
Post a Comment