TANGAZO


Tuesday, July 28, 2015

Lowassa aingia Ukawa, ahamia Chadema

Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Juma Duni Hajji akiwasili kwenye Hoteli ya Bahari Beach katika mkutano wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), wa kumpokea Waziri Mkuu mstaafu, Edward Lowassa wakati alipotangaza kung'atuka kwenye Chama chake cha Mapinduzi (CCM), Dar es Salaam leo. (Picha zote na Kassim Mbarouk-www.bayana.blogspot.com)
Baadhi ya wanachama na viongozi wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), wakiwa katika mkutano wa kumpokea Waziri Mkuu mstaafu, Edward Lowassa wakati alipotangaza kung'atuka kwenye Chama chake cha Mapinduzi (CCM) na kujiunga na umoja huo, kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadem) jijini Dar es Salaam leo. 
Mtoto wa Waziri Mkuu mstaafu, Edward Lowassa (wa pili kushoto), akiwa katika mkutano wa kumkabidhi kadi baba yake, mara baada ya kutangaza kung'atuka CCM na kujiunga na Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadem), Dar es Salaam leo. 
Mwanachama mpya wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Waziri Mkuu mstaafu, Edward Lowassa, akiingia kwenye ukumbi wa mikutano pamoja na Wenyeviti wenza wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), wakati alipotangaza kung'atuka kwenye chama chake cha CCM na kujiunga na Chadema, kupitia umoja huo.  
Mwanachama mpya wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Waziri Mkuu mstaafu, Edward Lowassa, akiingia kwenye ukumbi wa mikutano pamoja na Wenyeviti wenza wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa). 
Mwanachama mpya wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Waziri Mkuu mstaafu, Edward Lowassa (wa tatu kulia), akiwa na Wenyeviti wenza wa umoja wa Ukawa, James Mbatia (kushoto) wa NCCR-Mageuzi, Freeman Mbowe (wapili) wa Chadema na Profesa Ibrahim Lipumba (kulia) wa CUF, wakati alipojiunga rasmi na chama hicho, kupitia Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), jijini Dar es Salaam leo.
Mwenyekiti Mwenza wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), James Mbatia wa NCCR-Mageuzi, akisalimia wanachama wa umoja huo. 
Mwenyekiti Mwenza wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), Profesa Ibrahim Lipumba wa CUF, akisalimia wanachama wa umoja huo.
Mwanachama mpya wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Waziri Mkuu mstaafu, Edward Lowassa, akiwapungia wanachama wa Vyama vya Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), wakati alipotangaza kungatuka kwenye chama chake cha CCM na kujiunga na Chadema, kupitia umoja huo. 
Mwanachama mpya wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Waziri Mkuu mstaafu, Edward Lowassa (katikati), akiwa na Wenyeviti wenza wa umoja wa Ukawa, James Mbatia (kushoto) wa NCCR-Mageuzi, Freeman Mbowe (wapili) wa Chadema na Profesa Ibrahim Lipumba (kulia) wa CUF, wakati alipojiunga rasmi na chama hicho kupitia Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa).
Mwanachama mpya wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Waziri Mkuu mstaafu, Edward Lowassa, akizungumza na waandishi wa habari, Dar es Salaam leo, wakati alipojiunga rasmi na chama hicho kupitia Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa). Kulia ni Wenyeviti wenza wa umoja huo, James Mbatia wa NCCR-Mageuzi, Freeman Mbowe wa Chadema, Profesa Ibrahim Lipumba wa CUF na Emmanuel Makaidi wa NLD.
Waziri Mkuu mstaafu, Edward Lowassa, akizungumza na waandishi wa habari pamoja na viongozi wa Vyama vya Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), wakati akitangaza kung'atuka kwenye Chama chake cha CCM jijini leo. 
Baadhi ya waandishi wa habari, wakichukua picha wakati Waziri Mkuu mstaafu, Edward Lowassa, akitangaza kung'atuka kwenye Chama chake cha CCM jijini leo.  
Waziri Mkuu mstaafu, Edward Lowassa, akizungumza na waandishi wa habari pamoja na viongozi wa Vyama vya Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), wakati akitangaza kung'atuka kwenye Chama chake cha CCM jijini leo.
Baadhi ya wanachama wa Chadema na umoja wa Ukawa, wakifurahia hatua ya Waziri Mkuu mstaafu, Edward Lowassa, kung'atuka kwenye Chama chake cha CCM jijini leo. 
Waziri Mkuu mstaafu, Edward Lowassa, akizungumza na waandishi wa habari pamoja na viongozi wa Vyama vya Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), wakati akitangaza kung'atuka kwenye Chama chake cha CCM jijini leo.
Waziri Mkuu mstaafu, Edward Lowassa, akipongezwa na Mwenyekiti mwenza wa Ukawa, Profesa Lipumba wa CUF. 
Waziri Mkuu mstaafu, Edward Lowassa akikumbatiwa na mkewe, Regina Lowassa mara baada ya kutangaza kung'atuka katika chama chae cha CCM leo.
Wenyeviti wenza wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), Wenyeviti wa Vyama vya NCCR-Mageuzi, James Mbatia (kushoto), Freeman Mbowe (wa pili kushoto) wa Chadema, Profesa Ibrahim Lipumba (wa nne) wa CUF na Emmanuel Makaidi (kulia) wa NLD, wakiwa na mwanachama mpya wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), mmoja wa watia nia aliyekatwa na Chama Cha Mapinduzi (CCM), Waziri Mkuu mstaafu, Edward Lowassa (katikati), wakati alipokabidhiwa kadi ya chama hicho na kuzungumza na waandishi wa habari, Dar es Salaam leo.
Mke wa Waziri Mkuu mstaafu, Regina Lowassa akiwa na mtoto wake (kulia), wakati wa mkutano huo. 
Waziri Mkuu mstaafu, Edward Lowassa (kushoto), akiteta jambo na mmoja wa Wenyeviti wenza wa Ukawa, Profesa Ibrahim Lipumba wa CUF, wakati wa ,kutano huo.


