TANGAZO


Saturday, August 1, 2015

Mwanahabari Ahadi Kakore wa CCM ajiondoa kuomba kugombea Ubunge Jimbo la Same Magharibi

Mwanahabari Ahadi Kakore

KWANZA nimshukuru Mungu kwa kunipa afya njema tangu mwanzo wakati naanza mchakato wa kuomba ridhaa ya Chama changu Chama Cha Mapinduzi (CCM) hadi tarehe ya leo.

Pili niishukuru CCM kwa kuniamini tangu nilipojiunga hadi kufikia hatua ya kuomba ridhaa ya kupata nafasi ya Ubunge wa Jimbo la Same Magharibi,  mchakato ambao umefikia ukingoni Jumapili Agosti 8 mwaka 2015.

Pamoja na shukrani hizo lakini nipende kueleza umma hasa wana Same Magharibi kuwa nimeamua kujitoa kwenye mbio za Ubunge  kutokana kuombwa na Wazee wa Jimbo la Same Magharibi ili niweze kuongeza nguvu kwa Ndugu John Chagama.

Nia ya kuniomba kufanya hivyo ni kuhakikisha Ndugu Chagama anapata kura za kutosha ili kuhakikisha jimbo letu linabakia mikoni mwa CCM hata baada ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba mwaka huu.

Jimbo la Same Magharibi  bado ni miongoni mwa majimbo ambayo maendeleo yake yapo chini hivyo nina imani kwamba nikishirikiana na Chagama maendeleo yatapatikana kwa faifa ya wote.

Mwisho ni kwamba napenda kuwashukuru wote waliojitolea kwa hali na mali ili kufanikisha dhamira yangu hii, wapo waliotoa mali muda na kila aina ya msaada ili kufikia malengo niliyokuwa nimejiwekea, bila kusahau vyombo vya habari mbalimbali ikiwemo website, blogs, magazeti redio na runinga asante sana.

Ahadi Kakore ( CCM kadi Namba AF 5846080)
Namba ya simu ni 0784 890 387  kwa atakayehitaji ufafanuzi zaidi.
Agosti 1, 2015.

No comments:

Post a Comment