TANGAZO


Friday, May 22, 2015

Wafanyabiashara washauriwa kutumia mashine za EFD

Mkurugenzi  Mkuu na Muasisi  wa Kampuni ya Compulynx Tanzania Bw.Sailesh Savani akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam alipokuwa akikabidhi Hundi kwa mtunzi wa wimbo wa kampuni hiyo  Kanda ya  Afrika Mashariki. (Picha zote na Beatrice Lyimo – MAELEZO)
Mkurugenzi wa Kanda ya Afrika Mashariki wa Kampuni ya Cumpulynx Tanzania) Bw. James Alvan (wa kwanza kushoto)  akifafanua jambo kuhusu mashine za Eletronic Fiscal Device(EFD) zinazosambazwa na Kampuni hiyo kwa Tanzania.
Mkurugenzi  Mkuu na Muasisi  wa Kampuni ya Compulynx Tanzania Bw. Sailesh Savani (kushoto) akikabidhi hundi kwa mshindi wa shindano la ubunifu kwa  wafanyakazi wa kampuni hiyo kwa Afrika Mashariki  Bw.Tulizo Kaduma (Kulia) na katikati ni Afisa Biashara wa Kampuni hiyo Bi. Genesis Mwaipopo.

Na Beatrice Lyimo- Maelezo.
KAMPUNI  ya COMPULYNX  Tanzania inayoshughulika na usambazaji wa mashine za Electronic Fiscal Device (EFD) imewashauri wafanya biashara nchini kutumia mashine hizo ipasavyo kwani husaidia kukuza pato la Taifa. 

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi  Mtendaji wa kampuni hiyo Bw Sailesh Savani wakati akiongea na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam.
“Wafanyabiashara wasiwe waoga kutumia mashine za EFD kwani huleta uhalali wa pande zote mbili ikiwemo Serikali na wafanyabiashara hivyo kupelekea maendeleo ya nchi kwani kodi zitakusanywa kihalali” aliongeza Bw Savani.

Ameongeza kuwa mashine hizo husaidia kuweka kumbukumbu wa mfumo mzima wa biashara hivyo kuwasaidia wafanyabiashara kujua mapato na ulipaji wa kodi unaofanyika kihalali na kupelekea Serikali kujua mapato yapatikanayo nchini.

“Ukwepaji wa kulipa kodi umechangia maendeleo duni katika sekta ya Miundo mbinu pamoja na ukosefu wa huduma za jamii zikiwemo Maji, Hospitali na Elimu bora nchini”, alifafanua Mkurugenzi huyo.
Mbali na hayo kampuni hiyo inafanya shughuli mbalimbali zikiwemo kusambaza mitambo ya kieletroniki inayosaidia kukamata wahalifu katika maeneo mbali mbali ya biashara ikiwepo benki na maduka makubwa.

Pia kampuni hiyo ilifanya mashindano ya uimbaji iliyowashirikisha nchi tatu ikiwemo Tanzania, Kenya na Uganda na kumtangaza Bw. Tulizo Kaduma kutoka Tanzania kuwa mshindi wa shindano hilo. 

No comments:

Post a Comment