Kaimu Postamasta Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania (TPC), Fortunatus Kapinga, akizungumza na waandishi wa habari, alipokuwa akielezea kuhusu mafanikio ya shirika hilo kwa miaka 10 (2005 hadi 2015), Dar es Salaam juzi. Kushoto ni Kaimu Meneja Mkuu Rasilimali za shirika, Nehemiah Kyabalasi.
Kaimu Postamasta Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania (TPC), Fortunatus Kapinga, akizungumza na waandishi wa habari, alipokuwa akielezea kuhusu mafanikio ya shirika hilo kwa miaka 10 (2005 hadi 2015), Dar es Salaam juzi. Kulia ni Kaimu Meneja Mkuu Uendeshaji wa Huduma za shirika, John Tinga.
Baadhi ya Maofisa na Wakurugenzi wa Shirika la Posta Tanzania (TPC), wakiwa katika mkutano huo na waandishi wa habari, Dar es Salaam juzi.
Baadhi ya Maofisa na Wakurugenzi wa Shirika la Posta Tanzania (TPC), wakinakili masuala mbalimbali wakati wa mkutano huo na waandishi wa habari.
Kaimu Postamasta Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania (TPC), Fortunatus Kapinga, akizungumza na waandishi wa habari, alipokuwa akielezea kuhusu mafanikio ya shirika hilo kwa miaka 10 (2005 hadi 2015), Dar es Salaam juzi.
Kaimu Postamasta Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania (TPC), Fortunatus Kapinga, akizungumza na waandishi wa habari, alipokuwa akielezea kuhusu mafanikio ya shirika hilo kwa miaka 10 (2005 hadi 2015), Dar es Salaam juzi. Kushoto ni Kaimu Meneja Mkuu Rasilimali za shirika, Nehemiah Kyabalasi na kulia ni Kaimu Meneja Mkuu Uendeshaji wa Huduma za shirika, John Tinga.
Baadhi ya waandishi wa habari wakiwa katika mkutano huo na Kaimu Postamasta Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania (TPC), Fortunatus Kapinga, wakati alipokuwa akizungumzia kuhusu mafanikio ya shirika hilo kwa miaka 10 (2005 hadi 2015), Dar es Salaam juzi.
Kaimu Postamasta Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania (TPC), Fortunatus Kapinga, akizungumza na waandishi wa habari, jijini Dar es Salaam juzi.
Ofisa Uhusiano Mwandamizi wa Shirika la Posta Tanzania (TPC), Wilfred Miigo, akizungumza wakati wa mkutano huo.
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano cha Shirika la Posta Tanzania (TPC), Elia Madulesi, akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari wakati wa mkutano huo.
Mkuu wa Kitengo cha Mfumo wa Mawasiliano cha TPC, David Mtake, akijibu moja ya maswali ya waandishi wa habari, wakati wa mkutano huo.
Baadhi ya waandishi wa habari wakimsikiliza Kaimu Postamasta Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania (TPC), Fortunatus Kapinga, alipokuwa akizungumzia kuhusu mafanikio ya shirika hilo kwa miaka 10 (2005 hadi 2015), Dar es Salaam juzi. (Picha zote na Kassim Mbarouk-www.bayana.blogspot.com)
UTANGULIZI:
Kwa kuzingatia mafanikio ya
Serikali katika kipindi cha miaka kumi, Shirika la Posta Tanzania (TPC) ambalo liko
chini ya Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia (MCST), limeshiriki na
kuchangia kikamilifu mafanikio haya yenye lengo mahsusi la kuleta maendeleo ya
haraka kwa wananchi na hatimae kuifanya Tanzania kuwa nchi ya uchumi wa kati
ifikapo mwaka 2025 (vision 2025). Katika
kipindi cha miaka kumi (TPC) imefanikiwa katika maeneo kadha ikiwa ni pamoja na
kupanua wigo na kuanzisha huduma mpya na za kisasa, kongeza ubora wa huduma na
matumizi ya teknolojia ya habari na mawasiliano, kukidhi mahitaji ya soko la
mawasiliano na kukabiliana vyema na ushindani.
MIPANGO
YA SHIRIKA:
Mafanikio haya yalitokana na
utekelezaji wa mipango mkakati ya kibiashara ya miaka mitatu mitatu ya kuanzia
mwaka 2005 hadi 2007, 2008 hadi 2010 na
2011 hadi 2013. Kwa hivi sasa Shirika linatekeleza Mpango Kabambe
(Master Plan) wa kuanzia mwaka 2014 hadi 2023 ambao umelenga kujiimarisha zaidi
katika huduma zinazotumia miundombinu ya anuani za makazi (physical platform),
teknolojia ya digitali (digital platform) na huduma za kisasa za fedha (on-line
payment platform).