Waziri Mkuu mstaafu, Edward Lowassa, akijibu maswali ya waandishi wa habari wakati wa mkutano huo.
Waziri Mkuu mstaafu, Edward Lowassa, akijibu maswali mbalimbali ya waandishi wa habari wakati wa mkutano huo. 
Waziri Mkuu mstaafu, Edward Lowassa, akijibu maswali mbalimbali ya waandishi wa habari wakati wa mkutano huo.  
Mke wa Waziri Mkuu mstaafu, Regina Lowassa akikabidhiwa kadi ya Chadema na Mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe.
Mke wa Waziri Mkuu mstaafu, Regina Lowassa akiionesha kadi yake ya Chadema mara baada ya kukabidhiwa na Mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe. 
Waziri Mkuu mstaafu, Edward Lowassa, akikabidhiwa kadi ya uanachama wa Chadema na Mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe. Kulia ni mke wake, Regina Lowassa akiwa na kadi yake baada ya kukabidhiwa. 
Waziri Mkuu mstaafu, Edward Lowassa na mkewe, Regina Lowassa wakizionesha kadi zao mara baada ya kukabidhiwa na Mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe (kushoto), Dar es Salaam leo.
Waziri Mkuu mstaafu, Edward Lowassa na mkewe, Regina Lowassa wakizionesha kadi zao mara baada ya kukabidhiwa na Mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe (katikati), Dar es Salaam leo. 
Waziri Mkuu mstaafu, Edward Lowassa akipongezwa na Mwenyekiti wa Chama cha NLD, Emanuel Makaidi mara baada ya kukabidhiwa kadi na Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe.
Mwenyekiti mwenza wa Ukawa, Profesa Ibrahim Lipumba wa CUF, akijibu maswali ya waandishi wa habari, wakati wa kutano huo. 
Mwenyekiti mwenza wa Ukawa, Mwenyekiti wa Chama cha NLD, Emanuel Makaidi, akijibu maswali ya waandishi wa habari, wakati wa ,kutano huo. 
Mwenyekiti mwenza wa Ukawa, Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe, akijibu maswali ya waandishi wa habari, wakati wa kutano huo.  
Wenyekiti wenza wa Ukawa, wakipiga makofi pamoja na mwanachama mpya wa Chadema, Waziri Mkuu mstaafu, Edward Lowassa, wakati wa kutano huo.   
Baadhi ya waandishi wa habari wakiwa katika mkutano huo. 
Mwenyekiti mwenza wa Ukawa, Mwenyekiti wa Chama cha NLD, Emanuel Makaidi, akizungumza wakati wa kutano huo.  
Makamu Mwenyekiti wa Chama cha CUF, Juma Duni Haji, akizungumza wakati wa kutano huo.  
Mwenyekiti mwenza wa Ukawa, Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi, James Mbatia akizungumza wakati wa kutano huo.  
Baadhi ya waandishi wa habari wakiwa katika mkutano huo.  
Mwenyekiti mwenza wa Ukawa, Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe, akizungumza, wakati wa kutano huo.

No comments:

Post a Comment