Zaidi ya wanachama 18 wa kundi la waasi la FARC wameuawa katika shambulio la angani nchini Colombia.
Shambulio hilo lililotokea kusini magharibi mwa eneo la Cauca, ni baya zaidi tangu mashambulizi ya angani yaliporejelewa tena, dhidi ya waasi hao mwezi uliopita.
Rais Juan Manuel Santos, alianzisha tena mashambulio hayo baada wanajeshi kumi na moja kuviziwa na kuuawa na waasi hao.
Pande zote mbili zimekuwa zikishauriana tangu mwaka 2012, kujaribu kumaliza uhasama huo, uliodumu zaidi ya nusu karne nchini Colombia.
No comments:
Post a Comment