MIUNDOMBINU
YA SHIRIKA:
Shirika la Posta Tanzania limeendelea
kuwa ni Taasisi ya kitaifa yenye mtandao mpana zaidi nchini (physical network)
wa kutolea huduma zake na uwakala wa taasisi nyingine muhimu kiuchumi.
Mtandao huu uliounganishwa na
ofisi za Posta Duniani zipatazo 660,000 ni pamoja na:- Ofisi za Posta kamili
(DPO) – 164, Ofisi za Posta Wakala (FPO) 86, Vituo vya Wakala (SPO) - 36,
Masanduku ya barua – 173000, Vibali vya kuuza bidhaa za Posta – 2637 na Mifuko
ya kupokelea barua – 212.
Kutokana na kupanuka na
kuboreshwa mfumo wake wa usambazaji wa lojistiki, Shirika lilitekeleza kwa
mafanikio majukumu ya kitaifa ikiwa ni pamoja na chaguzi kuu za mwaka 2005 na
2010 pamoja na sensa ya watu na makazi iliyofanyika mwaka 2012.
MATUMIZI
YA TEHAMA:
Shirika lilifanikiwa kutekeleza
miradi mbali mbali ya matumizi ya TEHAMA ili kuongeza ubora wa huduma zake. Hii ni
pamoja na mifumo ya kimataifa ya ‘International Postal System’ (IPS); International ‘Financial System’ (IFS); Mfumo wa kitaifa wa Kaunta (Counter Automation)
na kuunganisha ofisi za Posta kwenye Mkongo wa Taifa. Kwa hivi sasa ofisi 28 zimeunganishwa kwenye
mkongo na tunataarajia ofisi nyingine 65 zitakuwa zimeunganishwa kupitia mkongo
unaojengwa na Kampuni ya VIETTEL ya Vietnam kabla ya mwisho wa mwaka huu.
Kutokana na uanzishwaji wa
mfumo wa IPS, kwa hivi sasa wateja
wanafuatilia mwenendo wa bidhaa zao kwa wakati na mahali popote ili kujua
zilipo kwa kutumia tovuti ya Shirika.
Kuhusu mfumo wa IFS Watanzania wanatuma au kutumiwa fedha katika nchi za
Kenya, Uganda, Rwanda, Burudi, Comoro na Zimbabwe.
Katika ngazi ya kitaifa, Shirika
limeanzisha na kuboresha moduli za mfumo wa “Postglobal” ambao unawezesha
wateja kufuatilia mwenendo wa bidhaa zao
ndani ya nchi (track & trace). Shirika pia limepanua huduma ya kukusanya na
kufanya malipo kwa niaba ya wateja (PostGiro) ambapo kwa mfano, huduma hii inatumika
kuuza hisa, kulipa hisa, gawio na pesheni
za wastaafu mahali popote hapa nchini kwa wateja wa Taasisi za NSSF, NIC, PSPF,
TCC, n.k. Kwa hivi sasa ofisi 112 zimeunganishwa
katika mfumo huu wa Post Global na ifikapo mwishoni mwa mwaka ahuu ofisi 147
zitakuwa zimeunganishwa.
HUDUMA
MTANDAO
Chini ya usimamizi wa WMST,
Shirika pamoja na Taasisi ya Teknolojia
cha Dar es Salaam (DIT) linatoa huduma za elimu mtandao (e-education) na
mikutano mtandao (e-conference) katika ofisi za Posta za Bagamoyo, Zanzibar, Arusha,
Morogoro, Mwanza na Mbeya. Aidha,
kwa kushirikiana na Umoja wa Mawasiliano Duniani (ITU), vimejengwa vituo vitatu
vya Kilosa, Wete na Masasi ikiwa ni mradi wa majaribio wa huduma za ki-intaneti
(internet based services).
Lengo ni kuanzisha huduma za
kisasa za Posta ikiwa ni pamoja na ‘hybrid mail’ na ‘internet shopping’.
