*Yumo Mkurugenzi wa Mkurugenzi wa Uchaguzi
Rais Jakaya Kikwete
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amefanya
mabadiliko ya Utendaji katika Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kwa kumteua Ndugu
Kailima Ramadhani Kombwey kuwa Mkurugenzi wa Uchaguzi.
Aidha,
Rais Kikwete amemteua Jaji Richard Mziray kuwa Jaji wa Mahakama ya Rufani ya
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Vile
vile, Rais Kikwete amewateua majaji wapya 13 wa Mahakama Kuu ya Tanzania.
Taarifa
iliyotolewa leo, Jumamosi, Julai 25, 2015 na Ofisi ya Katibu Mkuu Kiongozi,
Balozi Ombeni Sefue mjini Dar es Salaam inasema kuwa teuzi hizo zote zimeanza leo
hii.
Kwa
mujibu wa taarifa ya Balozi Sefue, Ndugu Kombwey ambaye anaapishwa baadaye leo
jioni, anachukua nafasi ya aliyekuwa Mkurugenzi wa Uchaguzi, Ndugu Julius
Benedicto Mallaba.
Badala
yake, Rais Kikwete amemteua Bwana Mallaba kuwa Jaji wa Mahakama Kuu ya
Tanzania. Kabla ya uteuzi wake, Bwana Kombwey alikuwa Mkurugenzi wa Utawala,
Tume ya Uchaguzi.
Taarifa
hiyo pia imesema kuwa Jaji Mziray ambaye anateuliwa kuwa Jaji wa Mahakama ya
Rufani ya Tanzania kwa sasa ni Jaji wa Mahakama Kuu, Dar es Salaam.
Majaji
wa Mahakama Kuu ambao wameteuliwa na Rais Kikwete, kwa mujibu wa taarifa hiyo, Ndugu
Ignas Pius Kitusi ambaye ni Msajili Mkuu, Mahakama ya Tanzania, Ndugu Wilfred
Peter Dyansobera ambaye ni Naibu Msajili, Mahakama Kuu; Ndugu Lameck Michael
Mlacha ambaye ni Naibu Msajili na Mwenyekiti wa Baraza la Rufani la Kodi; Ndugu
Salima Mussa Chikoyo ambaye ni Naibu Msajili, Mahakama Kuu, Divisheni ya Kazi; Ndugu
Isaya Arufani ambaye ni Naibu Msajili na Katibu wa Jaji Mkuu wa Tanzania na
Ndugu Julius Benedicto Mallaba.
Wengine
ni Ndugu Adam Juma Mambi ambaye ni Katibu Msaidizi, Tume ya Kurekebisha Sheria;
Ndugu Sirilius Betran Matupa ambaye kwa sasa ni Msaidizi wa Rais, Sheria, Ofisi
ya Rais, Ikulu; Ndugu Issa Maige ambaye ni wakili wa kujitegemea, Ndugu Licia
Gamunya Kairo ambaye ni wakili wa kujitegemea; Dkt. Masoud Shaaban Benhaji
wakili wa kujitegemea na Mhadhiri Mwadamizi, Chuo Kikuu Huria, Dar es Salaam, Ndugu
Victoria Makani ambaye ni wakili wa kujitegemea na Ndugu Rehema Joseph Kerefu
ambaye ni mwanasheria wa Jumuia ya Afrika Mashariki.
Taarifa
hiyo imesema kuwa wakati Ndugu Kombwey anaapishwa leo, majaji wataapishwa
katika tarehe itakayotangazwa baadaye.
Imetolewa na:
Kurugenzi
ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR ES SALAAM.
25
Julai, 2015


No comments:
Post a Comment