TANGAZO


Thursday, July 23, 2015

Kombe la Kagame: LLBA ya Burundi yailaza APR ya Rwanda bao 1-0 Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam

Golikipa wa timu ya APR ya Rwanda, Ndoli Claude, akiruka juu kudaka mpira uliokuwa umeelekezwa langoni mwake, wakati timu hiyo ilipopambana na LLBA FC ya Burundi, katika michuano ya Kombe la Kagame, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam leo. LLBA FC ilishinda bao 1-0. (Picha zote na Kassim Mbarouk-www.bayana.blogspot.com)
Beki wa APR, Rwatubyaye Abdoul akizuiya mpira uliokuwa ukiwaniwa na Ndarusanze Claude wa LLB FC.
Rusheshangoga Michel wa APR akiumiliki mpira huku akifuatwa na Ndarusanze Claude wa LLB FC.
Rusheshangoga Michel wa APR na Ndarusanze Claude wa LLBA FC, wakipambana kuwania mpira
Niyonkuru Pascal wa LLBA FC (kati) na Sekamana Maxime (10), wa APR, wakiruka juu kuupiga mpira kichwa wakati wa mchezo huo.
Rusheshangoga Michel wa APR, akiufuata mpira uliokuwa ukidhibitiwa na Murutabose Emedy (kulia) wa LLBA FC.
Kiza Fataki wa LLBA FC akipiga mpira huku akikabiliwa na Rusheshangoga Michel wa APR.
Rusheshangoga Michel wa APR, akijaribu kumzuia Murutabose Emedy wa LLBA FC ya Burundi.
Golikipa wa timu ya APR ya Rwanda, Ndoli Claude, akiudaka mpira uliopigwa na Murutabose Emedy (kulia) wa LLBA FC ya Burundi.

Mchezaji Ndarusanze Claude wa LLBA ya Burundi, akiufuata mpira uliokuwa umedhibitiwa na Rwatubaye Abdoul wa APR ya Rwanda wakati wa mchezo wa Kombe la Kagame, uliofanyika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam leo.  LLBA ilishinda bao 1-0. 
Mchezaji Ndarusanze Claude (kushoto) wa LLBA ya Burundi, akiudhibiti mpira huku akizongwa na Rwatubaye Abdoul wa APR. 


Rusheshangoga Michel wa APR, akiudhibiti mpira huku akizongwa na Ndarusanze Claude wa LLB FC.
Mchezaji Ndarusanze Claude (kushoto) wa LLBA ya Burundi (kulia), akiruka juu na Nsabimana Eric wa APR kuwania kuupiga kichwa mpira.

No comments:

Post a Comment