HUDUMA
ZA UWAKALA
Shirika lilipanua huduma za
uwakala hususan wa Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA) kwa kutumia mfumo wa
‘Rack System’ ambapo kila mwaka zaidi ya watahiniwa 100,000 waliosambaa nchini
kote wamerahisishiwa ulipaji wa ada za
usajili wa mitihani.
Shirika pia limeongeza huduma
za uwakala wa kibenki kupitia Benki ya Posta na CRDB katika ofisi za Posta
zilizoko wilayani. Hivi sasa, Ofisi za
Posta 56 zinatoa huduma za uwakala wa CRDB, lengo ni kufikia ofisi zenye
uwakala zaidi ya 100 ifikapo mwishoni mwa 2016.
Aidha, ofisi za Posta 158 zinatoa huduma za uwakala wa Benki ya
Posta. Katika dhana hiyo ya uwakala,
Shirika linatarajia kuanza uwakala na ECO BANK kwa upande wa ATM za benki hiyo
na pia Shirika litaendesha uwakala wa NMB kupitia vifaa vya MAXCOM.
Aidha, kutokana na mtandao
mpana Shirika pia lintoa huduma za uwakala kwa makampuni mbalimbali ikiwa ni
pamoja na TANESCO (luku), makampuni ya simu, vingamuzi n.k.
MFUMO
NA ANUANI ZA MAKAZI:
Chini ya usimamizi wa Wizara ya
Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia (WMST) na TCRA, utekelezaji wa mfumo mpya wa
Anuani za makazi na misimbo ya Posta (Post Code) ambao umelenga kila mwananchi
kuwa na anuani inayomtambulisha umechochea Shirika katika kuhudumia vizuri wananchi. Postikodi ni mfumo wa anuani unaotumia
utambulisho maalum katika kumfikishia mteja barua, nyaraka, kifurushi na kipeto
kwenye makazi/ofisini kwake. Shirika
limeanza kuendesha huduma zake kwa majaribio kupitia mfumo huu katika miji ya
Arusha na Dodoma. Kwa uzoefu uliopo wa
kuendesha huduma za EMS na p-Cum, Shirika limejiandaa vyema kuhakikisha kuwa Watanzania
wote wananufaika na mfumo huu.
UBORA
WA HUDUMA
Katika kipindi cha miaka kumi
Shirika limeongeza ubora na huduma zake hasa kwa kupanua wigo wa usafirishaji/usambazaji
unaofanyika na usiku kucha kwa kutumia magari yake (OMDS). Kwa hivi sasa bidhaa na nyaraka za wateja
katika sehemu kubwa ya nchi yetu zinafikishwa haraka na salama zaidi ndani ya
siku moja.
Kuhusu huduma bora katika ngazi
za kimataifa Umoja wa Posta Duniani (UPU) umeweka mfumo wa kupima utoaji huduma
kwa Posta zote Duniani
katika upimo uliofanyika mwaka
2012, Shirika la Posta Tanzania lilifanikiwa kupata daraja la tatu, ambalo ni
shaba. Ushindi huu ni uthibitisho kuwa
Shirika linatoa huduma bora na ni kichocheo ili katika miaka ijayo Shirika liweze kupata
daraja A, ambalo ni dhahabu.
RASILIMALI
WATU
Kwa upande wa rasilimali watu katika
ngazi ya kitaifa Shirika lilitunukiwa tuzo ya mwajiri bora wa mwaka 2012,
iliyokabidhiwa na Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho
Kikwete. Tuzo hiyo ilizingatia sera nzuri
ya utawala bora, ambayo inatoa fursa na uwazi katika kutoa ajira kwa watanzania
wa makundi yote wakiwemo wanawake na walemavu.
HITIMISHO
Pamoja na matokeo mengine
muhimu, matokeo halisi ya dhamira ya Shirika ni kuhakikisha kuwa Watanzania wanafaidika
na matunda ya huduma bora na za kisasa za mawasiliano ya Posta ambayo ni pamoja
na kuwarahisishia upatikanaji wa huduma za kibiashara na fedha (financial
inclusion), Elimu, Afya bora, kuwaongezea kasi katika matumizi ya Sayansi na Teknolojia,
kuwapunguzia umaskini na kwa ujumla kuwarahisishia uendeshaji wa maisha yao ya
kila siku.
Imetolewa na:
Ofisi ya Postamasta Mkuu
Shirika la Posta Tanzania
8 Mtaa wa Ohio/Ghana
S.L.P. 9551
11300DAR ES SALAAM.
Simu: 0684 88 75 61
0684 88 79 60

No comments:
Post a Comment